
Get the latest Education, TSC, Sports and General News at Educationnewshub.co.ke. Download free Unlimited Notes, Schemes of Work, Lesson Plans, Examination & Assessment Materials.
RATIONALIZED GRADE 6 – KISWAHILI – MUHULA – 1 –
KISWAHILI SAHILI
| WK | L | MADA | KIPINDI | MATOKEO MAALUM TARAJIWA | SHUGHULI ZA MAFUNZO | MASWALI DADISI | NYENZO | TATHMINI | MAONI |
| 1 | MARUDIO Mada mbalimbali Kufikia mwisho wa kipindi mwanafunzi aweze kuyakumbuka aliyoyapitia katika gredi ya TANO ili kujitayarisha kwa kazi mpya – Kuuliza na kujibu maswali ya kauli na ya kimaandishi. Karatasi za mitihani iliyopita -Kujaza mapengo | ||||||||
| VIUNGO VYA MWILI | |||||||||
| 2 | 1 | Kusikiliza na kuzungumza | Matamshi Bora: -Silabi
Sauti: d/nd ch/sh
| Kufikia mwisho wa kipindi, mwanafunzi aweze: -kutambua silabi zinazotokana na sauti zinazokaribiana katika maneno -kutamka silabi zinazotokana na sauti zinazokaribiana kimatamshi ili kuimarisha matamshi
| Mwanafunzi: atambue silabi za sauti, d/nd, ch/sh, (k.v. doa/ndoa, choka/shoka,) kutokana na maneno kwenye vitabu, ubaoni au kwa kutumia vifaa vya kidigitali -atamke silabi za sauti lengwa akiwa peke yake, wakiwa wawiliwawili au katika kikundi | Je, unajua maneno gani yenye silabi za sauti d/nd, ch/sh?
| Timothy Arege na wengine(2022) –Kiswahili Sahili kitabu cha wanafunzi– 6 uk.1-3 -Muongozo wa mwalimu uk.1-4 – Vifaa vya kidijitali – Kapu maneno | -Maswali ya kauli – Kutambua k.m. kwenye orodha -Kuambatanisha maneno
| |
| 2 | Kusikiliza na kuzungumza | Sauti: j/nj g/ng | Kufikia mwisho wa kipindi, mwanafunzi aweze: -kutambua silabi zinazotokana na sauti zinazokaribiana katika maneno -kutamka silabi zinazotokana na sauti zinazokaribiana kimatamshi ili kuimarisha matamshi
| Mwanafunzi: atambue silabi za sauti – j/nj na g/ng kama vile jaa/njaa, Ngoma/ngoma – asikilize silabi za sauti lengwa zikitamkwa na mwalimu, mgeni mwalikwa au kutoka kwa vifaa vya kidigitali (k.v. kinasasauti) -atamke silabi za sauti lengwa akiwa peke yake, wakiwa wawiliwawili au katika kikundi | Je, unajua maneno gani yenye silabi za sauti –j/nj na g/ng?
| Kiswahili Sahili kitabu cha wanafunzi– 6 uk. 1 -Muongozo wa mwalimu uk.1-4 -vifaa vya kijiditali -kapu maneno
| -Maswali ya kauli – Kutambua k.m. kwenye orodha -Kuambatanisha maneno
| ||
| 3 | Kusikiliza na kuzungumza | Vitanza ndimi | Kufikia mwisho wa kipindi mwanafunzi aweze:- -kutamka vitanzandimi vinavyoundwa kwa silabi za sauti zinazokaribiana kimatamshi ili kuimarisha matamshi bora | Mwanafunzi: -asikilize vitanzandimi vinavyoundwa kutokana na maneno yenye sauti lengwa vikikaririwa (k.v. Mkunjo ulikunjwa na waja wenye njaa kukicha) | Je, Unajua vitanzandimi gani vyenye silabi za sauti d/nd, h/sh,? | kitabu cha wanafunzi– 6 uk. 1 -Muongozo wa mwalimu uk.1-4 -vifaa vya kijiditali | -Maswali ya kauli – Kutambua k.m. kwenye orodha -Kuambatanisha maneno
| ||
| 4 | Kusikiliza na kuzungumza | Vitanza ndimi | -kuunda vitanzandimi vyenye maana kutokana na silabi za sauti lengwa ili kukuza ubunifu -kuchangamkia kukariri vitanzandimi vinavyoundwa kwa silabi za sauti zinazokaribiana kimatamshi ili kuimarisha matamshi.
| Mwanafunzi: -aunde vitanzandimi vinavyotokana na vitate husika akiwa peke yake, wawiliwawili au katika vikundi -awasilishe vitanzandimi alivyounda darasani ili wenzake wamtolee maoni -ashiriki katika kutoa maoni kuhusu vitanzandimi vya wenzake kwa upendo na heshima | Je, Unajua vitanzandimi gani vyenye silabi za sauti-, j/nj na g/ng? | Kiswahili Sahili kitabu cha wanafunzi– 6 uk. 1 -Muongozo wa mwalimu uk.1-4 -vifaa vya kijiditali -kapu maneno -uhusika wa wanafunzi | -Maswali ya kauli – Kutambua k.m. kwenye orodha -Kuambatanisha maneno
| ||
| 3 | 1 | –Kusoma | Ufahamu: Kifungu cha Hadithi
| Kufikia mwisho wa kipindi, mwanafunzi aweze: -kutambua msamiati wa suala lengwa uliotumika katika kifungu ili kuimarisha ufahamu -kueleza maana ya msamiati lengwa ili kuubainisha -kusoma kifungu cha hadithi akizingatia ujumbe | Mwanafunzi: -atambue viungo vya mwili vya ndani (k.v. moyo, mapafu, ini, kibofu, wengu, figo, ubongo, mifupa na mishipa) kutokana na picha, chati au kwenye tarakilishi -aeleze maana za msamiati alioutambua asome kifungu kuhusu suala lengwa kwenye kitabu akiwa peke yake, wawiliwawili au katika vikundi
| -Unazingatia nini unaposoma kifungu cha hadithi? -Kusoma kuhusu viungo vya mwili vya ndani kuna umuhimu gani?
| Kiswahili Sahili kitabu cha wanafunzi– 6 uk. -Muongozo wa mwalimu uk.
-kifungu cha hadithi kitabuni -michoro ya | -Kutunga sentensi -kuuliza na kujibu maswali ya kauli -zoezi la kimaandishi | |
| 2 | –Kusoma | Ufahamu: Kifungu cha Hadithi
| Kufikia mwisho wa kipindi, mwanfunzi aweze: -kusoma kifungu cha hadithi akizingatia ujumbe -kuonyesha ufahamu wa kifungu kwa kujibu maswali na kutoa muhtasari -kuchangamkia usomaji ili kuimarisha ufahamu. | Mwanafunzi: -asome kifungu cha hadithi -ajibu maswali kutokana na kifungu husika atoe muhtasari wa kifungu alichosoma -atunge sentensi akitumia msamiati wa suala lengwa uliotumiwa katika kifungu, akiwa peke yake, wawiliwawili au kikundi | -Ni hadithi gani umewahi kuisoma kuhusu viungo vya mwili vya ndani?
| kitabu cha wanafunzi uk. 7 -Muongozo wa mwalimu uk.6 | -Kutunga sentensi -kuuliza na kujibu maswali ya kauli -zoezi la kimaandishi | ||
| 3 | KUANDIKA
| Insha: Insha ya Wasifu
| Kufikia mwisho wa kipindi, mwanfunzi aweze: -kujadili maudhui ya insha ya wasifu kwa kuzingatia mada ili kukuza ubunifu . | -asome vielelezo vya insha ya wasifu vilivyoandikwa katika matini mbalimbali au tarakilishi huku akitambua maudhui -ashirikiane na wenzake kujadili mada na muundo wa insha ya wasifu -akishirikiane na wenzake katika vikundi ili kubainisha na kujadili vidokezo vifaavyo vya mada lengwa -ajadili maudhui ya insha ya wasifu kwa kurejelea mada | -ni kipi cha kuzingatia katika uandishi wa insha? | kitabu cha wanafunzi uk. 9 -Muongozo wa mwalimu uk6 – Maelezo ubaoni -Vifaa vya kidijitali | -Kuandika tungo mbalimbali -Wanafunzi kufanyiana tathmini
| ||
| 4 | KUADIKA
| Insha: Insha ya Wasifu
| -kuandika insha ya wasifu kwa ubunifu ili kujenga maelezo yenye kutoa picha dhahiri -kuchangamkia utunzi wa insha ya wasifu ili kujenga ubunifu | -aonyeshe ubunifu kwa kuandika insha ya wasifu isiyopungua maneno 200 inayohusu mada lengwa kwa kuzingatia, anwani, mpangilio mzuri wa mawazo, hati safi, kanuni za kisarufi na kwa lugha ya kiubunifu -awasomee wenzake insha aliyoandika ili kumpa motisha kuandika zaidi. | In yatakikana iwe na mpangilio upi? | kitabu cha wanafunzi uk. 9 -Muongozo wa mwalimu uk.7-13 – Maelezo ubaoni -Vifaa vya kidijitali | -Kuandika tungo mbalimbali -Wanafunzi kufanyiana tathmini
| ||
| 4 | 1 | SARUFI | Aina za Maneno: Vivumishi vya Sifa
| Kufikia mwisho wa kipindi, mwanfunzi aweze : -kueleza maana ya vivumishi vya sifa ili kuvitofautisha na aina zingine za maneno
| Mwanafunzi: -aeleze maana ya vivumishi lengwa kwa kurejelea vitu au watu katika mazingira yake (k.m.: Mwalimu mzuri, njia ndefu, kijiko kichafu) -atunge sentensi akitumia vivumishi vya sifa | Ni maneno gani unayotumia kuelezea sifa za watu au kitu?
| kitabu cha wanafunzi uk. -Muongozo wa mwalimu uk.7-13 | -Kutambua k.m. kwenye orodha –Kuambatanisha maneno lengwa -Kujaza mapengo | |
| 2 | SARUFI | Aina za Maneno: Vivumishi vya Sifa
| Kufikia mwisho wa kipindi, mwanafunzi aweze: -kutambua vivumishi vya sifa katika matini mbalimbali ili kuvibainisha -kutumia vivumishi vya sifa kutunga sentensi au vifungu vya maneno kwa usahihi | Mwanafunzi: -atambue vivumishi vya sifa (k.v. – zuri, -baya, -refu, -fupi, -ekundu, hodari) katika tarakilishi, kapu la maneno au mti wa maneno akiwa peke yake, wawiliwawili au katika kikundi -atambue vivumishi vya sifa katika sentensi | Ni maneno gani unayotumia kuelezea sifa za watu au kitu?
| kitabu cha wanafunzi uk. -Muongozo wa mwalimu uk.7-13 -kapu maneno -vifaa vya kidijitali -zoezi kitabuni | -Kutambua k.m. kwenye orodha –Kuambatanisha maneno lengwa -Kujaza mapengo | ||
| 3 | SARUFI | Aina za Maneno: Vivumishi vya Sifa
| Kufikia mwisho wa kipindi, mwanafunzi aweze: -kutambua vivumishi vya sifa katika matini mbalimbali ili kuvibainisha -kutumia vivumishi vya sifa kutunga sentensi au vifungu vya maneno kwa usahihi -kufurahia kutumia vivumishi vya sifa katika sentensi au vifungu vya maneno. | -atambue vivumishi vya sifa katika kifungu -aandike sentensi kwa usahihi akitumia vivumishi lengwa akiwa peke yake au katika kikundi -ajaze mapengo kwenye sentensi au vifungu vya maneno kwa kutumia vivumishi lengwa kwenye daftari au kwenye tarakilishi. | Je unaweza kuvitambua vivumishi vya sifa katika vifungu hivi? | kitabu cha wanafunzi uk. -Muongozo wa mwalimu uk.7-13 -kapu maneno -vifaa vya kidijitali -zoezi kitabuni | -Kutambua k.m. kwenye orodha –Kuambatanisha maneno lengwa -Kujaza mapengo | ||
| 4 | SARUFI
| Aina za Maneno: Vivumishi Viashiria
| Kufikia mwisho wa kipindi, mwanafunzi aweze: -kueleza maana ya vivumishi viashiria ipasavyo ili kuvibainisha -kutambua vivumishi viashiria katika matini mbalimbali
| Mwanafunzi: -aeleze maana ya vivumishi lengwa kwa kurejelea vitu vilivyo karibu naye, mbali naye na mbali kabisa (k.m: Kitabu hiki/hicho/kile) -atambue vivumishi viashiria (k.v. huyu, huyo, yule, hivi, hivyo, vile) katika tarakilishi, kapu la maneno au mti wa maneno ili kukuza hamu ya ujifunzaji -atambue vivumishi viashiria katika sentensi -atambue vivumishi katika kifungu | Ni maneno gani unayoweza kutumia kuonyesha umbali wa mtu au kitu? | kitabu cha wanafunzi uk. -Muongozo wa mwalimu uk.7-13 -kapu maneno -vifaa vya kidijitali -zoezi kitabuni | -Kutambua k.m. kwenye orodha –Kuambatanisha maneno lengwa -Kujaza mapengo | ||
| 5 | 1 | SARUFI
| Aina za Maneno: Vivumishi Viashiria
| Kufikia mwisho wa kipindi, mwanfunzi aweze: -kutumia vivumishi viashiria katika sentensi au vifungu vya maneno kwa usahihi -kufurahia kutumia vivumishi viashiria katika sentensi au vifungu vya maneno. | -aandike sentensi akitumia vivumishi lengwa kwa usahihi wakiwa wawiliwawili au kikundi -ajaze mapengo kwenye sentensi au vifungu vya maneno kwa kutumia vivumishi lengwa -atunge sentensi sahihi au vifungu vya maneno katika kifaa cha kidijitali akitumia vivumishi lengwa. | Je unaweza kuvitambua vivumishi vya Viashiria katika vifungu hivi? | kitabu cha wanafunzi uk. -Muongozo wa mwalimu uk.7-13 -kapu maneno -vifaa vya kidijitali -zoezi kitabuni | -Kutambua k.m. kwenye orodha –Kuambatanisha maneno lengwa -Kujaza mapengo | |
| MICHEZO | |||||||||
| 2 | KUSIKILIZA NA KUZUNGUMZA
| Maamkuzi na Maagano
| Kufikia mwisho wa kipindi, mwanafunzi aweze: -kujadili umuhimu maamkuzi na maagano katika mawasiliano -kujadili maamkuzi na maagano yanayotumika katika miktadha mbalimbali
| Mwanafunzi: -ajadili na wenzake umuhimu wa maamkuzi na maagano -atambue maamkuzi mbalimbali na maagano mbalimbali. kutoka kwenye chati, ubao, michoro, picha au vifaa vya kidijitali -ashirikiane na mwenzake kujadili maamkuzi na maagano yanayolengwa na matumizi yake -apewe orodha ya maamkuzi na maagano ili kuyaambatanisha na majibu sahihi kwenye tarakilishi au kitabu | -Kwa nini watu huamkuana?
| kitabu cha wanafunzi uk. 16-19 -Muongozo wa mwalimu uk.14 -chati -picha mbalimbali -video fupi | -Maswali ya kauli – Kutambua k.m. kwenye orodha -Kuambatanisha maneno
| ||
| 3 | KUSIKILIZA NA KUZUNGUMZA
| Maamkuzi na Maagano
| Kufikia mwisho wa kipindi, mwanfunzi aweze: -kutumia aina mbalimbali za maamkuzi na maagano katika mawasiliano -kuchangamkia maamkuzi na maagano katika mahusiano. | -ashirikiane na wenzake kuigiza maamkuzi na maagano lengwa na kuheshimu nafasi ya kila mmoja katika maigizo haya -ahusishe mzazi au mlezi wake kutambua maamkuzi na maagano yanayotumiwa katika jamii yake | -Kuagana kuna umuhimu gani?
| kitabu cha wanafunzi uk.16-19 -Muongozo wa mwalimu uk.15 -picha mbalimbali -video fupi | -Maswali ya kauli – Kutambua k.m. kwenye orodha -Kuambatanisha maneno
| ||
| 4 | KUSOMA | -Kusoma kwa Kina: Matumizi ya Kamusi
| Kufikia mwisho wa kipindi, mwanafunzi aweze: -kutambua maana, tahajia, ngeli na aina za maneno kwa kutumia kamusi
| Mwanafunzi: -ashiriki katika mjadala na wenzake kuhusu jinsi ya kutumia kamusi kutambua maana, tahajia, ngeli, aina za maneno na maana za maneno hayo -asikilize msamiati wa suala lengwa ukisomwa na mwalimu, mgeni mwalikwa au katika kifaa cha kidijitali na kutambua tahajia yake kwa kutumia kamusi akiwa peke yake au katika kikundi -achague maneno kutoka kapu maneno, , kadi maneno au kifaa cha kidijitali na kutambua ngeli, aina na maana za maneno hayo kwa kurejelea kamusi akiwa peke yake au katika kikundi. | -Unatafutaje maana ya maneno kwenye kamusi?
| kitabu cha wanafunzi uk19-22. -Muongozo wa mwalimu uk.17 -makala kitabuni -vifaa vya kidijitali -kamusi -Kadi maneno | -Kutunga sentensi -kuuliza na kujibu maswali ya kauli -zoezi la kimaandishi | ||
| 6 | 1 | KUSOMA | -Kusoma kwa Kina: Matumizi ya Kamusi
| Kufikia mwisho wa kipindi, mwanfunzi aweze: -kutumia kamusi ipasavyo kutafuta maana za maneno mageni yaliyo katika matini aliyosoma ili kukuza msamiati wake -kuchangamkia umuhimu wa kamusi katika kukuza msamiati na sarufi ya Kiswahili. | -atumie kamusi kutafuta maana za maneno mbalimbali akiwa peke yake, wawiliwawili au katika kikundi -atumie mtandao kutafuta maana za maneno -atumie mtandao kusikiliza na kusoma maelezo kuhusu msamiati anaotafutia maana | -Kwa nini tunatumia kamusi?
| kitabu cha wanafunzi uk. 19-22 -Muongozo wa mwalimu uk.18 -makala kitabuni -vifaa vya kidijitali -kamusi -Kadi maneno | -Kutunga sentensi -kuuliza na kujibu maswali ya kauli -zoezi la kimaandishi | |
| 2 | KUANDIKA | Insha ya Masimulizi
| Kufikia mwisho wa kipindi, mwanafunzi aweze: -kueleza muundo na mtindo wa uandishi wa isha ya masimulizi -kubainisha vidokezo vya kutumia katika kuandika insha ya masimulizi
| Mwanafunzi: -ashirikiane na wenzake katika vikundi ili kubainisha na kujadili vidokezo vifaavyo vya mada lengwa -ashirikiane na wenzake kujadili mada na muundo wa insha ya masimulizi na kukuza umilisi wa mawasiliano na ushirikiano -atambue insha ya masimulizi kwa kurejelea vielelezo vya insha zilizoandikwa kwenye matini mbalimbali au tarakilishi | Je, unazingatia nini ili kuandika insha nzuri ya masimulizi? | kitabu cha wanafunzi uk. 22-24 -Muongozo wa mwalimu uk.19 -maelezo kitabuni -insha zilizoandikwa kwenya matini | -Kuandika tungo mbalimbali -Wanafunzi kufanyiana tathmini
| ||
| 3 | KUANDIKA | Insha ya Masimulizi | Kufikia mwisho wa kipindi, mwanfunzi aweze: -kuandika insha ya masimulizi kwa kuzingatia mtindo na muundo wake -kuchangamkia utunzi wa insha ya masimulizi ili kujenga ubunifu. | -aandike insha isiyopungua maneno 200 inayosimulia kisa cha tukio linalohusiana na michezo kwa kuzingatia ubunifu -awasomee wenzake insha aliyoandika ili kuitathmini. | Je, unazingatia nini ili kuandika insha nzuri ya masimulizi? | kitabu cha wanafunzi uk. 22-24 -Muongozo wa mwalimu uk. 20 –maelezo kitabun | -Kuandika tungo mbalimbali -Wanafunzi kufanyiana tathmini | ||
| 4 | SARUFI | Aina za Maneno: Vivumishi vya Idadi
| Kufikia mwisho wa kipindi, mwanafunzi aweze: -kueleza maana ya vivumishi vya idadi ili kuvitofautisha na aina nyingine za vivumishi -kutambua vivumishi vya idadi katika matini | Mwanafunzi: -atambue vivumishi vya idadi katika tarakilishi, kapu la maneno au mti wa maneno. -atambue vivumishi vya idadi katika sentensi -atambue vivumishi vya idadi katika kifungu
| Ni maneno gani unayotumia kutajia idadi ya vitu? | kitabu cha wanafunzi uk24-26. -Muongozo wa mwalimu uk.21 -kapu maneno -vifaa vya kidijitali | -Kutambua k.m. kwenye orodha –Kuambatanisha maneno lengwa -Kujaza mapengo | ||
| 7 | 1 | SARUFI | Aina za Maneno: Vivumishi vya Idadi
| Kufikia mwisho wa kipindi, mwanfunzi aweze: -kutumia vivumishi vya idadi katika sentensi au vifungu vya maneno kwa usahihi -kufurahia kutumia vivumishi vya idadi katika sentensi au vifungu vya maneno. | -aeleze maana ya vivumishi lengwa kwa kurejelea vitu vilivyo katika mazingira yao -aandike sentensi akitumia vivumishi lengwa kwa usahihi wakiwa wawiliwawili au katika kikundi -atunge sentensi sahihi au vifungu vya maneno akitumia vivumishi lengwa. | Ni maneno gani unayotumia kutajia idadi ya vitu? | kitabu cha wanafunzi uk24-26. -Muongozo wa mwalimu uk.21 -kapu maneno -vifaa vya kidijitali -zoezi kitabuni | -Kutambua k.m. kwenye orodha –Kuambatanisha maneno lengwa -Kujaza mapengo | |
| 2 | SARUFI | Aina za Maneno: Vivumishi Viulizi
| Kufikia mwisho wa kipindi, mwanafunzi aweze: -kueleza maana ya vivumishi viulizi ili kuvitofautisha na aina nyingine za vivumishi -kutambua vivumishi viulizi katika matini
| Mwanafunzi: -ashirikiane na wenzake kueleza maana ya vivumishi viulizi -atambue vivumishi viulizi (k.v. –pi? gani?) katika tarakilishi, kapu la maneno au mti wa maneno atambue vivumishi viulizi katika sentensi -atambue vivumishi viulizi katika kifungu kifupi | Ni maneno gani unayotumia kuulizia swali? | kitabu cha wanafunzi uk26-28. -Muongozo wa mwalimu uk.23 -kapu maneno -vifaa vya kidijitali -zoezi kitabuni | -Kutambua k.m. kwenye orodha –Kuambatanisha maneno lengwa -Kujaza mapengo | ||
| 3 | Sarufi | Aina za Maneno: Vivumishi Viulizi
| Kufikia mwisho wa kipindi, mwanfunzi aweze: -kutumia vivumishi viulizi katika sentensi au vifungu vya maneno kwa usahihi -kufurahia kutumia vivumishi viulizi katika sentensi au vifungu vya maneno. | -aeleze maana ya vivumishi lengwa kwa kurejelea vitu vilivyo katika mazingira yake -ajaze mapengo kwenye sentensi au vifungu vya maneno kwa kutumia vivumishi lengwa -atunge sentensi sahihi au vifungu vya maneno akitumia vivumishi lengwa katika daftari lake au katika kifaa cha kidijitali | Vivumishi viulizi hutumiwa wakati upi? | kitabu cha wanafunzi uk26-28. -Muongozo wa mwalimu uk.23 -kapu maneno -vifaa vya kidijitali -zoezi kitabuni | -Kutambua k.m. kwenye orodha –Kuambatanisha maneno lengwa -Kujaza mapengo | ||
| 4 | Sarufi | Aina za Maneno: Vivumishi Viulizi
| Kufikia mwisho wa kipindi, mwanfunzi aweze: -kutumia vivumishi viulizi katika sentensi au vifungu vya maneno kwa usahihi -kufurahia kutumia vivumishi viulizi katika sentensi au vifungu vya maneno. | -aeleze maana ya vivumishi lengwa kwa kurejelea vitu vilivyo katika mazingira yake -ajaze mapengo kwenye sentensi au vifungu vya maneno kwa kutumia vivumishi lengwa -atunge sentensi sahihi au vifungu vya maneno akitumia vivumishi lengwa katika daftari lake au katika kifaa cha kidijitali | Vivumishi viulizi hutumiwa wakati upi? | kitabu cha wanafunzi uk26-28. -Muongozo wa mwalimu uk.23 -kapu maneno -vifaa vya kidijitali -zoezi kitabuni | |||
| 8 | TATHMINI YA MASOMO LIKIZO FUPI | ||||||||
| 9 | 1 | SARUFI | Aina za Maneno: Kivumishi Kirejeshi (amba-)
| Kufikia mwisho wa kipindi, mwanafunzi aweze: -kueleza matumizi ya kivumishi kirejeshi amba- ili kuyabainisha -kutambua kivumishi kirejeshi amba- katik matini | Mwanafunzi: -ashirikiane na wenzake kueleza matumizi ya kivumishi kirejeshi amba– ipasavyo -atambue kivumishi kirejeshi amba- katika tarakilishi, kapu la maneno au mti wa maneno, sentensi, kifungu | Je, unakumbuka aina gani za vivumishi? | kitabu cha wanafunzi uk. 28-30 -Muongozo wa mwalimu uk.25 -kapu maneno -vifaa vya kidijitali -zoezi kitabuni | -Kutambua k.m. kwenye orodha –Kuambatanisha maneno lengwa -Kujaza mapengo | |
| 2 | SARUFI | Aina za Maneno: Kivumishi Kirejeshi (amba-)
| Kufikia mwisho wa kipindi, mwanafunzi aweze: -kutumia kivumishi kirejeshi amba- katika sentensi au vifungu vya maneno kwa usahihi -kufurahia kutumia kivumishi kirejeshi amba- katika sentensi au vifungu vya maneno. | -aeleze maana ya kivumishi lengwa kwa kurejelea vitu vilivyo katika mazingira yake -aandike sentensi akitumia kivumishi lengwa kwa usahihi wakiwa wawiliwawili au kikundi -ajaze mapengo kwenye sentensi au vifungu vya | Je, unakumbuka aina gani za vivumishi? | kitabu cha wanafunzi uk. 28-30 -Muongozo wa mwalimu uk.25 -kapu maneno -vifaa vya kidijitali -zoezi kitabuni | -Kutambua k.m. kwenye orodha –Kuambatanisha maneno lengwa -Kujaza mapengo | ||
| MAHUSIANO | |||||||||
| 3 | KUSIKILIZA NA KUZUNGUMZA | Matamshi Bora: Vitendawili Sauti: -d/nd -ch/sh -j/nj -g/ng | Kufikia mwisho wa kipindi, mwanafunzi aweze: -kutambua vitendawili vyenye sauti zinazokaribiana kimatamshi ili kuvibainisha -kutamka maneno yenye sauti zinazokaribiana kimatamshi katika vitendawili ili kuyatambulisha | Mwanafunzi: -atambue vitendawili vyenye maneno ya sauti d/nd, ch/sh, j/nj, g/ng katika chati, ubao au vifaa vya) -atamke maneno yenye sauti lengwa katika vitendawili
| Je, kwa nini watu hutega na kutegua vitendawili? | kitabu cha wanafunzi uk. 31-32 -Muongozo wa mwalimu uk.27 -uhusika wa wanafunzi -chati iliyoandikwa maneno yenya sauti lengwa | -Kutambua k.m. kwenye orodha –Kuambatanisha maneno lengwa -Kujaza mapengo | ||
| 4 | KUSIKILIZA NA KUZUNGUMZA | Matamshi Bora: Vitendawili Sauti: -d/nd -ch/sh -j/nj -g/ng
| Kufikia mwisho wa kipindi, mwanafunzi aweze: -kutega na kutegua vitendawili vyenye sauti zinazokaribiana kimatamshi ili kujenga matamshi bora -kuchangamkia matumizi ya vitendawili vyenye sauti zinazokaribiana kimatamshi kama njia ya kujenga utamkaji | -ashiriki katika kutega na kutegua vitendawili vyenye sauti zinazokaribiana wakiwa wawiliwawili au katika vikundi -asikilize vitendawili vikitegwa na kuteguliwa kupitia vyombo vya kidijitali. -aandike vitendawili alivyovisikiliza na kuwategea wenzake darasani ili | Je, kwa nini watu hutega na kutegua vitendawili? | kitabu cha wanafunzi uk. 31-32 -Muongozo wa mwalimu uk.27 uhusika wa wanafunzi -chati iliyoandikwa maneno yenya sauti lengwa | -Kutambua k.m. kwenye orodha –Kuambatanisha maneno lengwa -Kujaza mapengo | ||
| 10 | 1 | KUSOMA | Ufahamu: Kifungu cha Hadithi
| Kufikia mwisho wa kipindi, mwanafunzi aweze: -kutambua msamiati wa mahusiano uliotumika katika kifungu ili kuimarisha ufahamu -kueleza maana ya msamiati lengwa ili kuubainisha -kusoma kifungu kwa ufasaha ili kupata ujumbe
| Mwanafunzi: -atambue msamiati unaotumiwa kuonyesha mahusiano kati ya watu katika jamii akitumia kapu maneno, mti maneno au tarakilishi -aeleze maana ya msamiati huu kama unavyotumiwa katika jamii wakati wa mawasiliano -asome kifungu au mchezo mfupi kwa sauti akipishana zamu na wenzake | Kuna umuhimu gani kusoma kuhusu mahusiano? | kitabu cha wanafunzi uk. 32-34 -Muongozo wa mwalimu uk.28
-Kifungu cha hadithi kwenye kitabu -Kamusi -kadi maneno | -Kutunga sentensi -kuuliza na kujibu maswali ya kauli -zoezi la kimaandishi | |
| 2 | KUSOMA | Ufahamu: Kifungu cha Hadithi
| Kufikia mwisho wa kipindi, mwanafunzi aweze: -kusoma kifungu kwa ufasaha ili kupata ujumbe -kuonyesha uelewa wa kifungu kwa kujibu maswali na kutoa muhtasari -kuchangamkia habari au ujumbe kwenye kifungu ili kujenga utamaduni wa usomaji. | -asome kifungu au mchezo mfupi kwa sauti akipishana zamu na wenzake -ajibu maswali kutokana na kifungu -atoe muhtasari kuhusu kifungu alichosoma | Mahusiano huimarisha vipi jamii? | kitabu cha wanafunzi uk. 32-34 -Muongozo wa mwalimu uk.28 -Kifungu cha hadithi kwenye kitabu -zoezi kitabuni | -Kutunga sentensi -kuuliza na kujibu maswali ya kauli -zoezi la kimaandishi | ||
| 3 | KUANDIKA | Kuandika kwa Kutumia Tarakilishi
| Kufikia mwisho wa kipindi, mwanafunzi aweze: -kutambua aina mbalimbali za maandishi ya tarakilishi na ishara zinazotumiwa katika maandishi ya tarakilishi -kuandika kifungu kifupi kuhusu suala lengwa kwa kutumia maandishi mbalimbali yaliyotofautishwa katika tarakilishi -kufurahia utumiaji wa tarakilishi katika kuandika. | Mwanafunzi: -atambue aina mbalimbali za maandishi ya tarakilishi akiwa peke yake, wawilwawili au katika kikundi -ashirikiane na wenzake kutambua ishara zinazotumiwa kutofautisha maandishi akiwa pekee yake au katika kikundi -aandike kwa ubunifu kwenye tarakilishi kifungu cha aya moja ya maneno yasiyopungua 50 kuhusu mahusiano kati ya watu katika jamii | Je, unajua maandishi ya aina gani yanayotumika katika tarakilishi?
| kitabu cha wanafunzi uk. 35-36 -Muongozo wa mwalimu uk.30
-maelezo kitabuni -insha zilizoandikwa kwenya matini | -Kuandika tungo mbalimbali -Wanafunzi kufanyiana tathmini
| ||
| 4 | KUANDIKA | Kuandika kwa Kutumia Tarakilishi | Kufikia mwisho wa kipindi, mwanafunzi aweze: -kuandika kifungu kifupi kuhusu suala lengwa kwa kutumia maandishi mbalimbali yaliyotofautishwa katika tarakilishi -kufurahia utumiaji wa tarakilishi katika kuandika. | -atumie kipanya kuchagua sehemu ya maandishi anayolenga kutofautisha -atumie kipanya kuteua ishara anayotaka kutumia kutofautisha maandishi kama vile ishara ya chapa koza, italiki na kupigia mistari. -aonyeshe ujuzi wa kidijitali kwa kuwatumia wenzake kifungu alichoandika mtandaoni ili wamtolee maoni. | Je, unajua maandishi ya aina gani yanayotumika katika tarakilishi?
| kitabu cha wanafunzi uk. 35-36 -Muongozo wa mwalimu uk.30
-maelezo kitabuni -insha zilizoandikwa kwenya matini | -Kuandika tungo mbalimbali -Wanafunzi kufanyiana tathmini
| ||
| 11 | 1 | SARUFI | Aina za Maneno: Viwakilishi vya Nafsi
| Kufikia mwisho wa kipindi, mwanafunzi aweze: -kueleza maana ya viwakilishi vya nafsi ili kuvitofautisha na viwakilishi vingine -kutambua viwakilishi vya nafsi katika matini mbalimbali
| Mwanafunzi: -ajadili katika kikundi au wawiliwawili maana ya viwakilishi vya nafsi huko akitoa mifano -atambue viwakilishi vya nafsi katika ubao, tarakilishi, kapu la maneno au mti wa maneno, sentensi , kifungu kifupi | Je, ni maneno yapi yanayotumika kuwakilisha nafsi mbalimbali? | kitabu cha wanafunzi uk. 37-40 -Muongozo wa mwalimu uk.32 -kapu maneno -vifaa vya kidijitali -zoezi kitabuni | -Kutambua k.m. kwenye orodha –Kuambatanisha maneno lengwa -Kujaza mapengo | |
| 2 | SARUFI | Aina za Maneno: Viwakilishi vya Nafsi
| Kufikia mwisho wa kipindi, mwanafunzi aweze: -kutumia viwakilishi vya nafsi kwa usahihi katika sentensi -kuonea fahari matumizi ya viwakilishi vya nafsi katika mawasiliano. | -atumie viwakilishi vya nafsi kutunga sentensi kwenye daftari au tarakilishi -ajaze mapengo kwa kutumia viwakilishi vya nafsi ili kukamilisha sentensi kwenye daftari au katika tarakilishi. | Je, ni maneno yapi yanayotumika kuwakilisha nafsi mbalimbali? | kitabu cha wanafunzi uk. 37-40 -Muongozo wa mwalimu uk.32 -kapu maneno -vifaa vya kidijitali -zoezi kitabuni | -Kutambua k.m. kwenye orodha –Kuambatanisha maneno lengwa -Kujaza mapengo | ||
| 3 | SARUFI | Aina za Maneno: Viwakilishi Viashiria
| Kufikia mwisho wa kipindi, mwanafunzi aweze: -kueleza maana ya viwakilishi viashiria ili kuvibainisha -kutambua viwakilishi viashiria katika matini mbalimbali -kutumia viwakilishi viashiria kwa usahihi katika sentensi -kuonea fahari matumizi ya viwakilishi viashiria katika mawasiliano. | Mwanafunzi: -ajadili katika kikundi au wawiliwawili maana ya viwakilishi viashiria huko akitoa mifano mwafaka –atambue viwakilishi viashiria katika ubao, tarakilishi, kapu la maneno au mti wa maneno, sentensi , kifungu kifupi | Je, unajua maneno yapi yanayotumika kuonyesha umbali wa kitu? | kitabu cha wanafunzi uk. 40-42 -Muongozo wa mwalimu uk.34
-kapu maneno -vifaa vya kidijitali -zoezi kitabuni | -Kutambua k.m. kwenye orodha –Kuambatanisha maneno lengwa -Kujaza mapengo | ||
| 4 | SARUFI | Aina za Maneno: Viwakilishi Viashiria
| Kufikia mwisho wa kipindi, mwanafunzi aweze: -kutumia viwakilishi viashiria kwa usahihi katika sentensi -kuonea fahari matumizi ya viwakilishi viashiria katika mawasiliano. | -atambue viwakilishi viashiria katika kifungu kifupi -atunge sentensi akitumia viwakilishi viashiria -ajaze mapengo kwa kutumia viwakilishi viashiria ili kukamilisha sentensi kwenye daftari au katika tarakilishi. | Je, unajua maneno yapi yanayotumika kuonyesha umbali wa kitu | -kapu maneno -vifaa vya kidijitali -zoezi kitabuni
-kapu maneno -vifaa vya kidijitali -zoezi kitabuni | -Kutambua k.m. kwenye orodha –Kuambatanisha maneno lengwa -Kujaza mapengo | ||
| 12 | Marudio ya mada mbalimbali kuanzia mwanzoni mwa muhula | ||||||||
| 13 | TAHMINI YA MWISHO WA MUHULA | ||||||||
Get the latest Mwalimu National Sacco BOSA Loans Application Form {Free Download}, here. PDF Latest…
Here is the revised and latest Mwalimu National Sacco FOSA Salary Advance Application Form {Free…
Here is the latest Mwalimu National Sacco FOSA Instant Loan Application Form {Free Download}. Download…
The landscape of digital gambling has shifted toward high-octane mechanics that prioritize volatility and massive…
The Teachers Service Commission (TSC) has advertised 170 job vacancies across, covering senior, mid‑level, and…
Health Cabinet Secretary Aden Duale has ordered immediate changes to the Social Health Authority (SHA)…