KISWAHILI USHAIRI NOTES WITH EXAMPLES AND GUIDES

MWONGOZO WA USHAIRI

USHAIRI WA 1

Soma shairi lifuatalo kwa makini halafu ujibu maswali yanayofuata

  1. Naja sasa ni ndiyani, naja kwetu Mzalendo

Naja nirudi nyumbani, nilowekwa nako kando

Kwetu’ mi nakutamani, kulo na mwingi uhondo

Nijaye ni yule nyundo, misumari hadharini

You did not find what you wanted? Worry not. Just search for more notes and other learning/teaching materials, below. Simply type in the box below and click on the search button.

[ivory-search id=”14715″ title=”Default Search Form”]

  1. Naja kwingine kuwapi, kulojaa langu pendo?

Huenda nende kwinginepi, sawa nako kwa muundo?

Kaa kwingine anapi, ela kwenye lakwe gando?

Nijaye ni ile nyundo, misumari hadharini

 

  1. Naja nije rudi papo, panigedeme mgando

Ningaambwa kwetu hapo, kwamba kwanuka uvundo

Sitakwenda penginepo, tarudi kuko kwa mwando

Nijaye ni ile nyundo, misumari hadharini

 

  1. Naja sitapakimbiya, ningambwa kuna vimondo

‘Takuja kuvilekeya, vinganijiya kwa vundo

nilipozawa tafiya, sikimbii kwenda kando

nijaye ni ile nyundo, misumari hadharini

 

  1. Naja hiwa ‘mekomaa, kuzidi nilivyo mwando

Tena n’najiandaa, kwa fikira na vitendo

Kwetu nije kuifaa, na kuitiliya pondo

Nijaye ni ile nyundo, misumari hadharini

 

  1. Naja na ingawa naja, siwaeki mifundo

Moyo wangu ushatuja, mawi nalotendwa mwando

Ela wataoningoja, na vyao viwi vitendo

Nijaye ni ile nyundo, misumari hadharini

 

  1. a) Eleza jinsi ‘uzalendo’ wa mshairi unavyojitokeza katika beti za 1 na 2         alama 4
  2. Fafanua jazanda zinazopatikana katika mshororo:

Kaa kwingine anapi, ela kwenye lakwe gando?                                             alama 2

  1. Andika ubeti wa tatu katika lugha nathari alama 4
  2. (i) Katika ubeti wa 5 mshairi amebadilika Eleza                                           alama 2

(ii)   Ananuia kufanya nini pindi arudipo?                                                      Alama 2

  1. Eleza ujumbe unaopatikana katika ubeti wa 6 alama  2
  2. Andika maneno haya katika kiswahili sanifu alama  2
    1. Mwando
    2. Ningambwa
  3. Kibwagizo cha shairi kinampa sifa gani mshairi? Alama 2

 

MWONGOZO WA KUSAHIHISHA SHAIRI WA 1

 

7)   `UZalendo’

(i)   Anarudi kwao

(ii)  Anapenda kwao

(iii)Anatamani kwao

(iv) Nyumbani kunamlisha

(v) Ndiko kuna uhondo

(vi) Hawezi kulinganisha kwao na kwingine                                                              zozote 4 x 1 4

  1. b) Jazanda

(i)   Anajilinganisha na kaa na angeishi baharini mahali pakubwa

(ii)Kaa ana lile gando, kile kifaa anachokitumia kupatia chakula na vile vile kama silabi, paini nyumba ambapo pana chakula na usalama au mtu kwao ni kwao ndipo pampapo riziki/  ussalama na utulivu

2×1 = 2

  1. c) Lugha Nathari

(i)    Ninarudi  hapo kwetu

(ii) Hata nikiambiwa pananuka

(iii)  Siendi pengine narudi hapo tu

(iv)  Nyundo/ Mjuzi/ Bingwa/ Shujaa/ Mweledi/ Stadi ninakuja misumar jihadhari  alama 4 x 1 = 4

  1. d) (i) Amekomaa zaidi anajiandaa kwa fikira na vitendo                                                     alama 2

(ii) Kuifaa nchi yake kuleta maendeleo /kurekebisha kujenga mji/ kuondoa uhasama      alama 2

  1. (i) Yeye hana kinyongo anapokuja (lakini kwa waliomtenda na wale wanaomngojea kwa maovu atapambana nao)                                                                                                                 alama 2
  2. f) (i) Mwando – Mwanzo

(ii) Ningambwa – Ningeambiwa                                                                                         2×1 =2

  1. g) sifa inayopatikana katika shairi kuhusu mhusika

(i)  hajabadilika (ni ile nyundo / bado yu tayari)

(ii) bado yu tayari kupambana na matatizo na anaweza/ mtekelezi                            2 x 1 = 2

 

USHAIRI WA 2

Soma shairi hili kisha ujibu maswali.

 

Jukwani naingia, huku hapa pasokota,

Kwa uchungu ninalia,hii tumbo nitaikata,

Msiba mejiletea,nimekila kiso takata,

We tumbo nitakupani,uwe umetosheka?

 

Wazee hata vijana,wote umewasubua,

Huruma nao hauna,heshima kawakosea,

Ukambani na Sagana,hata mbwa wararua,

We tumbo nitakupani,uwe umetosheka?

 

Wahasibu ofisini,kibwebwe mejifunga,

Miaka mingi vitabuni,ili wasikose unga,

Nadhari wanadhamini,hesabu wanazirenga,

We tumbo nitakupani, uwe umetosheka?

 

Wapenzi wa kiholela,pia wanakuogopa,

Baada yao kulala, wana wao wanatupa,

Wakihitaji chakula,wanachokora mapipa,

We tumbo nitakupani,uwe umetosheka?

 

Wafugaji hata nao,kama dawa wakwamini,

Hawajali jiranio,wamesusia amani,

Wanaiba ng’ombe wao,na kuzua kisirani,

We tumbo nitakupani,uwe umetosheka?

 

Nayo mizozo ya maji, kaonekana kwa mara,

Hiyo nayo ni dibaji,sababu sio harara,

Njaa wahepe wenyeji, huo ndio mkarara,

We tumbo nitakupani,uwe umetosheka?

 

Ningeweza kukuuza,ingekuwa siku njema,

Tena kwa bei ya meza,sokoni nimesimama,

Wala tena singewaza,kuhusu wali na sima,

We tumbo nitakupani,uwe umetosheka?

 

Hatima umefikika,naenda zangu nikale,

Mate yanidondoka,kwa mnukio wa wale,

Naomba kwenda kukaa,wala sio nikalale,

We tumbo nitakupani,uwe umetosheka?

Maswali

  • Lipe anwani mwafaka shairi hili.                                                                                   (Alama 2)
  • Shairi hili ni la aina gani? Toa sababu.                                                                           (Alama 2)
  • Huku ukitolea mifano mwafaka, taja arudhi zilizotumiwa katika ubeti wa tatu. (Alama 4)
  • Andika ubeti wa nne kwa lugha nathari. (Alama 4)
  • Thibitisha kuwepo kwa idhini ya ushairi. (Alama 2)
  • Taja madhila anayoelezea mtunzi wa shairi hili yaletwayo na tumbo. (Alama 4)
  • Elezea maana ya maneno yafuatayo. (Alama 2)

(a) Dibaji

(b) Harara

 

MWONGOZO WA KUSAHIHISHA USHAIRI WA 2

  1. i) –           Tumbo lisilotosheka

–           Matatizo ya tumbo                                                                                          2×1=2

  1. ii) –           Tarbia- mishororo minne                                                                                 2×1=2

iii)        –           Mishororo

  • Vina vya kati (ni) na vya mwisho (nga)
  • Vipande viwili- utao na ukwapi
  • Kibwagizo
  • Mizani (urari wa mizani ukwapi 8 na utao 8) jumla 16                         4×1=4
  1. iv) – Wapendanao mapenzi yasiyo na dhati wanakuogopa. Wapatao mimba, watoto wao hawajali. Watoto watakapo chakula huwa wanatafuta mapipani. Tumbo nikupe nini ili utosheke?

4×1=4

  1. v) – Kukosa heshima- hata mbwa wararua

–           Ufisadi- hesabu wanazirenga

–           Kutowajibikia wana- wanachokora mapipa

–           wizi- wa ng’ombe

–           Mizozo/ kutoelewana- mradi waliepe njaa                                                      4×1=4

  1. vi) – Dibaji- Thibitisho/ uhalali

Harara- hasira/ hamaki                                                                                    2×1=2

 

USHAIRI WA 3

Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali.

  LAU HAKUNA MAUTI. Na Abdalla Said Kizere

  1. Lau dunia nanena, tuseme si ati ati,

Mauti kawa hakuna, katika wote wakati,

Vipi tungelisongana, tunaoishi tiati?

Lau hakuna mauti, vipi tungelisongana?

 

  1. Dunia ingetatana, na kizazi katikati,

Huku kwazaliwa bwana, kule kwazawa binti,

Vipi tungelioana, na kuzaa hatuwati?

Lau hakuna mauti, vipi tungelisongana?

 

  1. Lau mauti hakuna, tungesongana sharuti,

Kwa viumbe kukazana, wanadamu na manyati,

Vipi tungelijazana, kwa kusitawi umati?

Lau hakuna mauti, vipi tungelisongana?

 

  1. Walakini Subuhana, kapanga sisi na miti,

Ili tusizidi sana, si wengi na si katiti

Maisha ya kupishana, yule ende yule keti,

Lau hakuna mauti, vipi tungelisongana?

 

  1. Ndipo dunia kufana, ikawa kama yakuti,

Kwa uwezowe Rabana, kaipanga madhubuti,

Maisha kugawiana, kayagawa kwa mauti,

Lau hakuna mauti, vipi tungelisongana?

 

  1. Njia ingekuwa hapana, pembeni na katikati,

Sote tungeambatana, kama ukosi na shati,

Na njaa ingetutafuna, pa kulima hatupati,

Lau hakuna mauti, vipi tungelisongana?

 

  1. Peleleza utaona, hayataki utafiti,

Kama tungelikongana, ingekuwa ni bahati,

Vipi tungesukumana, katika hiyo hayati?

Lau hakuna mauti, vipi tungelisongana?

 

  1. Mbele sitokwenda tena, hapa mwisho nasukuti,

Yaoleni waungwana, shauri yake Jabaruti,

Yote tuloelezana, katenda bila senti,

Lau hakuna mauti, vipi tungelisongana?

 

MASWALI

  1. a) Je, hili ni shairi la bahari gani? Eleza (alama 2)
  2. b) Eleza vile mwandishi alivyotumia uhuru wa kishairi (alama 4)
  3. c) Eleza umbo la shairi hili (alama 4)
  4. d) Fafanua ujumbe unaojitokeza katika ubeti wa tano (alama 4)
  5. e) Andika majina mawili ya Mungu kwa mujibu wa shairi (alama 2)
  6. f) Kwa kutolea mifano, eleza mbinu mbili za lugha zilizotumiwa katika shairi hili                                                                                     (alama 2)
  7. g) Eleza maana ya maneno yafuatayo kulingana na shairi (alama 2)

(i)   Tiati _________________

(ii)  Shani_________________

 

MWONGOZO WA KUSAHIHISHA USHAIRI WA 3

  1. (i) Tarbia – – mishororo mine

(ii) Pindu  – utao katika mkarara ndio kianzio cha ubeti unaofuatia mf. Ubeti 3

iii) Mtiririko – vina vya kati vinafanana na vya mwisho pia vinafanana katika shairi lote

 

Vya kati                            vya mwisho

na,                                                            ti,

na,                                                            ti,

na,                                                             ti,

ti,                                                   na.

 

(iv)  mathnawi – lina vipande viwili – utao na ukwapi

      

 

  1. b) (i)    Inkisari –kwazawa, ńgekuwa, ńgetutafuna, nanena, sitokwenda
  • Tabdila – Sharuti badala ya sharti
  • Kuboronga sarufi – mauti kawa hakuna – ikiwa hakuna mauti,

– katika wote wakati  – katika wakati wote

  • Lahaja (ya kimvita) – hatuwati (hatuwachi)
  • – yaoleni (yaoneni)

 

  1. c)
  • Beti 8
  • Mishororo 4 katika kila ubeti
  • mizani 16 katika kila mshororo
  • vina vya kati vya mwisho

na,                                     ti,

na,                                     ti,

na,                                     ti,

ti,                                       na.

  • vipande viwili – utao na ukwapi
  • Lina kibwagizo kinarudiwarudiwa “lau hakuna mauti, vipi tungelisongeni

 

  1. d) (i) Dunia haiwezi kujaa watu kupita kiasi

(ii)   Mwenyezi Mungu anajua kupanga

  • Baadhi ya watu wafe na baadhi wazaliwe
  • Bila kifo tungesongamana/jaa sana
  1. e) (i) Subuhana

(ii)   Rabana

(iii)   Jabaruti

 

  1. f) (i) Balagha – k.v  Vipi tungelisongana, tunaoishi tiati?

(ii)   Tashbihi   – ikawa kama ya kuti

  • Kama ukosi na shati

(iii)   Takriri   – si ati ati

  • Lau hakuna mauti, vipi tungelisongana?

 

USHAIRI WA 4

Soma shairi  lifuatalo, kisha ujibu maswali;                                               (alama 20)

Sinisumbuwe akili, nakusihi e mwendani,

Afiya yangu dhahili, mno nataka amani,

Nawe umenikabili, nenende sipitalini,

Sisi tokea azali, twenda zetu mizimuni,

Nifwateni sipitali, na dawa ziko nyumbani?

 

Mababu hawakujali, wajihisipo tabani,

Tuna dawa za asili, hupati sipitalini,

Kwa nguvu za kirijali, mkuyati uamini,

Kaafuri pia kali, dawa ya ndwele Fulani,

Nifwateni sipitali, na dawa ziko nyumbani?

 

Mtu akiwa halali, tumbo lina walakini,

Dawa yake ni subili, au zongo huauni,

Zabadi pia sahali, kwa maradhi yalondani,

Au kwenda wasaili, wenyewe walo pangani,

Nifwateni sipitali, na dawa ziko nyumbani?

 

Mtu kwenda sipitali, ni kutojuwa yakini,

Dakitari k’ona mwili, tanena kensa tumboni,

Visu vitiwe makali, tayari kwa pirisheni,

Ukatwe kama figili, tumbo nyangwe na maini,

Nifwateni sipitali, na dawa ziko nyumbani?

 

Japo maradhi dhahili, kuteguliwa tegoni,

Yakifika sipitali, huwa hayana kifani,

Wambiwa damu kalili, ndugu msaidieni,

Watu wakitaamali, kumbe ndiyo buriani,

Nifwateni sipitali, na dawa ziko nyumbani?

 

Mizimu wakupa kweli, wakueleze undani,

Maradhiyo ni ajali, yataka vitu thamani,

Ulete kuku wawili, wa manjano na kijani,

Matunda pia asali, vitu vyae chanoni,

Nafwatani sipitali, na dawa zi mlangoni?

MASWALI – USHAIRI                                                                               (ALAMA 20)

  1. a) Lipe kichwa mwafaka shairi hili. (alama 2)
  2. b) Mtunzi alikuwa na lengo gani alipotunga shairi hili? (alama 2)
  3. c) Mbona mshairi hataki kwenda hospitali?                                                             (alama 4)
  4. d) Kwa kuzingatia muundo wa shairi hili, eleza mbinu zilizotumika (alama 6)
  5. e) kwa nini mshairi alitumia ritifaa katika ushairi? (alama 2)
  6. f) Andika maana ya maneno yafuatayo yalivyotumika katika shairi (alama 4)
  7. i) Dhahili
  8. ii) Azali

iii) Sahali

  1. iv) Tumbo nyangwe 

MWONGOZO WA KUSAHIHISHA USHAIRI 4

  1. a) i)          Sipitali sendi/ siendi
  2. ii) Udhaifu wa hospitali

iii)        Umaarufu wa miti- shamba

  1. b) i)          Kupigia debe miti- shamba
  2. ii) Kukosoa huduma za hospitali
  3. c) i)          Tangu zamani, wao huenda mzimuni
  4. ii) Madawa ya asili yapo

iii)        Hapendi upasuaji

  1. Mtu anaweza kupoteza maisha
  • Tunafuata kieleleza cha mababu wetu
  1. d) i) Inkisani- tabani, wambiwa
  2. ii) Mazida- Afiya
  • Takhmisa- Mishororo tano
  1. Kibwagizo- Nifwateni sipitali, na dawa ziko nyumbani?
  2. Mtiririko (vina vya kati ni “li” ilhali vya utao ni “ni”
  3. Mizani kumi na sita kwa kila mshororo
  4. e) Inkinsani
  5. f) i) Dhalili- Hafifu, isio na nguvu
  6. ii) Azali- zamani
  • Sahali- Nafuu

Tumbo nyangwe- Utumbo mdogo

 

USHAIRI WA 5

  1. Soma shairi lifuatalo kwa makini kisha ujibu maswali.

Niokoa Muokozi, uniondolee mashaka.

Kuyatukua siwezi, mjayo nimedhikika

Nimekithiri simanzi, ni katika kuudhika

Mja wako nasumbuka, nipate niyatakayo.

 

Mja wako nasumbuka, nataka kwao afua

Nirehemu kwa haraka, nami nipate pumua

Naomba hisikitika, na mikono hiinua

Mtenda ndiwe Moliwa, nipate niyatakayo.

 

Mtenda ndiwe Moliwa, we ndiwe Mola wa anga

Mazito kuyaondoa, pamoja na kuyatenga

Ukauepusha ukiwa, ya pingu zilonifunga

Nikundulia  muwanga, nipate niyatakayo

 

Muwanga nikundulia, nipate toka kizani

Na huzuni n’ondolea, itoke mwangu moyoni

Mambo mema niegheshea, maovu nisitamani.

Nitendea we Manani, nipate niyatakayo.

 

Igeuze  yangu nia, dhaifu unipe mema

Nili katika dunia, kwa afia na uzima

Moliwa nitimizia, yatimize yawe mema

Nifurahike mtima, nipate niyatakayo.

 

  • Shairi hili ni la bahari gani? Eleza. (alama 2)
  • Taja madhumuni ya shairi hili.                                                                 (alama 3)

(c) Eleza muundo wa shairi hili.                                                                      (alama 4)

(d) Thibitisha namna uhuru wa kishairi unaibuka katika shairi.                      (alama 4)

(e) Andika ubeti wa pili katika lugha sufufu.                                                 (alama 4)

(f) Toa maana ya:

  • Nimedhikika
  • Muwanga nikundulia
  • Nifurahike mtima (alama 3)

 

MWONGOZO WA KUSAHIHISHA USHAIRI WA 5

 

  1. a) Pindu- Kifungu katika mshororo wa mwisho wa ubeti kuanza ubeti mpya               1×2=2

 

  1. b) –Kuonyesha kuwa mja hana nguvu

-Amekumbwa na masaibu

-Maombi kwa mola amwokoe na ampe afya

-Mungu amtoe katika giza

-Mungu ampe maisha mema

Zozote 3×1=3 mks

  1. c) Muundo

-Tarbia

-Vina vya kati na vya mwisho

-Mizani

-Kibwagizo

4×1=4 mks

  1. d) Inksari-

-Mjayo; Mja waho

-Nondolea

-Zilonifunga

 

Mazida –Moliwa

 

Tabdila –Afia

 

Kuboronga sarufi –igeuze yangu nia

4×1=4mks

 

  1. e) Kiumbe wako nimeteseka mno. Naomba unipe afueni na unirehemu. Ninaomba nikikusudia. Wewe ndiwe Muumba unayeweza kunipa niyahitajiyo. 4×1=4mks

 

  1. f) i) Nimeteseka au ni taabani
  2. ii) Nimulikie; niletee nuru, nizinduke

iii)      Nichangamke au nistarehe moyoni.

 

USHAIRI WA 6

            Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali.

Wataalamu muwe macho, vuani moto muenge,

Muenge hicho ambacho, cha watu wenye mawenge,

Mawenge yenye kijicho, kiswahili wakivunge,

Barakala tuwapinge, sichafue kiswahili.

 

Sichafue kiswahili, barakala tuwapinge,

Apige kila hali, wasiguse tuwainge,

Tuwainge wende mbali, kiswahili tujijenge,

Barakala tuwapinge, sichafue kiswahili.

 

Sichafue yetu lugha, waharibu Wabanange,

Wabanange iwe nyagha, waiweke tengetenge,

Lugha kuitwa; ulugha, lafidhi watia denge,

Barakala tuwapinge, sichafue kiswahili.

 

 

Tuichange heshima, na ulugha tuupinge,

Tuhifadhi kwa salama, na kisingio unyonge,

Kelele za maamuna, si watu ni visinge,

Barakala tuwapinge, sichafue kiswahili.

 

Kasema sheikh Amri, kiswahili tukisenge,

Kistawi kinawiri, kitumike kwenye bunge,

Hii ni yetu fahari, lugha yetu tuichunge.

Barakala tuwapinge, sichafue kiswahili.

 

Kikipatwa na maradhi, kwa sindano tukidunge,

Kila jama kutidhi, kipatwe hapo tupunge,

Tukitia mfawadhi, kama kunde na kihenge,

Barakala tuwapinge, sichafue kiswahili.

 

MASWALI

(a) Ni mtindo gani aliotumia mshairi katika kutunga ubeti wa 1 na 2. (fafanua kwa kutoa mfano)

(alama 4)

(b) Mshairi ametoa mapendekezo kadha katika shairi kuhusu jinsi ya kuimarisha na kuhifadhi lugha ya kiswahili. Taja na ufafanue matano kati ya hayo.                             (alama 5)

(c) Mshairi anazungumza na akina nani? Anazungumzia nini?                             (alama 4)

(d) Mshairi ametumia tamathali mbalimbali kuwasilisha ujumbe wake. Taja mifano mitatu tofauti ya tamathali hizo.                                                                                                          (alama 3)

(e) Eleza maana ya maneno yafuatayo kama yalivyotumiwa katika shairi.          (alama 4)

  • Muenge
  • Barakala
  • Mtawadhi

MWONGOZO WA KUSAHIHISHA SHAIRI LA 6                                                                                  

8.a)           –      Mtindo wa sabilia: mshororo wa mwisho (kibwagizo) imerudiwarudiwa

–      Pindu: neno moja au sehemu yote ya ubeti wa kwanza hutumiwa kama ukwapi wa ubeti unaofuata

 

  1. Anapendekeza wataalamu wawe macho ili maweye walindwe

–     Kizazi cha sasa wasiige wenye kutaka kugandamiza Kiswahili

–     Barakala wapigwe vikali

–     Ifanywe lugha murwa/ rasmi bungeni

–     Sindano kipigwe kikipatwa na maradhi

  1. Anazungumza na kizazi cha kisasa ili waitunze, kuitukuza na kulinda Kiswahili

Anazungumza juu ya kule kuhifadhi lugha ya Kiswahili

  1. Takriri- Kibwagizo kinarudiwarudiwa kutilia mkazo

Tashihishi-mfano: “kipatwa na maradhi kipigwe sindano” (lugha-uhai)

Chuku-Uzuri wa lugha umeongezwa chumvi

  1. Muenge-Kujitayarisha/ kujihadhirisha
See also  Migwani Secondary School's KCSE Results, KNEC Code, Admissions, Location, Contacts, Fees, Students' Uniform, History, Directions and KCSE Overall School Grade Count Summary

Barakala-Wanaoiga desturi ya kigeni

Mfawadhi-Jitihada

Maamuma-Watu waja

 

  1. a) Kwa vyovyote vile kile anachoona ni chake na ni halali kwake ataitetea mpaka apate/ apewe
  2. SAKARANI – Sababu beti la Takhmisa na la Tarbia zimechanganywa kuitunga

-Ubeti wa kwanza ni wa aina ya takhmisa (mishororo mitano) na ubeti wa pili ni Tarbia

-Ubeti wa pili una mishororo minne na vina vya ndani ni tofauti

Mizani ni nane ukwapi na utao (16 kwenye mshororo)

Uhuru wa lugha k.m taidai badala- nitadai

  1. Yu tayari kufanya kila jambo hata ikiwa ni kwa ncha ya upanga ikiwa mlimani, baharini, yu tayari kufuatilia
  2. Msanii anawapa motisha wasanii wake wawe wakiishi wakijua haki zao ni lazima wapewe la sivyo waitetee kwa vyovyote vile
  3. Mwandishi anasema kuwa izingirwe na ilindwe vilivyo kwa udi na ambari na mabawa lazima haki itunzwe ili isipokonywe au isiponyoke kwani mwanaume inajulikana akiwa hivyo
  4. Mata- Kifo

Maizi- Cha manufaa/ dhamana

Fususi-Mchungaji

 

USHAIRI WA 7

  1. i) Una moyo gani                        N’nakuuliza                 Wangu mhisani

Na kiasi gani                           Unavyojiweza             Ijapo tufani

Ukiwa laini                              Utajipoteza                  Usijibani

Kusimama   Pweke   Kwataka     Makini

 

  1. ii) Zitavuma pepo                        Zitapupuliza                Uanguke chini

Ela uwe papo                          Unajikweleza              Na kujiamini

Utikiishapo                              Umejiuiza                    Pigo la moyoni

Kusimama    Pweke    Kwataka    Makini

 

iii)        Utie migati                              Ya kutuoteza               Hapo aridhini

Kwa nia na dhati                     Usiogeuza                   Au kuihini

Zidate baruti                           Uwe wapuuza             Welele usoni

Kusimama   Pweke     Kwataka     Makini

 

  1. iv) Sishike vishindo                      Na mauzauza               Ya kukuzaini

Kita kama nyundo                  Ukinuiliza                    Unayoamini

Na uje mkondo                       Utadikimiza                Kujipa mizani

Kusimama   Pweke     Kwataka      Makini

 

  1. v) Wengine wasiwe                     Unaoweleza                Yaliyo maani

Wewe ndiwe                           Unaoweleza                Yaliyo maani

Ela kichukuwe                                    Pia kujikaza                 Katika midani

Kusimama    Pweke     Kwataka       Makini

  1. a) Lipe kichwa shairi hili (al 2)
  2. b) Kwa nini kusimama pweke “kwataka makini ’’                                              (al 2)
  3. c) Ni hatua gani zinazopendekezwa mtu anayenuia kusimama pweke?             (al 5)
  4. d) Andika arudhi za shairi hili                                                                             (al 5)
  5. e) Eleza msamiati ufuatao kama ulivyotumiwa katika shairi hili                        (al 6)
  6. Muhisani
  7. Migati
  • Vishindo
  1. Kweleza
  2. Mizani

 

 

MWONGOZO WA KUSAHIHISHA USHAIRI WA 7

  1. a) – Upweke wataka umakini

– Upweke ni uvundo                                                                                       (al 2)

 

  1. b) – Kwasababu matatizo au shida zinapomsonga mtu, asipokuwa na utulivu wa fikira basi – “Yeye huvunjika moyo” kwa vile hapana mtu wa kushirikiana naye   (al 2)

 

  1. c) – Mtu anastahili kuwa mwenye moyo mgumu/ wa ujasiri

–           Awe tayari kusimama kwa udhabiti pindi shida zinapomkabili

–           Ajiamini kwa lolote atendalo kwa imara

–           Awe si mtu wa kutenda mambo ovyo ovyo ambayo yanaweza kumshawishi akaingia mtegoni

–           Awe mstahimilivu na mwenye msimamo dhabiti

–           Awe tayari kudinda na siri za ndani

 

  1. d) i) Lina beti tano
  2. ii) Kila ubeti una mishororo minne, minne

iii)        Ukawafi- Lina vipande vitatu- ukwapi, utao na mwandamizi

  1. iv) Kila kipande kina mizani 6, jumla 18 kila mshororo
  2. v) Kibwagizo chenye kimefupishwa mizani 12
  3. vi) Vina vya ukwapi vinabadilika badilika. Vina vya utao na mwandamizi

vinatiririka

  1. e) Mhisani – Mtu mwema

Migati – Vizuizi

Mkindo – Mw

Unajikweleza –

USHAIRI WA 8

Soma shairi lifuatalo na kisha ujibu maswali yafuatayo.

UKUBWA JAA

Dunia yetu dunia, watu wanakufitini,                                                                                               Dunia huna udhia, watu wanakulaani,                                                                                    Dunia huna hatia, wabebeshwa kila zani,                                                                             Dunia unaonewa, umetenda kosa gani!

Dunia umenyamaza, umetua kwa makini,                                                                  Dunia vitu mejaza, watu wanataka nini?                                                              Dunia wanakucheza,binadamu maluuni,                                                                                     Dunia unaonewa, umetenda kosa gani!

Dunia mtu akose, hukutia mdomoni,                                                                                      Dunia hebu waase, hao watu mafatani,                                                                                Dunia chuki mpuse, muipate afueni,                                                                                   Dunia unaonewa, umetenda kosa gani!

Dunia una lawama, za uongo si yakini,                                                                      Dunia wanokusema, ni manjunju si razini,                                                                            Dunia huna hasama, waja ndio kisirani,                                                                  Dunia unaonewa, umetenda kosa gani!

Dunia kuharibika, hayo amezusha nani?                                                                     Dunia watu humaka, hao wanokuhini,                                                                                           Dunia umejazika, kila tunu ya thamani,                                                                     Dunia unaonewa, umetenda kosa gani!

Dunia unatukisha, bwerere bila undani,                                                                                  Dunia unatukosha, maji tele baharini,                                                                                   Dunia unaotehsa, mimea tosha shambani,                                                                      Dunia unaonewa, umetenda kosa gani!

Dunia hujageuka, tangu umbwe na manani                                                                Dunia watu ndo, nyoka, mahaini na wahuni                                                                  Dunia una baraka, mwenye pupa hazioni                                                                         Dunia huna ubaya, wabaya ni insani.

 

 

Maswali:

(a) Shairi hili ni la bahari gani? Toa sababu yako.                                                  (alama 3)

(b) (i) Kichwa cha shairi hili kinaoanaje na maudhui ya shairi?.                             (alama 2)

(ii) Andika methali moja inayoeleza maudhui ya shairi hili.                                    (alama 3)

(c)Eleza sifa tatu za wanadamu kama anavyoeleza mshairi.                                 (alama 3)

(d)Kwa kutoa mifano kutokana na shairi hili, eleza mbinu tatu za lugha alizotumia
mshairi.                                                                                                           (alama 6)

(e) Eleza maana ya vifungu vifuatavyo vya maneno kama vilivyotumika katika shairi.
(i) bwerere bila undani
(ii) hao watu mafatani
(iii) afueni
(iv) insani                                                                                                        (alama 4)

 

MWONGOZO WA KUSAHIHISHA USHAIRI WA 8

1.

(a) Ni bahari ya kikwamba neno dunia limerudiwa mwanzoni mwa kila mshororo. Bahari nyingine ni ukara, kwa kuzingatia mwanzo, mloto, na mleo, vina vya ukwapi vinabadilika bali cha utao hakibadiliki. Pia, kuna manthawi, mistari ina ukwapi na utao (vipande viwili).

(b)            (i)        Kutokana na ukubwa wake, dunia inatupiwa lawama kwa maovu, udhia na hatia za kila

aina. Dunia inalinganishwa na jalala la kutupia taka.

(ii)       Mbaazi ukikosa kuzaa husingizia jua.

(c)           Binadamu hawapendi kulaumiwa.

Wana kisirani

Ni wahuni, wahaini

Ni waongo.

(d)            Mbinu za lugha:-

Takiri – neno dunia limerudiwarudiwa na pia kibwagizo.

Dunia umeonewa, umetenda kosa gani?’

Tashhisi – Dunia imehuishwa kama mfano:- “Dunia hebu waase inaombwa itoe

mawaidha kwa walimwengu. Isitiara – ‘Dunia watu ndo nyoka’.

Watu wanalinganishwa na nyoka

(e)       Maana ya vifungu:

Bwerere – bila undani – bure pasipo chuki, kinyongo.

Hao watu mafatani – hao watu wafitini

Afueni – nafuu, afadhali

Insani – watu, binadamu.

 

USHAIRI WA 9

  1. Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali.

Jama, Jama, Jamani

Mbona twabebeshwa mateso hivi

Mizigo mikubwa ya dhiki kama

Kwamba hatuna haki ya kusema

Kukataa ndoa za lazima

Kukataa kuozwa wazee

Kukataa kukatishwa masomo

Kukataa tohara ya lazima

 

Jama, Jama Jamani

Iweje tuteswe mateso haya

Na watu wasio kuwa hata na haya kama

Kwamba hatuna haki ya kulalamika

Kulalamikia kutumikishwa kama mayaya

Kulalamikia kudhalilishwa kiunyama

Kulalamikia kutolindwa na sheria

 

Jama, Jama, Jamani

Sasa hii ni awamu nyingine

Na macho tumeyafungua kabisa

Tumekataa kudhalilishwa kabisa

Tumekataa kuteswa kama watumwa

Tumekataa tohara ya lazima

Tumekataa kuozwa……. Tumekataa! Tumekataa

Hii awamu ya ’Haki ya mtoto wa kike’

Maswali

  1. a) Taja mambo matatu muhimu yaliyozungumzwa na mshairi kisha ueleze kila

moja.                                                                                                           (Alama 6)

  1. b) Eleza muundo wa shairi hili (Alama 4)
  2. c) Taja mbinu mbili za lugha alizotumia mshairi kisha ueleze kila moja(Alama 4)
  3. d) Kwa nini mshairi huyu anasema hii ni ’awamu’ nyingine? (Alama 3)
  4. e) Eleza maana ya maneno haya kama yalivyotumiwa na mshairi (alama 3)
  • awamu
  • kudhalilishwa
  • Dhiki

MWONGOZO WA KUSAHIHISHA USHAIRI WA 9

  1. a) SHAIRI

Mambo matatu muhimu yaliyozungumziwa na mshairi na maelezo ya kila moja.

Kutaja alama 1

Kueleza alama 1

Jumla ( alama 6)

 

  1. i) Mateso

-Mizigo mikubwa ya dhiki

-Hakuna haki ya kunena

 

  1. ii) Ndoa ya lazima

-Kuozwa kwa wazee

-Kukatishiwa masomo

 

iii) Tohara

-Tohara ya lazima

-Hawaruhusiwi kusema chochote

 

  1. iv) Sheria

-Haiwalindi

-Kudhalilishwa kinyama

 

  1. v) Awamu tofauti

-Wamekataa kudharauliwa

-Wamekataa kuteswa

-Wamekataa  tohara za lazima.

 

  • Muundo wa shairi

i)Ni wimbo ambao haufuati muundo wowote wa ushairi

ii)Ni shairi huru

iii)Halina mpangilio wowote wa kiarudhi

iv)Halina mgao wa mishororo

v)Halina vina wala mizani

vi)Halina kibwagizo

vii) Lina beti 3

viii)Mishororo si sawa  katoka kila ubeti

  1. Mbinu mbili za lugha alizotumia mshairi. Maelezo ya kila moja
  2. i) Nyimbo-Amezitumia Kwa njia mwafaka ili anase hisia za wasomaji.
  3. ii) Takriri-Amejaribu pia kusisitiza ili kuwekea uzito yale anayozungumzia.

-Anataka msomaji apate mvuto mzuri kwa lile analolizungumzia. Mfano tumekataa kudhalilishwa, tumekataa kuteswa, tumekataa tohara.

iii) Mdokezo. Mfano Tumekataa kuozwa …

  1. iv) Tashbihi . mfano ubeti wa pili- Kutumikishwa kama yaya

 

                       

  1.    Sababu za mshairi kusema; ‘hii ni awamu nyingine’

i)Ulikuwa ukurasa mpya wa maisha.

ii)Kuna mabadiliko ya kuondoa ukandamizaji.

iii)Wanawake wamekataa kuozwa kwa lazima.

iv)Wamekataa kudhalilishwa kabisa

  1. Maana ya maneno

i)) awamu-Kipindi

  1. ii) kudhalilishwa-kukandamizwa/ kudunishwa / kufedheheshwa
  2. dhiki-shida

 

USHAIRI WA 10

 

 Soma shairi lifuatalo  kisha ujibu maswali yafuatayo

  1. Mkata ni mkatika, harithi hatoridhiwa

Sina ninalolishika, wala ninalochukuwa

Mlimwengu kanipoka, hata tone la muruwa!

Mrithi nini wanangu?

 

  1. Sina ngo’mbe sina mbuzi, sina konde sina buwa

Sina hata makaazi, mupasayo kuyajuwa

Sina mazuri makuzi, jinsi nilivyoachwa

Mrithi nini wanangu?

 

  1. Sina kazi sina bazi, ila wingi wa shakawa

Sina chembe ya majazi, mno nikukamuliwa

Nakwa’cheni upagazi, ngumu kwenu ku’tuwa

Mrithi nini wanangu?

 

  1. Sina sikuachi jina, mkata hatasifiwa

Hata nifanye la mana, mno mi kulaumiwa

Poleni wangu sana, sana kwenu cha kutowa

Mrithi nini wanangu?

 

  1. Sina leo sina jana, sina kesho kutwaliwa

Sina zizi sina shina, wala tawi kuchipuwa

Sina wanangu mi sina , sana la kuacha kuraduwa

Mrithi nini wanangu?

 

  1. Sina utu sina haki, mila yangu meuliwa

Nyuma yangu ili dhiki, na mbele imekaliwa

N’nawana na miliki, hadi nitakapofukiwa

Mrithi nini wanangu?

 

  1. Sina ila kesho kwenu, wenyewe kuiongowa

Muwane kwa nyinyi mbinu, mwende pasi kupumuwa

Leo siyo kesho yenu, kama mutajikamuwa

Mrithi nini wananngu?

 

 

 

  • Taja mambo yoyote mawili ambayo mtunzi angewarithisha wanawe.      (alama 2)
  • Eleza sababu ya mtunzi kutoweza kuwarithisha wanawe.                                                   (alama 3)
  • Andika ubeti wa nne kwa lugha nathari.                                                                             (alama 4)
  • Dondoa mifano miwili miwili ya :                                                                            (alama 2)
    • Inkisari
    • Tabdila
  • Chambua shairi hili kwa upande wa :
    • Dhamira                                                                  (alama 2)
    • Muundo                                                                  (alama 4)

 

  • Eleza maana ya vifungu vifuatavyo kama vilivyotumiwa katika shairi.                 (alama 3)
    • Mlimwengu kanipoka
    • Sina konde sina buwa.
    • Wingi wa shakawa.

 

MWONGOZO WA KUSAHIHISHA USHAIRI WA 10

 

  • – Makazi mabovu

–     Upagazi

–     Kutothaminiwa

–     Dhiki

–     Kufanya kesho ya wengine nzuri

 

  • – Ni maskini hohehahe / hana kitu

–     Aliporwa kila kitu.

–     Hana  mifugo.

–     Hana kazi yoyote.

–     Hana sifa / umaarufu.

–     Ana makazi mabovu.

 

  • – Sina jina nitakawacha kwani maskini hasifiwi

–     Hata nikifanya jambo la maana ninalaumiwa tu.

–     Poleni sana wanangu kwa kuwa sina la kuwatolea.

–     Mtarithi nini wanangu?

 

  • (i) Inkisari
  • Mana – Maana
  • Meuliwa – Imeuliwa
  • Nitapofukiwa – Nitakapofukiwa.

 

(ii) Tabdila

Muruwa           – Murua

Kutowa           -Kutoa

Kuchipuwa      -Kuchipua

Kuiongowa     – Kuiongoa

Kupumuwa     – Kupumua

 

  • (i) Dhamira
  • Kuwahimiza watu kufanya bidii wakiwa vijana.
  • Kulalamika kwamba maskini hana haki / huonewa / hapewi nafasi.

 

(ii) Muundo

  • Shairi ni aina ya tarbia / unne.Lina mishororo minne katika kila ubeti.
  • Mishororo ya kwanza mitatu imegawika katika sehemu mbili (ukwapi na utao).
  • Kila kipande kina mizani nane na kila mshororo una mizani kumi na sita.
  • Vina vya kati vinatofautiana kutoka ubeti mmoja hadi mwingine, lakini vina vya mwisho ni sawa katika shairi zima katika mishororo ya kwanza mitatu.
  • Shairi hili lina kibwagizo ambacho kimefupishwa.

Mrithi nini wanangu?

  • Shairi hili lina beti saba.

 

  • (a) Mlimwengu kunipoka – Mlimwengu kanipokonya.

(b) Sina konde sina buwa  – Sina shamba sina chochote.

(c) Wingi wa shakawa – mashaka mengi.

 

USHAIRI WA 11

                                    Soma shairi hili kisha ujibu maswali.

 

Jicho, tavumiliaje, kwa hayo uyaonayo?

Kicho, utasubirije, maonevu yapitayo

Kwacho, lijalo na lije, nimechoka vumiliyo

Naandika!

 

Moyo, unao timbuko, maudhi tuyasikiayo

Nayo, visa na mauko, wanyonge wayakutayo

Kwayo, sina zuiliko, natoa niyahisiyo

Naandika!

 

Hawa, wanotulimiya, dhiki wavumiliayo

Hawa, mamiya mamiya, na mali wazalishayo

Hawa, ndo wanaoumiya, na maafa wakutayo

Naandika!

 

Hawa, sioni wengine, kwao liko angamiyo

Hawa, uwapa unene, watukufu wenye nayo

Hawa, bado ni wavune, kwa shida waikutayo

Naandika!

 

Bado, wawapo mabwana, wenye pupa na kamiyo

Bado, tafauti sana,  kwa pato na mengineyo

Bado, tuling’owe shina, ulaji pia na choyo

Naandika!

 

Maswali

  • Shairi hili laweza kuwekwa katika bahari zipi? (alama 4)

Thibitisha kila jibu lako.

 

  • Eleza dhamira ya mshairi. (alama 2)
  • Onyesha mifano miwili ya uhuru wa kishairi jinsi ulivyotumika katika shairi.            (alama 2)
  • Andika ubeti wa tatu kwa lugha nathari.            (alama 4)
  • Tambulisha kwa mifano mbinu zozote mbili za sanaa katika shairi. (alama2)
  • Fafanua sifa za kiarudhi zilizotumika katika ubeti wa tano. (alama 3)
  • Eleza maana ya maneno haya kama yalivyotumiwa katika shairi. (alama 3)

(i)  Zuiliko

(ii)  Wavune

(iii)  Wenye pupa na Kamiyo.

 

MWONGOZO WA KUSAHIHISHA USHAIRI WA 11

 

  1. a)         Tarbia            –           Lina mishororo minne katika kila ubeti

            Msuko            –           Kibwagizo kimefupishwa.

Ukara             –           Vina vya nje vinatiririka katika beti zote ilhali vya

ndani havitiririki.

Ukawafi         –           Una vipande vitatu (ukwapi, utao na mwandamizi)

katika mishiroro ya kwanza mitatu ya kila ubeti isipokuwa kibwagizo

Kikwamba – Katika beti za 3-5 neno moja ndilo linaanza kila mshororo.

Sakarani – Kuna bahari kadhaa katika shairi.

  1. Kuwahimiza watu (hasa wanyonge P) wainuke na kupinga Pmaovu na maonevu wanayofanyiwa na matajiri wenye uwezo.
  2. Inkisari km vumiliyo – kuvumilia nanaandika.

Mazida kurefusha k.m. angamiyo, vumiliyo n.k.

Tabdila k.m mamiya badala ya mamia

 

  1. Hawa wanaotulimia wanavumiliaP dhiki

Wao ni wengi P na ndio huzalisha mali.

Wao ndio wanaoumiaP na kupata mateso / taabu

Wanayokumbana nayo.Ninaandika / ninasema

 

  1. Takriri – hawa, bado, mamiya.

Balagha – uyaonaje?

Taharuki – Naandika!

Inkisari – Hawa, ndo

Kinaya – Watukufu wenye nayo

 

  1. f) Kuna mishororo minne

Kuna vipande vitatu katika mishororo ya kwanza mitatu na kimoja katika kibwagizo

Vina vinatiririka / vinafanana

Mizani                        2,- 6-8

2-6-8

2 – 6 – 8

4

  1. g) i)          Cha kunizuia / kizuizi / kizingiti / uoga / hofu/ pingamizi
  2. ii) Wachovu /dhaifu /hafifu

iii)        Walio na tamaa kubwa / walafi/ mabwanyenye

SHAIRI LA 12

Soma shairi hili kisha ujibu mawali  yanayofuata.

SABUNI YA ROHO

Ewe tunu ya mtima, kwa nini wanikimbia?

Ndiwe suluhu la zama, waja wakukimbilia,

Waja wanakutazama, madeni wakalipia,

Ndiwe sabuni ya roho, ndiwe mvunja mlima.

 

Ndiwe mafuta ya roho, walisema wa zamani,

Utanunua majoho, majumba na nyumbani,

Umezitakasa roho, umekuwa mhisani,

Ndiwe sabuni ya roho, ndiwe mvunja mlima.

 

Matajiri wakujua, wema wako wameonja,

Nguo zao umefua, wakupata kwa ujanja,

Sura Zao ‘mefufua, Wanazuru kila nyanja,

Ndiwe sabuni ya roho, ndiwe mvunja mlima.

 

Ndiwe mvunja mlima, onana na masikini

Watazame mayatima, kwao kumekua wa duni

Wabebe waliokwama, wainue walio chini,

Ndiwe sabuni ya roho, ndiwe mvunja mlima.

 

Ndiwe mvunja mlima,wapi kapata uwezo?

Umezua uhasama, waja kupata mizozo,

Ndiwe chanzo cha zahama, umewaitia vikwazo,

See also  Grade 5 CBC schemes of work free- term 1 to 3

Ndiwe  sabuni ya roho, Ndiwe mvunja mlima.

 

 

Umevunja usuhuba, familia zazozana,

Walokuwa mahabuba, kila mara wagombana,

Roho zao umekaba, majumbani wachinjana,

Ndiwe sabuni ya roho, ndiwe mvunja mlima.

 

Nakutafuta kwa hamu, sabuni unirehemu,

Sinilipue ja bomu, sije kawa marehemu,

Niondoe jehanamu, ya ufukara wa sumu,

Ndiwe sabuni ya roho, ndiwe mvunja mlima.

 

Naondoka wangu moyo, nikuitapo itika

Fulusi wacha uchoyo, tatua yalonifika,

Nichekeshe kibogoyo, nami nipate kuwika,

Ndiwe sabuni ya roho, ndiwe mvunja mlima.

 

 

  • Mshairi anaongea na nani katika shairi hili?      [alama 1]
  • Taja majina mengine matatu aliyopewa huyu anayesemeshwa.      [alama 3]
  • Anayezungumziwa katika shairi hili amesababisha balaa gani?                  [alama 2]
  • Mshairi anatoa mwito gani kwa mwenziwe?      [alama 4]
  • Fafanua maudhui ya ubeti wa sita.      [alama 2]

 

  • Mbinu kadha za uandishi zimetumiwa na msanii kuwasilisha ujumbe wake. Taja mbinu zozote tatu na uzitolee mifano katika shairi. [alama 3]

 

  • Fafanua maana ya:

Sura zao “mefufua, wanazuru kila nyanja.                                                       [alama 1]

  • Andika ubeti wa saba katika lugha nathari.     [ alama 4]

 

MWONGOZO WA KUSAHIHISHA USHAIRI WA 12

 

  1. (a) pesa.

(b)Majina aliyopewa.

  • Sabuni ya roho.
  • Mvunja mlima.
  • Mafuta ya roho.
  • Fulusi .
  • Tunu ya mtima.
  • Suluhu la zama.

 

(c) Amesababisha balaa gani.

  • Amesababisha uhasama/ uadui.
  • Ugomvi kati ya wapenzi.

 

(d) Mtoto kwa mwenziwe.

  • Awaarike maskini na mayatima .
  • Asimwangamize bali bali amwondoe kwenye ufukara.
  • Amwitapo aitike.
  • Aache uchoyo / amtatulie shida zake.
  • Amchekeshe /amfurahishe.

(e) Maudhui  ya ubeti wa sita .

-Pesa zimezua uhasama katika ndoa nyingi na kusababisha vifo.

(f) Mbinu za uandishi.

  • Istiara –Pesa ni sabuni/mafuta. n.k
  • Semi – mvunja mlima.

— sabuni ya roho.

(iii)   Tashhisi –umevunja usuhuba.

-umezua uhasama.

(iv)Balagha- kwa nini wanikimbia?

–wapi kapata uwezo?

(v)Takriri—Ndiwe mvunja mlima.

Mbinu na mfano alama 1

(g) Maana ya-

Sura zao imefufua, wanazuru kila nyanja.

-Pesa zimewaletea furaha hata wanatalii sehemu zozote wanazotaka.

Alama 1

 

(h)Lugha nathari.

Mashairi anasema kuwa anamtafuta pesa sana ili amsaide. Anamsihi asimpige kwa kumtoroka na kumwacha hoi bila uwezo. Anamwomba amuondoe katika lindi hili la umaskini kwa vile yeye ndiye anayetuliza watu na kuwaondolea matatizo ya kila namna.                                   Alama 4

 

USHAIRI WA 13

Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali.

  1. Lau dunia nanena, tuseme si ati ati,

Mauti kawa hakuna, katika wote wakati,

Vipi tungelisongana, tunaoishi tiati?

Lau hakuna mauti, vipi tungelisongana?

 

  1. Dunia ingetatana, na kizazi katikati,

Huku kwazaliwa bwana, kule kwazawa binti,

Vipi tungeliona, na kuzaa hatuwati?

Lau hakuna mauti, vipi tungelisongana?

 

  1. Lau mauti hakuna, tungesongana sharuti,

Kwa viumbe kukazana, wanadamu na manyati,

Vipi tungelijazana, kwa kusitawi umati?

Lau hakuna mauti, vipi tungelisongana?

 

  1. Walakini subuhana, kapanga sisi na miti,

Ili tusizidi sana, si wengi na si katiti,

Maisha ya kupishana, yule ende yule keti,

Lau hakuna mauti, vipi tungelisongana?

 

  1. Ndipo dunia kufana, ikawa kama yakuti,

Kwa uwezewe Rabana, kaipanga madhubuti,

Maisha kugawiana, kayagawa kwa mauti,

Lau hakuna mauti, vipi tungelisongana?

 

  1. Njia ingekuwa hapana, pembeni na katikati ,

Sote tungeambatana, pa kulima hatupati,

Na njaa ingetutafuna, pa kulima hatupati,

Lau hakuna mauti, vipi tungelisongana?

 

  1. Peleleza utaona, hayataki utafiti,

Kama tungelikongana , ingelikuwa ni bahati,

Vipi tungelisukumana, katika hiyo hayati?

Lau hakuna mauti, vipi tungelisongana?

 

  1. Mbele sitakwenda tena, hapa mwisho nasukuti,

Yaeleni waungwana, shauri yake jabaruti,

Yote tuloelezana, katenda bila senti,

Lau hakuna mauti, vipi tungelisongana?

 

MASWALI

  1. a) Shairi hili ni la bahari gani?  (alama 2)

 

  1. b) kwa kutoa mifano mwafaka onyesha jinsi mtunzi wa shairi hili alivyotumia

uhuru wa utunzi                                                                                                                  (alama 2)

 

  1. c) Eleza muundo wa shairi hili   (alama 4)
  2. c) Andika ubeti wa tano katika lugha nathari.  (alama 4)
  3. d) Tambulisha mbinu zozote mbili za lugha zilizotumiwa na mshairi (alama 4)
  4. e) Eleza maana ya maneno haya kama yalivyotumika katika shairi

i)katiti

  1. ii) yakuti

iii) Hatuwati

  1. iv) Nasukuti                                                      (alama 4)

 

MWONGOZO WA KUSAHIHISHA USHAIRI WA 13

Bahari la shairi

  • Tarbia au unne
  • Mtirirko – vina vya kati na vya nje vinafafana katika shairi nzima.

Km vya kati                                        vya mwisho

na                                            ti

na                                            ti

na                                            ti

ti                                              na

  • Mathnawi- lina vipande viwili

Ukwapi na utao.

 

  1. Idhini / uhuru / ruhusa
    • Inkisari km ngekuwa, ngetutafuna
    • Tabdila km sharuti – sharti.
    • Kuboronga sarufi – mauti kawa hakuna

– katika wote wakati

(iv)       Lahaja – Hatuwati – Hatuwachi

Yaoleni – yaoneni

 

  1. Umbo /sura / muundo / mpangilio
    • Beti 8
  • Mishororo 4 kila ubeti / tarbia / unne
  • Mizani 16 kila mshororo
  • Mtiririko wa vina.
  • Vipande viwili
  • Kibwagizo kunachorudiwarudiwa

 

  1. Ujumbe katika ubeti wa 5
    • Dunia haiwezi kujaa watu kupita kiasi.
    • Mwenyezi mungu anajua kupanga
    • Baadhi ya watu wale na baadhi wazaliwe.
    • Bila kifo duniani tungesongomana            

 

  1. Mbinu za lugha
    • Balagha km –          vipi tungelisongana, tunaoishi tiati?
    • Tashbihi –          ikawa kama yakuti kama ukosi na shati
    • Takriri –           si ati ati

(i)         Katiti          –           kidogo / chache

(ii)        Yakuti        –           kito cha thamani

(iii)        Hatuwati   –           hatuwachi

(iv)        Nasukuti    –           sirudi nyumi,

 

USHAIRI WA 14

KIFO

  1. ‘likuwa tisini moja 2.         ‘lituachia vioja

‘lipojikunja pamoja                                                      Raha hatujaionja

Kutuaga mara moja                                                     Tumezidi na kungoja

Safari moja kwa moja                                                 Matumaini ya waja.

 

  1. Kifo hatuna faraja 4.         Maisha ‘mekosa haja

Baba livuka daraja                                                      Na mama amejikunja

‘likuwa wetu kiranja                                                   katwa auma viganja

Majonzi ‘lituachia                                                       Nyumba sasa inavuja

 

  1. Vitamu nani taonja 6.         Kifo kwetu sisi waja

Mali sasa imefuja                                                        Tumaini hutuvunja

Mifupa tutaivunja                                                       Ingawa ndio daraja

Mifugo katu uwanja                                                    Haituweki pamoja

 

MASWALI

  1. Eleza umbo la shairi hili. (alama 4)
  2. Mshairi ana ujumbe gani ? (alama 2)
  3. Taja mbinu zozote tatu za lugha alizotumia mshairi na uzitolee mifano kutoka shairi.(alama 6)
  4. Andika ubeti wa tatu kwa lugha ya nathari. (alama 4)
  5. Eleza maana ya mistari hii kama ilivyotumika katika shairi. (alama 2)
  6. i) Baba livuka daraja
  7. Kutwa auma viganja
  8. i) Mshairi ametumia mbinu gani katika maneno haya .                                      (alama 1)

‘likuwa

‘lituachia

‘lipojikunja

  1. ii) Kwa nini akatumia mbinu hiyo?                                                                            (alama 1)

 

MWONGOZO WA KUSAHIHISHA SHAIRI LA 14

  1. – Beti -6

–           Mishororo 4 kila ubeti

–           mizani 8 kila mshororo

–           Kipokeo  kinatofautiana kila ubeti

–           Utenzi

  1. –           Kifo ndio daraja ya kila mtu

–           kifo huacha watu bila matumaini

–           hufanya watu wateseke

  1. –           Takriri – moja

–           Tashhisi – kifo

–           Taswira

–           Tunia – fuja, vunja

  1. – Hawana raha baba alipofariki aliwekuwa kiongozi wao sasa amewaachia shida tupu.
  2. –           Alifariki

–           Anajuta

  1. –           Inkisani           –           idadi ya mizani iwe sawa / urari wa mizani

 

USHAIRI WA 15

Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali yote.

 

KIPIMO NI KIPI?

Nitampa nani, sauti yangu ya dhati

Kwa kipimo gani, ingawa kiwe katiti

Amefanya nini, La kutetea umati

Kipimo ni kipi?

 

Yupi wa maani, asosita katikati

Alo na maoni, yasojua gatigati

Atazame chini, kwa kile ule wakati

Kipimo ni kipi?

 

Alo mzalendo, atambuaye shuruti

Asiye mafundo, asojua mangiriti

Anoshika pendo, hata katika mauti

Kipimo ni kipi?

 

Kipimo ni kipi, changu mimi kudhibiti

Utu uko wapi, ni wapi unapoketi

Nije kwa mkwapi, au ndani kwa buheti

Kipimo ni kipi?

 

  • Eleza umbo la shairi hili                               Alama 4
  • Taja tamadhaliza usemi na kisha utoe mifano                           Alama 3
  • Taja na ueleze namna mshairi alivyotumia uhuru wa ushairi?                              Alama 2
  • Eleza maudhui ya shairi hili?                              Alama 3
  • Andika ubeti wa tatu kwa lugha nathari                            Alama 4
  • Eleza msamiati ufuatao kama ulivyotumiwa                         Alama 4
    • Katiti
    • Gatigati
    • Shuruti
    • Mangiriti

MWONGOZO WA KUSAHIHISHA USHAIRI WA 15

    • Tarbia –lina mishororo minne.
    • Vina vya ndani havitiririki –vina vya nje vinatiririka.
    • Mizani 6-8

6-8

6-8

8

  • Lina kibwagizo –kipimo ni kipi?
  • Vipande viwili isipokuwa kibwagizo.

Alama 4

    • Balagha –kipimo ni kipi?
    • Usemi –atazame chini.
    • Tashhisi –kukipa kitu kisicho na uhai. (maoni yasojua gatigati)
  • Inkisari- asosita –asiyesita

-alo -aliye

-yasojua -yasiojua

-anoshika-anayeshika

Tabdila-maani-maana

    • Watu wapende nchi yao kwa kufuata sheria zake.
    • Watu wasichukue watu wengine.
    • Watu hawana utu.
    • Hana uhuru wa kutoa maoni.

Apendaye nchi yake na kufuata

Sheria zake, asiyechukia watu wala kuhadaa,

Kudanganya, au yule ashikaye

Pendo hadi kifoni, atajulikanaje au atapimwaje?        Alama 4

  • Katiti –kidogo.

Gatigati –ubaguzi/upendeleo.

Shuruti –lazima.

Mangiriti –mambo ya kuhadaa/uongo.

 

USHAIRI WA 16

 

Vita vya ndimi

 

 

Huyo! Amshike huyo!

Hakuna bunduki wala kifaru

Bomu na risasi hata hawazijui!

Lakini mno wanashambuliana.

Kwa ndimi zilizonolewa kwa makali

Vipande vya matusi silaha zao.

 

Yu imara mmoja wao.

Akirusha kombora la neno zito!

Limtingishe adui wake

Na kumgusa hisia kwa pigo kuu.

Pigo linalopenya moyoni kama kichomi

Kuchipuza joto la hasira na kisasi

Katika mapigano yaso na kikomo.

 

Filimbi ya suluhu inapulizwa kuwaamua!

Ni nani anayekubali suluhu?

Roho zinakataa katakata

Huku ukaidi ukinyemelea na kutawala kote

Mapandikizi ya watu yakipigana

Vitu shadidi visivyo ukomo

Vita vya ndimi!

 

Magharibi sasa

Jua linapungia mkono  machweo

Nalo giza likinyemelea kwa kiburi na kasi

Sisikii tena sauti za misonyo

Mate ya watesi yamekauka

 

Makanwa yao yamelemewa na uchovu

Sasa wameshikana mikono

Nyuso zao zikitabasamu

Ishara ya suluhu!

 

 

  • Hili ni shairi la aina gani?      (alama 1)
  • Eleza sifa za utunzi alizotumia mshairi.      (alama 4)
  • Taja kwa kutolea mifano tamathali za usemi zozote tatu zilizotumiwa katika shairi hili.(alama 3)
  • Fafanua mishororo hii:
    • Akirusha kombora la neno zito!
    • Makanwa yao yamelemewa na uchovu                                                     (alama 4)
  • Zungumzia mgogoro katika shairi na namna unavyomalizika.      (alama 6)
  • Toa maana ya msamiati huu
    • Kichomi
    • Misonyo       (alama2)

 

MWONGOZO WA KUSAHIHISHA USHAIRI 16

  1. (a) (i) Shairi huru.
  • Shairi la kimapindusi.

(b) Sifa za utunzi. (muundo umbo)

  1. Shairi lina beti nne.
  2. Idadi ya mishororo inatofautiana katika beti za shairi.
  • Halina mpangilio maalum wa mizani.
  1. Halina vina (masivina)
  2. Halina kibwagizo.
  3. Beti zake hazijagawanywa katika vipande.

Zozote 4×1=4

(c) Tamathari za msemi.

  1. Nidaa/siyali/mshangao.

Km. Huyo! Amurike huyo!

Km. Ni nani anayekubali suluhu?

Km. Pigo linalopenya moyoni kama kichwani.

Km. Roho zinakataa kata kata.

  1. Tashhisi

Km. Jua linapungia mkono machweo.

  1. Istiari

Km. Kuchipuza joto la hasira na kisasi.

Zozote 3×1=3

 

(d)

  1. Akimsha kumbora la neno zito!

Akitoa matusi ya kuudhi/kukasirisha.

  1. Makanwa yao yamelemewa na uchovu.

Midomo yao haitoi matusi tena (imetulia)

(2×2=4)

(e)Mgogoro:

  1. Kuna vitu vya maadui wawili.
  2. Wanapigana kwa midomo yao – wanatusiana
  • Matusi yenyewe ni makali mno.
  1. Matusi yanaleta hasira/hamaki kwa anayetusiwa.
  2. Ingawa kuna juhudi za kuwapatanisha wanakataa kabisa.
  3. Wanazidi kuwa wakaidi na kuendeleza vita vyao vya matusi.

Zozote 4×1=4

Kumalizika

  1. Jioni inapofika, wamechoka ndipo wanatulia.
  2. Wanaridhiana (wanashikana mikono) huku wakitabasamu na kusameheana.

Zozote 2×1=2

(f)

  1. Kichomi – lenye kuumiza
  2. Misonyo – mifyonyo, kufyonya kwa hamaki au ishara ya chuki.

 

USHAIRI WA 17

Soma mashairi ya A na B kisha ujibu maswali.

A

Mtu ni afya yake, ndio uzima wa mtu

Mtu ni kuwa na chake, hakuwi ela kwa kitu

Mtu ni bahati yake, kupendekeza kwa watu

Mtu si fakhari kwako, kuitwa nyama ya mwitu

 

Mtu ni ulimi wake, kunena vyema na watu

Mtu ni kijungu chake, kuweka mawe matatu

Mtu ni mwenda kwa lake., mtoshawa na kula kitu

Mtu  si uzuri kwake, kuitwa nyama wa mwitu

 

Mtu ni mwenye nadhari, apimaye kula kitu

Mtu ni moyo hariri, mwenye imani na watu

Mtu ni alo na ari, shika sana mwana kwetu

Mtu si yake fakhari, kuitwa nyama wa mwitu

 

Mtu ni mkono wazi, mtasadaku na watu

Mtu ni mwenye maozi, kuoneya kula kitu

Mtu ni alo tulizo, asopenda utukutu

Mtu si jambo pendezi, kuitwa nyama wa mwitu

 

Mtu ni mwenye ahadi, ndio u’ngwana na utu

Mtu ni alo baridi, mbembeleza wa watu

Mtu ni moyo asadi, asoonewa na mtu

Mtu si yake ifadi, kuitwa nyama wa mwitu

 

Mtu niliyoyanena, pima sana ewe mtu

Mtu sikuja tukan, kukirihi nyoyo watu

Mtu nakupa maana, wende nyendo za kiutu

Mtu si uzuri sana, kuitwa nyama wa mwitu

Mtu ni mtenda njema, atwiiye Mola wetu

Mtu ni mbele na nyuma, pima sana mwana kwetu

Mtu natiye khatima, fafanua kula kitu

Mtu si yake hisima, kuitwa nyama wa mwitu.

 

B

MTU HACHAGUI KAZI

Naamba kazi ni kazi, vyovyote vile iwavyo

Madamu si ubazazi, kwa mwanaadamu ndivyo

Kushona na upagazi, pia vile vyenginevyo

Kazi ni kitu azizi, wala vyenginevyo sivyo

Mtu hachagui kazi.

 

Mtu hadharau kazi, ile ahisiyo duni

Ayuzuie machozi, walilia jambo gani

Ukulima na ukwezi, na uvuvi baharini

Hizi nazo njema kazi, yafaa uzibaini

Mtu hachagui kazi

 

Si laiki kubughudhi, hakuna iliyo duni

Hayo makubwa maradhi, na tena uhayawani

Kazi zote zina hadhi, hivyo tusibagueni

Inafaa tuziridhi, tuzitende kwa yakini

Mtu hachagui kazi.

 

Ni wajibu kuipenda, na kuikiri moyoni

Na kwa dhati kuitenda, kwa juhudi na makini

Matatizo huyashinda, na uvivu kuuhuni

Hapo mtu atashinda, na magumu kumhuni

Mtu hachagui kazi

 

MASWALI

  • Lipe shairi la A kichwa mwafaka.                                                                 (alama 1)
  • Kwa mifano mwafaka fafanua bahari katika shairi la A na B. (alama 4)
  • Toa sababu za mwandishi kuchagua “Mtu hachagua kazi” kama kichwa cha shairi la B.

(alama 1)

  • Mtunzi alikuwa na ujumbe gani katika mashairi haya? (alama 4)
  • Andika ubeti wa pili wa shairi A katika lugha nathari. (alama 4)
  • Eleza muundo wa shairi la B. (alama 4)
  • Eleza maana ya maneno haya kama yalivyotumika katika mashairi haya. (alama 2)

 

(i) Nadhari

(ii) Ubazazi

MWONGOZO WA KUSAHIHISHIA USHAIRI WA 17

  • Mtu si mnyama wa mwitu (alama 1)
  • Shairi A
    • Kikwamba – neon la kwanza katika kila mshororo ni sawa – mtu.
    • Ukara – kina cha mwisho hakibadiliki huku cha kati kikibadilika

2 x 1 = 2.

Shairi B

  • Msuko – mshororo wa mwisho wa kila ubeti umefupishwa.
  • Ukaraguni – vina vya kati na vya mwisho vinabadilikabadilika.

2 x 1 =2.

  • Ni kibwagizo na kinabeba uzito wa ujumbe unaozungumziwa.Alama 1.

– Mtu anatakikana kutenda mazuri kila wakati.

– Kazi zote ni nzuri kwa hivyo tusiwe watu wa kubagua kazi

2 x 1 = 2.

– Mtu hujulikana kwa yale anayosema yeye na watu wengine.

– Ni mtu mwenyewe kujijenga.

– Mtu ni yule anayetumia chake na kutosheka nacho.

– Si jambo zuri mtu kuitwa mnyama wa mwituni.

4 x 1 = 4.

  • Shairi B

– Beti nne (4)

– Mishororo mitano kila ubeti.

– Mizani kumi na sita kila mshororo.

– Kibwagizo kimefupishwa.

– Kuna vipande viwili, ukkkwapi na utao.

– Vina vinabadilika badilika.

4 x 1 = 4.

  • Nadhari – busara
  • Ubazazi – ulaghai

 

USHAIRI WA 18

Soma shairi lifuatalo kisha uiibu maswali

 

 

Duniani husifiki;

Wala hupati thamani,

Yalisemwa hukumbuki?

Na wazee wa zamani,

“Mkono haurambiki,

Bila kitu kiganjani

 

Wangapi watu azizi,

Fulani bin Fulani,

See also  Free Set book notes, guides, English Literature notes, Poetry notes and Many More: A Doll's House, Blossoms, The Pearl...

Waliokichinja mbuzi,

Kukirimu mitaani,

Sasa kama wapuuzi,

Kwa hali kuwa ta’bani

 

Walifanya makubeli.

Wakaapa hadharani,

La uongo huwa kweli,

” Kubishika kitaani,

Na tangu kukosa mali,

Wakawa kama nyani!

 

Walifanya mahashumu.

Kuwaliko masultani,

Ushekhe na Ualimu,

Kufasiri vitabuni,

Na leo wana wazimu,

Kama si wanachuoni.

 

 

Maswali

 

(a)  Kwa maneno yako mwenyewe eleza ujumbe wa shairi hili.                                                  (Alama 3)

(b)  Eleza jinsi mshairi anavyosisitiza huo ujumbe katika shairi lote.                              (Alama 4)

(c)  Eleza kwa tafsili umbo la shairi hili.                                                                                     (Alama 5)

(d) Andika ubeti wa kwanza katika lugha nathari.                                                                       (Alama 3)

(e)  Eleza maana ya maneno haya kama yalivyo tumika katika shairi;

(i)      Kiganjani.

(ii)      Kukirimu.

(iii)      Makubeli.

(iv)      Mahashumu.

(v)      Wanachuoni                                                                                                          (Alama 5)

USHAIR1:

Soma shairi lifuatalo kisfea ujibu saaswali vanavofuata:

 

Niliusiwa zamani, babu aliniusia, N

ili bado utotoni, hapo aliponambia,

Babu yaweke kitwani, yasije yakapotea,

Penye nia ipo njia, usikate tumaini.

 

  1. Wewe bado ni mgeni, katika hii dunia,

Mimi ndiye wa zamani, mengi nimejionea,

Sasa niko uzeeni, uzee umewadia,

penye nia ipo njia, usikate tumaini.

 

  1. Mtima ndio sukani, waongoza’kila ndia,

Weka mkazo moyoni, kila unalofwatia,

Moyoni mwako amini, kuwa utalifikia,

Penye nia ipo njia, usikate tumaini.

 

  1. Kama uko safarini , waongoza kila ndia,

Bahari kuu kinani, mawimbi yakuchachia,

Usikate tumaini. hapo ndipo penye ndia,

Penye nia ipo njia, usikate tumaini.

 

  1. Hapo hapo mawimbini, wewe hapo pigania,

Hapo ndipo milangoni, mawimbi yakuzuia,

Mtima utie kani, bandarini utangia,

Penye nia ipo njia, usikate tumaini.

 

  1. Na iwapo ni shuleni, masomo yakutatia,

Usiasi masomoni, kusoma ukakimbia,

Kidogodogo bongoni, elimu itakungia,

Penye nia ipo njia, usikate tumaini.

 

  1. Kama wenda uchumini, biashara waania.

Usihofu asilani, hasara ikitukia,

Leo ukipata duni, na kesbo litazidia,

Penye nia ipo njia, usikate tumaini.

 

 

  • Andika methaii ambayo ingetumiwa kujumuisha ujumbe katika ubeti wa pili.     (Alama 1)
  • Kutokana na shairi hili, ni katika nyanja zipi za maisha tunapopaswa kujikakamua? Tujikakamue vipi?                                                                                                      (alama 6)
  • Taja arudhi ambazo zimetumiwa kuusarifu ubeti wa kwanza.     (Alama 4)
  • Huku ukitoa mfano mmoja bainisha uhuru wa kishairi ambao umetumiwa katika ubeti wa 3.

(alama 1)

  • Andika ubeti pili kwa lugha ya nathari.                 (Alama 4)
  • Eleza maana ya maneno yafuatayo kama yalivyotumika katika shairi.
    • (i)
    • (ii)
    • (iii) Sukani
    • (iv)                                                                             (Alama 4)

 

MWONGOZO WA KUSAHIHISHIA USHAIRI WA 18

  1. (a)            Mshairi anasemaa kuwa mtu ambaye hana mali hadhaminiwi kwa kuwa mkono mtupu                                ( alama 3)

(b)

  • kwa kueleza vile Sultan, Shehe, walimu walivyopungua thamani.
  • Kwa kutumia methali; mkono mtupu haulambwi
  • Kwa kutumia methali, tashbihi za kinyume mfano

Azizi kuwa kama wapuuzi

Makubeli kuwa kama nyani.                                                                     (alama3)

(c) Umbo la shairi

  • Ni shairi huru
  • Tasdisa / usita/ utenzi/ shairiguni (ubeti 3- Baheri ina mzani saba.) Pia zuhali (mtiririko) Kwa vina vyenye irabu yenye keketo i isipokuwa ubeti wa mwisho wenye irabu u.
  • Kila mshororo una kina kimoja tu cha nje (kipande kimoja)
  • Vina havina urari.

Maelezo yoyote kuhusu vina

Ubeti:

  1. ki, ni,ki,ni,ki,ni.
  2. zi,ni,zi, ni,zi,ni
  3. li,ni,li,ni,li,ni.
  4. mu,ni,mu,ni,mu,ni.
  • Lina kituo kinacho badilikabadilika
  • Mizani: nane kila mshororo
  • Idadi ya beti –nne. (zozote 5×1=5)

(d) Mshairi anasema kuwa duniani hatambuliwi (hathaminiwi). Anatukumbusha kuwa wahenga walisema ‘mkono mtupu haulambwi.’ Kwamba duniani ukiwa huna kitu basi huthaminiwi.                                                      (Alama 4)

(e)            (i) Kiganjani – mkononi /kitangani.

(ii) Kukirimu – kufanya wema, kufadhili fanyia hisani.

(iii) Makubeli- watukufu/ wanadhama /wenye vyeo/ wakubwa.

(iv) Mahashumu – waheshimiwa / makubeli / watukufu.

(v) Wanachuoni – waeledi /wajuzi / wataalamu /wasomi.

  1. (a) Kuishi kwingi ni kuona mengi (alama 1)

(b) Safarini – matatizo yakizidi tusipoteze tumaini kwani huwa tumekaribia kufanikiwa.

  • Masomoni – masomo yakiwa magumu tusiache kusoma, tuuhimize ubongo mpaka uitikie.
  • Katika biashara – hasara ikiingia tusione kama tumefika mwisho. Kufaidika na kuhasarika ni kawaida katika biashara (alama 6)

 

(c) ubeti una mishororo minne (tarbia)

  • Kila mshororo una vipande viwili, ukwapi na utao.
  • Mpangilio wa vina .

_______ni __________ a

_______ni___________a

_______ni___________a

________a__________ni

 

Mizani

________8________8

________8________8

________8________8

________8________8

 

Kibwagizo ni: penye nia ipo njia, usikate tumaini.                                           (alama 1)

  • Mazida- kurefusha maneno k.m “Usikate” tumaini ya “ sikate”

Lahaja     kitwani badala ya kichwani

ndia badala ya njia, n.k.

Inkisari – unalofwatia badala ya “ unalolifuatia”

Kubadili sauti/ kuboronga sarufi – penye nia ipo njia – moyoni mwako amini                 (Tabdila)

Kubainisha ½

Mfano ½                                  (alama 1)

(e)

  • Mshairi ana umri mdogo na hajazoea vituko vya dunia.
  • Babu amekula chumui nyingi na ameona mengi.
  • Sasa ni mzee kwani ana umri mkubwa.
  • Palipo na matumaini hapakosi mafanikio kwa hivyo asikate tamaa.

(alama 4)

  • Aliniusia – alinishauri
  • Mtima –moyo
  • Sukani – kiongozi
  • Waania – shindania                                                                         (alama 4)

 

USHAIRI WA 19

 

Soma shairi hili kisha ujibu maswali yanayofuata

 

Kaka:  Kusoma nilikosoma, kambiwa sipati kazi,

            Yapata mwaka mzima, nategemea shangazi,

Wasiojuwa husema, ‘ sababu sina ujuzi,’

Huno uhaba wa kazi, mesababishwa ni wake.

 

Dada:  Mbona watuingilia, kaka acha ubaguzi,

            Likukeralo twambia, tulijuwe waziwazi,

Au unalochukia ni wake kufanya kazi?

Mambo ya siku hizi,watu ni bega kwa bega.

 

Kaka:  Siwangilie kwa nini, nanyi mwatukopa kazi

            Kwani tokea zamani, hazikuwa shida hizi,

Mtu kitoka shuleni, kibaruwa si tatizi,

Leo hatupati kazi, kisa nyinyi wanawake

 

Dada:  Hapo kaka hujasema, kuwa wake ndiyo chanzi,

Chanzo cha  hii nakama, waume kukosa kazi,

Bure mwatupa lawama, wenyewe mna ajizi,

Mtindo wa siku hizi, watu ni bega kwa bega.

 

Kaka:  Hayo unayotamka, yote niya upuuzi,

            Mumetoroka kupika, kazi yenu toka enzi,

Bilashi mwahangaika, kushabihi vijakazi,

Sasa hatupati kazi, kisa nyinyi wanawake.

 

Dada;  Mbona wafanya ukali, ishakuwa ni chukizi?

            Hata na yangu kauli, umekuwa husikizi,

Nisemaye ni halali,ukweli uliowazi,

Mtindo wa siku hizi, watu ni bega kwa bega.

 

Kaka:  Yana uhalali gani, mbona basi huelezi?

            Kipita maofisini, mumejaa kama inzi,

Mwataka tuwe mekoni, wala halitupendezi,

Na nje hakuna kazi, kisa nyinyi wanawake.

 

Dada:  kakangu una matata, kuyaelewa siwezi,

Wasema unamopita, wambiwa hakuna kazi?

Na sisi wake twapata, haraka pasi ajizi,

Sababu siku hizi, watu ni bega kwa bega.

 

Kaka:  Sisi kazi hatupati, wengi wetu ni mijizi,

Elanyi muna bahati, mabosi hawawaizi,

Hampotezi wakati, ni kidogo pingamizi,

Nasi hatupati kazi, kisa nyingi wanawake..

 

Dada:  kakangu wanichekesha, hadi sina kizuizi,

Vipi lakukasirisha, sisi tukifanya kazi?

Hujui ndivyo maisha, yaendavyo siku hizi?

Mtindo wa siku hizi, watu ni bega kwa bega.

 

Kaka:  Huna haja ya kucheka, nisemayo si upuzi,

Kazi inayojulika, yenu ni kukuna nazi,

Kisha mwenda zianika, mukaziuze takizi,

Leo hatupati kazi, kisa nyinyi wanawake.

 

Dada:  Yalikuwa ni ya kale, kuuza chicha za nazi,

Ela leo twenda mbele, na nyuma hatujibanzi,

Hakuna aliyelele, kushiriki usingizi,

Kwani mambo siku hizi, watu ni bega kwa bega.

 

Kaka:  kulla kitu mwakitaka, kiwe chenu siku hizi,

Ishakuwa na miaka, pia mwataka ihozi,

Nasikia mwatamka, mwaka huno wa ledizi,

Mwisho mutataka myezi, iwe yenu wanawake.

 

 

Hai mana kubishana, nikashabihi mkizi,

Mengi niliyoyanena, yafanyie uchunguzi,

Iwapo tutafanana, yupi taleya vizazi?

Sisi hatupati kazi, hadi murudi mekoni.

 

Dada:  Baba mbele mama nyuma, yamekuwa simulizi,

Muradi sote twasoma, soteni tuwe walezi,

Wake haturudi  nyuma, tunataka mapinduzi,

Maisha ya siku hizi, watu ni bega kwa bega.

 

 

MASWALI

  1. a) Lipe shairi hili kichwa mwafaka. (Alama 2)

 

b)Dada anatoa sababu gani ya wanawake kuajiriwa maofisini?                                 (Alama2)

 

  1. c) Kaka anataja sababu zipi za wanaume kukosa kuajiriwa kazi? (Alama2)

 

  1. d) Eleza umbo la shairi hili (Alama3)

 

e)Dondoa na ueleze mifano miwili tofauti ya uhuru wa kishairi katika shairi            (Alama4)

 

  1. f) Kwa mujibu wa shairi hili, kazi za wanawake ni zipi? (Alama2)

 

  1. g) Eleza ubeti wa mwisho kwa maneno yako mwenyewe (Alama2)

 

  1. h) Eleza maana ya msamiati ufuatao kama ulivyotumiwa katika shairi. (Alama3)

(i) Kulla

(ii)  Nakama

(iii)  Ajizi

 

             MWONGOZO WA KUSAHIHISHIA USHAIRI 19

 

  1. a) i) Uhaba wa kazi
  2. ii) Ukosefu wa kazi

iii)        Wanaume kubaguliwa kazini                                                              ( 1x 2 =2)

 

  1. b) – Miasha ya siku hizi yanahitaji waume na wake, ni sawa kufanya kazi bega kwa

bega.                                                                                                    ( 1 x 2=2)

  1. c) i) Wanawake wameingilia kazi za wanaume
  2. ii) Wanawake kupata kazi ni rahisi kuliko waume kwa sababu wakuu wanawaajiri

kwa maslahi yao wenyewe                                                                 ( 2 x 1= 2)

  1. d) i) Ngonjera         –           majibizano
  2. ii) Tarbia              –           mishororo minne kwa kila ubeti

iii)        Ukara              –           vina vya nje vyatiririka ilhali vya utao vyabadilikabadilika    iv)            Takriri              –           ‘Kisa nyinyi, wanawake’ na ‘watu ni bega kwa bega.

( 3 x 1 = 3)

  1. (Kutaja – alama 1 na kueleza alama 1)
    1. Kuvuruga / kubananga / kufinyanga sarufi

k.m.     –           likukerelo        –           linalokukera

–           Soteni              –           Sote

  1. Tabdila (kubadilisha heruf kimaksudi)

k.m.     –           Inzi      –           nzi

–           Kulla   –           kila

–           tulijuwe-          tulijue

  • Inkisari

–           Kipita  –           nikipita

–           Kitoka             –           akitoka

–           elanyi   –           ela nyinyi.

  1. Kutumia maneno ya lugha nyingine au lahaja

k.v       –           ledizi

–           aliyelele

–           kula                                                                             ( 2 x 2= 4)

 

  1. f) i) Kupika
  2. ii) kukuna nazi (kazi za mekoni)

iii)        kuzaa na kulea wana.                                                                          ( 2 x 1 = 2)

  1. Mambo ya kuwekwa (kutangulizwa) baba au wanaume mbele na wanawake wawe

nyuma yameisha. Maadamu (kwa vile ) sote sisi waume kwa wake tunapata elimu

pamoja – basi vilevile sote tuwe walezi wa watoto. Tusibaguliwe. Moja ikawa kazi

ya mtu  mmoja tu.

Wanawake tutapigana mpaka tupatiwe haki yetu ya usawa. Lazima kupatikane mabadiliko. Maisha ya siku hizi watu wote lazima wawe pamoja, wafanye kazi sawa.

                                                                                                                  ( alama 2)

  1. i)         Kulla   –           kila                                                                              1
  2. ii) Nakama- maangamizo, gharika                                                  1

iii)        Ajiri     –           ugoigoi,ulegevu, uzembe                                            1

 

USHAIRI WA 20

Soma shairi hili kasha ujibu maswali.

  1. Pasi kuhofu lawama, imenibidi kunena,

Nina mengi ya kusema,                       ambayo ni ya maana

Kwetu sote ni lazima,                         viumbe kuambizana,

Yashinda kifo fitina,                           fatani si mtu mwema.

 

  1. Sahau I akilini, yataka kukumbushana,

Madamu tu duniani,                            la kosa huelezana,

Ili tuwe hadharini,                               tujilinde na fitina,

Yashinda kifo fitina,                           fatani si mtu mwema

 

  1. Uchochezi ukitiwa, uwongo unapofana,

Lolote laweza kuwa,                           hata watu kupigana,

Fitina yaweza ua,                                binadamu wengi sana,

Yashinda kifo fitina,                           fatani si mtu mwema.

 

  1. Fatani anapojua, jamii yasikizana,

Aweza leta adawa,                              ya fitina kugombana,

Hata akawa baguwa,                           ndugu wakafarikana,

Yashinda kifo fitina,                           fatani si ntu mwema.

 

  1. Nahakikisha wenzangu, fitina ina laana,

Fitina kwa Bwana Mungu,                 katu hataki iona,

Yasaliti walimwengu,                         mume mke kuachana,

Yashinda kifo fitina,                           fatani si mtu mwema.

 

  1. Fitina si kitu safi, nazidi toa bayana,

Fitina ina makofi,                                muda ukijulikana,

Fitina ni ukorofi,                                 mfano wake hapana,

Yashinda kifo fitina,                           fatani si mtu mwema.

 

  1. Fitina yashinda tusi,                           uovu wa kutukana,

Fitina ina maasi,                                  madhambi ya kujazana,

Fitina ina utesi,                                    tena usowezekana,

Yashinda kifo fitina,                           fatani si mtu mwema

 

  1. Fitina si masihara, yashinda hata khiana,

Fitina ina madhara,                             nchi zaweza gongana,

Fitina aina izara,                                  na aibu nyingi sana,

Yashinda kifo fitina,                           fatani si mtu mwema.

 

  1. Fitina haina shaka, ni mbovu nasema tena,

Fitina mali hakika,                               ya ghibu nawe waona,

Fitina ina mashaka,                             na dhiki kila namna,

Yashinda kifo fitina,                           fatani si mtu mwema.

 

  1. fitina kitu haramu, tamati zaidi sina,

Fitina na binadamu,                            wawe wakichukiana,

Fitina ni mbaya sumu,                         ya au sifa na jina,

Yashinda kifo fitina,                           fatani si mtu, mwema.

 

Maswali:        

(a)        Bainisha athari tano za fitina kulingana na mshairi                                                     (alama 5)

(b)        Ubeti wa sita umechukua mikondo na bahari tofauti tofauti. Zitaje na utoe mifano

(alama 4)

(c)        Andika ubeti wa nne kwa lugha ya nathari (kawaida)                                               (alama 3)

(d)       Mshairi ametumia mbinu zipi kufanya jumbe zake zieleweke kwa bayana zaidi.

(alama 4)

(e)        Eleza maana ya msamiati ufuatao kama ulivyotumika katika shairi.

(i)         Adawa

(ii)        Fatana

(iii)       Wakafarikana

(iv)       Tusi                                                                                                                 (alama 4)

 

Soma shairi hili kisha ujibi maswali yanayofuata.

 

  1. Tusitake kusimama, bila kwanza kusimama,

Au dede kuwa hima, kabla hatujakaa,

Tutakapo kuchutama, kuinama inafaa,

Tujihimu kujinyima, makubwa kutoyavaa.

 

  1. Tusitake kuenenda, guu lisipokomaa,

Tujizonge na mikanda, inapochagiza njaa,

Na mazuri tukipenda, ni lazima kuyandaa,

Tujiase kujipinda, kujepusha na balaa.

 

  1. Tusitake uvulana, au sifa kuzagaa,

Tushikaye nyonga sana, tunuiyapo kupaa,

Kama uweza hapana, tutoelee dagaa,

Tujiase hicho kina, maji yajapokujaa.

 

 

  1. Tusitake vya wenzetu, walochuma kwa hadaa,

Wanaofyatua vitu, na kasha vikasambaa,

Uwezo hatuna katu, umaskini fazaa,

Tujihimu kula vyetu, siendekeze tamaa.

 

  1. Mtaka kuiga watu, kufata kubwa rubaa,

Vyao vijaile kwetu, vifaa vingi vifaa,

Tunamezwa na machatu, tusibakishwe dhiraa,

Tujihimu kilo chetu, hata kama twapagaa.

 

(a)        Lipe shairi hili kichwa mwafaka.                                                                    (alama 1)

(b)        Eleza madhumuni ya shairi hili                                                                       (alama 2)

(c)        shairi hili ni bahari gani? Toa  sababu.                                                            (alama 4)

(d)       Bainisha umbo katika ubeti wa kwanza na wa mwisho ukizingatia vina na mizani.

(alama 4)

 

 

(e)        Andika ubeti wa kwanza kwa lugha nathari.                                                  (alama 4)

(f)        Taja mbinu moja ya kisanii inayoibuka katika ubeti wa nne. Kwa nini

imetumiwa?                                                                                                     (alama 2)

(g)        Eleza msamiati ufuatao kama unavyotokea katika shairi.                               (alama 3)

(i)         Kuiga

(ii)        Dede

(iii)       Tujizonge.

 

MWONGOZO WA KUSAHIHISHIA USHAIRI WA 20

 

6          a)         (i)         Vifo

(ii)        Vita

  • Ugomvi / kuvuruga amani
  • Talaka
  • Ukorofi
  • Chuki zozote 5×1=5

 

  1. b) (i) Tarbia  –           Mishororo minne

(ii)        Kikwamba-     neno / kianzio kimerudiwarudiwa                   2×2=4

 

  1. Mfitini agunduapo jamii yaelewana huleta utengano kwa kuingiza fitina.

Hata anaweza kuwatenganisha ndugu.

Mfitini ni mbaya kushinda kifo / mauti                                  3×1=3

 

  1. d) (i)         Jazanda –         Fitina mbaya sumu

(ii)        Takriri-            Kibwagizo kurudiwarudiwa Neno fitina        2×2=4

  1. e) i)          adawa – uadui
  2. ii) fatani – anayefitini

iii)        wakafarikana – wakatengana, wakawa kando kando

  1. iv) tusi – tukano.                                                                          4 x 1 = 4

 

7          a)                     Kujinyima.

Tusitake makuu.                                                                      (Alama 1)

 

  1. b) Kuhimiza msomaji asiwe na tamaa.

Kuonya dhidi ya kuwa na pupa.                                             1×2=2

 

  1. c) Tarbia –            mishororo minne kila ubeti

Ukara –            Vina vya mwisho vinatiririka.                         2×2=4

 

  1. d) Umbo:             ubeti                                    ubeti        5

mizani          8,8                                        8,8

vina           ma,a                                     tu, a                     4×1=4

 

  1. e) Lugha sufufu.

Tusitamani kusimama kabla ya kutambaa au kabla ya kukaa.

Tunapotaka kuchutama ni lazima tuiname.

Tujifunze kujinyima yale ambayo hatuyawezi                        4×1=4

 

  1. f) Ritifaa –           ‘siendekeze

Sababu-           Kupata urari wa mizani                                   2×1=2

 

  1. Msamiati

(i)         Kuiga –            kufanya afanyavyo mtu mwingine

(ii)        Dede –             Imara, bila kushikilia kitu, bila usaidizi.

(iii)       Tujizonge-       Tujifunge, tujikaze.                                         3×1=3

 

29 Comments

Add a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Optimized by Optimole
Verified by MonsterInsights