KCPE 2023 Kiswahili Commonly Tested Questions

COMMONLY KCPE TESTED QUESTIONS

KISWAHILI

200 PREDICTION QUESTIONS

                                              Time: 2 Hours 30 Mins

 

Soma vifungu vifuatavyo. Vina nafasi 1 mpaka 15. Jaza mapengo.

Tunapotia guu katika __1__ __2__, walimu wetu wapendwa wanaendelea kutupa__3__huku tukifunzwa mengi kama vile __4__ ambavyo hutoa taarifa kuhusu vitenzi, vivumishi na hata vielezi. Huku hayo yakiendelea, tumepata __5__ kufahamu akisami pia, __6__, __7__ ambayo ni sehemu moja ya saba. Kwa moyo wa shukrani, __8__ kuwapa kongole mzomzo.

 

Kristina alipojiangalia tena__9__ kioo, aligundua kuwa uso wake uliokuwa __10__na kufanya mabaka sasa ulianza kurudisha unyevuunyevu wa awali. __11__ mauti ya mume wake yapata majuma mawili __12__ yalimdhoofisha, __13__ kuwa __14__. Kwa vyovyote vile, ilimpasa kuyazika ya kale na kuendelea na safari ya maisha japo kwa kuuma __15__.

 

Jaza nafasi zilizoachwa wazi kuanzia 16 – 30 kukamilisha vifungu vifuatavyo:-

Nina uhakika __16__ mwendo wa usiku wa manane hivi. Mlio wa __17__ yangu ndio ulionigutusha. Niliinua __18__. Lo! Ilikuwa ni sauti ya Mluna wangu aliyekuwa akizimbua __19__ huko ughaibuni. Baada ya maamkizi, alitaka, bila kupoteza mwia, ni atumie maelezo fulani kwa njia ya faksi. Nami kwa kuwa sikuwa na huduma hiyo ya __20__, nilimweleza ningetuma kwa __21__ “Haidhuru.” alisema. Kutokana na ukosefu wa __22__ simu ilikatika. Hata hivyo, ujumbe ulikuwa umewasilishwa. Bila kupoteza wakati, nilichukua __23__ na kuanza kuandika maelezo yale. Kwa ndege nzuri, tarakilishi hiyo ilikuwa imeunganishwa na __24__. Papo hapo nikamtumia ujumbe.

 

Kukutana __25__ naye kulikuwa kwa sadfa. Nilikuwa __26__ kondeni __27__. __28__. Mara nikamwona kijana Skambe __29__ barasteni. Hali yake ilisikitisha kutokana na __30__ ulevi haramu

 

Soma vifungu vifuatavyo. Vina nafasi 31 hadi 15, Jaza mapengo yaliyomo kwenye vifungo.

Wahenga ______31_______ waliposema kuwa ______32______. Watahiniwa wengi huandika insha ______33______ mithili ya vipofu pasi na kutambua _______34______uandishi wa insha.

Kama yalivyo maswali mengine katika mitihani ______35______ uandishi wa insha vilevile ni ______36______ kujibiwa kwa kuzingatia ______37______ yanayotolewa kabla ya swali lenyewe. Jambo la ajabu ni kwamba, wengi wa wanafunzi huanza tu kuandika ______38______  ya kuisoma sehemu hii muhimu. Amri ya mtahini ni muhimu sana na ni sharti ifuatwe kikamilifu.

 

Fisi alikuwa amezoea _______39________ kwa muda mrefu sana. Maisha yake ya kuiparamia _______40______ na wanyama wengine yalikuwa yamemshinda. Hii ni ______41______ wanyama kama simba na chui waliyateketeza mabaki ya mawindo yao. Aliamua kuanza kufanya ______42______. Alitengeneza silaha kama mishale ili kuwawinda wanyama wengine,jambo ambalo lilikuwa limepingwa vikali na mfalme wao. Tendo hilo lilikuwa ______43______. Juhudi zake ______44______ kwani mishale yake ilikuwa ______45______ na haingemudu kumfuma mnyama yeyote.

 

Soma vifungu vifuatavyo. Vina nafasi 46 mpaka 60. Jaza mapengo.

Ijumaa     46      tulimtembelea Fauzia. Tulipofika kwake     47      kwa mikono miwili.    48     sebuleni ambapo tuliipata familia yake pamoja wakitazama kipindi fulani       49    runinga. Tuliandaliwa      50     wali, nyama, mboga na matunda.     51     mwenyeji kupiga dua, tulianza kula. Tulipomaliza chakula    52   tulishauriana na mwenyeji wetu na    53     kuhusu mradi wetu wa maji     54     utakinufaisha kijiji chetu. Kisha tukamuaga alamsiki naye akatujibu    55   .

Tunapaswa kuwa na moyo wakusaidiana    56    ilivyokuwa zamani.    57    mmoja wetu     58     msaada kwa ajili ya jambo fulani, inafaa tumsaidie bila   59    . Tukifanya hivyo, tutakuwa pia tunajiwekea akiba maishani kwani    60    .

 

Kutoka swali la 61 hadi 120, jibu swali kulingana na maagizo    61.Chagua maelezo yaliyo sahihi.

  1. Arafa: ujumbe wa maandishi unaotumwa kwa simu.
  2. Kipepesi: chombo cha kutuma na kupokea barua.
  3. Kikokotoo: chombo cha kutuma ujumbe kwa sauti.
  4. Mtandao: mfumo wa mawasiliano kupitia tarakilishi.

 

 

  1. Chagua silabi.
    1. Sh
    2. Dha
    3. Ng
    4. Th
  2. Upi ni usemi halisi wa sentensi ifuatayo?

Mwalimu kwa hasira aliwaamuru wanafunzi wote wapige magoti na kumaliza kazi yao ya ziada. Mwalimu

  1. Tambua sentensi yenye kivumishi cha idadi.
    1. Mtumwa huyu ni mtiifu sana.
    2. Kitabu cha kasisi si cheusi.
    3. Jino langu linauma sana.
    4. Kiatu cha kwanza hakifai.
  2. Ni jozi gani iliyokosewa?
    1. Skrubu – bisibisi.
    2. Mpini – jembe.
    3. Mchi – kinu.
    4. Mkufu – kipini.
  3. Ni kiunganishi gani kisichoweza kukamilisha sentensi ifuatayo?

Kauleni aliadhibiwa vikali ________________________ kufukuzwa shuleni.

  1. Tambua sentensi yenye a unganifu.
    1. Cha walimu ni safi.
    2. Kitabu cha mwalimu kimeanguka.
    3. Msipoziba nyufa mtajenga kuta.
    4. Nilimwona alipokuwa akienda maktabani.
  2. Ni kundi gani lenye nominoambata?
    1. Maji, marashi, mate.
    2. Njugumawe, batamzinga, askarikanzu.
    3. Safu ya milima, umati wa watu, kichala cha matunda.
    4. Kenya, Juma, Agosti.
  3. Nomino maskani huwa katika ngeli gani?
  4. Paka huyu ndiye alaye buku katika wingi ni paka hawa 71.Tambua sentensi yenye kielezi.
    1. Katika debe tanna maji.
    2. Kilichosimama ni hiki.
    3. Niliitika kwa sauti.
    4. Mtoto aliyesimama kando ya mto ni mwoga.
  5. Banati ni kwa msichana kama vile ___________________________ ni kwa kaptura.
  6. Chagua nahau iliyo tofauti kimaana.
    1. Aga dunia
    2. Kata kamba
    3. Konga roho
    4. Enda na ulelengoma
  7. Kamilisha methali: Wema 75.Kitendawili:

Mzungu analala na ndevu ziko nie.

  1. Nyambua kitenzi kilichopigwa mstari katika kauli ya kufanyiwa. KUFA
  2. Tambulisha nomino tadunisha na nomino kuza ya neno kiti ni
  3. Chagua sentensi moja yenye maana sawa na ile uliyopewa katika sentensi iliyo hapo chini

Ni heri nivumilie shida kuliko kuiba  a.Ni bora niibe nikiwa na shida

  1. Afadhali nisiibe hata nikiwa na shida
  2. Nisingekuwa na njaa nisingeiba
  3. Niliiba kwa vile nilikuwa na njaa
  1. Tumia kilinganishi sahihi

Matilda-

  1. Anafanana na dada yangu
  2. Anakaa kama dada yangu
  3. Anafanana kama dada yangu
  4. Analingana kama dada yangu
  1. Mbio za farasi ni _________________________
  2. Mzazi wa mke humwita mume wa binti
  3. Taja kiwakilishi katika sentensi

Ninakipenda chakula hiki kwa sababu chenyewe ni kitamu.

  1. Taja neno moja tu linalosimamia fungu zima. Kabaila alizivua nguo akaosha mwili.
  2. Eleza tofauti baina ya sentensi katika jozi (sawia)

i.Mvua ilinyesha ndogo ndogo ii.Mvua ilinyesha kidogo kidogo

  1. Andika jina la kitendo na mtenzi kutokana na KITENZI ulichopewa Rehemu __________________      _________________
  2. Badilisha sentensi hii kwa wingi.

Malkia wa kijiji ana macho ya kikon:be.

  1. Kumramba mtu kisogo ni
  2. Badilisha sentensi ifuatayo katika wakati RUDUFU

Mgeni anakuja kwangu

 

  1. Ni kikundi kipi kilicho na viarifa pekee?
    1. Angua, chomoa, zana, vizuri
    2. Vunja, sana, chora, lia
    3. Polepole, upesi upesi, mbiombio
    4. La, pa, ita, ona
  2. Kamilisha methali ifuatayo:Asiyeona nafsiye _____________________________
  3. Chagua sentensi isiyoakifishwa vizuri
    1. Mwanafunzi bora-aliyeongoza katika mtihani-alituzwa.
    2. Mtu anayeipenda nchi yake (kwa dhati) huitetea zaidi.
    3. Sokoni mlikuwa na matunda mengi: mapera, maparachichi na karakara.
    4. Usilijibu swali lolote,” mtahini alielekeza.
  4. Tambua sentensi yenye vivumishi vya pekee
    1. Mwanariadha hodari alizawadiwa.
    2. Wageni wenyewe waliula mkate wote.
    3. Mtu mzuri ni anayevifanya vitendo vizuri kwa kuradidi.
    4. Shuleni palikuwa na bawabu mwenye maarifa tele.
  5. Ni kitenzi gani kilichoradidiwa katika sentensi zifuatazo?
    1. Anayetembea upesiupesi hufika kwa haraka
    2. Ukiwasemasema watu utakuwa mfitini.
    3. Machungwa yale yale ndiyo yaliyoliwa.
    4. Tulitembea asteaste kuelekea madhabahuni.
  6. Bainisha usemi wa taarifa wa:

“Wanafunzi wawa hawa ndio waliotia fora mtihanini, “mwalimu mkuu alisema.

  1. Neno mwanasesere ina silabi ngapi?
  2. Nenikaribu limetumikaje katika sentensi ifuatayo?

Wastaafu wote walilipwa zaidi ya karibu milioni moja.

  1. Tumia kiunganishi kifaacho.

Ni kwa nini umenmpa funguo za nyumba yako ________________ unajua kuwa yeye ni mwizi?

  1. Andika sentensi ifuatayo bila kirejeshi -amba

Mfanyakazi ambaye atafanya bidii atapandishwa madaraka.

  1. Ni upi wingi wa sentensi hii?

Ubavu wa mnyama wangu umevunjwa na  jirani mwenye wivu.

  1. Kama juzi ilikuwa Jumatano tarehe kumi na nane, mtondo itakuwa siku gani tarehe ngapi?
  2. Ni sentensi ipi yenye maana sawa na Sio nadra wao hutembeleana.
    1. Wao hutembeleana mara chache
    2. Wao hutembeleana mara nyingi
    3. Si mara kwa mara wao hutembeleana
    4. Kutembeleana kwao ni adimu
  3. Ni methali gani yenye maana sawa na:

Ngoja ngoja huumiza mtu matumbo?

  1. Chagua sentensi iliyotumia sitiari.
    1. Maua ni sungura siku hizi.
    2. Moyo wake ulimshauri asikate tamaa.
    3. Alice alijifungua salama salimini.
    4. Ondigo ni mweusi mithili ya masizi.
  2. Andika sentensi ifuatayo katika kauli ya majirani wenye wivu kutendewa Kaguai alienda uwanjani akaucheza mpira. 105. Makao ya mchwa si
  3. Neno, ‘tulimpokea’ lina silabi ngapi 107. Chagua wingi wa sentensi ifuatayo:

Mti ule wa mchungwa ulizaa tunda tamu.

  1. Chagua jibu sahihi:

‘Wachezaji wa soka huhimizana kufanya mazoezi kila siku’. ‘na’ imetumika kuonyesha:

  1. Kufupishwa kwa viwakilishi nafsi.
  2. Hali ya kukubaliana katika jambo.
  3. Wakati usiodhihirika kwenye kitendo.
  4. Mnyambuliko wa kauli ya kutendana.
  1. Ni sentensi ipi ambayo inaunganisha sentensi zifuatazo ipasavyo.

Tamira alipika wali. Wali ulikuwa kwa Riziki.

  1. Wali ulipikwa kwa Riziki na Tamira.
  2. Tamira alipikiwa wali kwa Riziki.
  3. Riziki alipikiwa wali kwa Tamara
  4. Wali ulipikwa kwa Tamira na Riziki.
  1. Ni jibu lipi lenye methali zenye maana sawa?

i.Chanda chema huvikwa pete. ii.Chumia juani ulie kivulini.  iii.Mcheza kwao hutuzwa.

iv.Mfuata nyuki hakosi asali.

  1. (i) (iv)
  2. (ii) (iv)
  3. (i) (iii)
  4. (ii) (iii)
  1. Chagua jibu lisilo ambatanishwa ipasavyo.
    1. – zito kama ndovu
    2. mbio kama duma
    3. – eusi kama mpingo
    4. chungu kama shubiri
  2. Ni kundi lipi la nomino ambalo lipo katika ngeli ya YA-YA
    1. maisha, maagizo
    2. marashi, maarifa
    3. maji, maembe
    4. maskani, mavazi
  3. Rudi ni kurejea ulipokuwa umetoka. Rudi pia ni:
  4. Chagua sentensi iliyoakifishwa vizuri:
    1. Hoyee, Mtoto amecheka kweli?
    2. Je? Unamfahamu karani huyu.
    3. Farida alinunua vifaa vifuatavyo: kitabu, kalamu na kifutio.
    4. Wachezaji walishangilia! baada ya ushindi huo jana jioni.
  5. Jesca anaishi kilomita moja kaskazini mashariki mwa shule yetu. Kibibi naye anaishi kilomita moja kusini mwa shule hiyo. Je, Kibibi anaishi upande gani wa Jesca?
  6. Kauli, ‘Lugogo ni samaki majini’, imetumia tamathali gani ya usemi?
  7. Chagua jibu lenye nomino ya makundi
    1. Mzengwe wa nyuki.
    2. Thurea ya nyota.
    3. Kishazi cha samaki.
    4. Shungi la nywele.
  8. Onyesha sentensi yenye kivumishi.
    1. Mwajuma alisafisha darasa jana.
    2. Gari limefika mapema.
    3. Kule kuna miti mirefu.
    4. Wawili walisajiliwa chuoni.
  9. Ni jibu lipi lenye mapambo ya puani pekee?
    1. Jebu, kipuli
    2. Usinga, udodi
    3. Furungu, njuga
    4. Kipini, kikero
  10. 5/6 kwa maneno ni

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 121 hadi 130.

Hadithi! Hadithi! Hapo zamani za kale kabla ya majabali kukauka, kuku na mwewe walikuwa marafiki wa dhati. Usahibu wao ulikuwa ule wa kufa kuzikana. Waliishi pamoja kwa miaka na mikaka. Walishirikiana na kusaidiana katika lolote lililotokea, la furaha na la majonzi.

Walifanya kazi pamoja. Kila mmoja alijitahidi kadiri ya uwezo wake. Walishirikiana kama kinu na mchi. Bega kwa bega, walifanya kazi zao. Mwewe alijitwika jukumu la kulisha familia zote mbili naye kuku alikuwa na jukumu la kuwalinda watoto wao. Kuku alihakikisha wameshiba na kutulia.

Ndege hawa waliishi kwa amani na utulivu bila kukumbwa na tatizo lililowashinda kutatua. Urafiki wao ulifanya wakati mwingine walale njaa ili watoto wao washibe.

Siku moja walipata barua ya ualishi kutoka kwa ndege wenzao. Karamu ya kukata kwa shoka ilikuwa iandaliwe. Mwewe aliwatayarisha wanawe kwa sherehe. Kuku aligundua kuwa vifaranga wake walikuwa na kucha ndefu zilizowaaibisha. Hivyo, aliamua kumwomba mwewe wen.be. Mwewe alimpa wembe bila kusita kisha akamwambia, “Hakikisha kwamba umerudisha wembe wangu mara moja.”

Kuku alitekeleza wajibu wake kwa haraka. Muda si muda, familia hizo mbili zikang’oa nanga kwa furaha. Karamun, kila mmoja na watoto wake alibugia mapochopocho. Vinywaji vilikuwa tele. Baada ya sherehe, walirejea nyumbani.

Siku iliyofuata, mwewe alimtuma mtoto wake kwa kuku kuuchukua wembe ili wanyolewe. Kuku alipigwa na butwaa alipogundua kwamba wembe wa mwewe haukuwapo. Wasiwasi ulimvamia mara moja. Huku na kule, alianza kuchakurachakura. Jasho lilimtiririka lakini wapi! Juhudi zake hazikumfaa.

Mtoto wa mwewe aliripoti haya kwa mama yake. Bila kungoja, mwewe alifika nyumbani kwa kuku. “Aka! Hujui wewe kuwa wembe huo ni mmoja kama moyo? Lazima nitwae fidia. Nitawala vifaranga wako mmoja mmoja hadi unirejeshee wembe wangu.” Maneno hayo yalimchoma kuku moyoni kama mkuki. Tangu siku hiyo, kuku huchakurachakura huku na kule akiutafuta wembe wa mwewe. Naye mwewe huruka juu akiwasaka vifaranga wa kuku.

  1. Aya ya kwanza inaudokezea kwamba
    1. urafiki wa mwewe na kuku ulikuwa wa unafiki.
    2. mwewe na kuku walitengana sana.
    3. urafiki wa ndege hawa haukuwa wa ukweli.
    4. kuku na mwewe walipendana sana
  2. Neno lililopigiwa mstari mwishoni mwa aya ya kwanza lina maana sawa na a.huzuni.
  3. Katika kifungu ulichosoma, ni nani aliyekuwa akitafuta chakula?
    1. Wote wawili.
    2. Watoto wao.
  4. Mwewe na kuku walishirikiana kama kinu na mchi. Methali inayoafikiana na hali hii ni
    1. bendera hufuata upepo.
    2. baniani mbaya kiatu chake dawa.
    3. kidole kimoja hakivunji chawa.
    4. adui mpende.
  5. Ni nini ambacho kinaonyesha kuwa ndege hawa waliwajali watoto wao?
    1. Kuwatafutia chakula kila siku.
    2. Kuwatetea kila siku.
    3. Kulala njaa ili watoto washibe.
    4. Kwenda karamuni pamoja.
  6. Barua waliyoipata mwewe na kuku
    1. iliandikiwa watoto wao.
    2. iliwaalika katika karamu.
    3. iliwafurahisha sana.
    4. iliwaletea chakula.
  7. Ni kweli kuwa
    1. mwewe alikuwa mwaminifu.
    2. kuku hakuwapenda watoto wake.
    3. watoto wa mwewe walikuwa wachafu.
    4. kuku alikuwa mzembe.
  8. zikang’oa nanga…” ni sawa na
    1. zikaanza safari.
    2. zikakamilisha safari.
    3. zikafika sherehení.
  9. Kulingana na kifungu ulichokisoma, ni nini kilichomtia kuku wasiwasi alipogundua kuwa wembe haukuwapo?
    1. Kuvunjika kwa urafiki wao.
    2. Kunyakuliwa kwa watoto wake.
    3. Onyo alilokuwa amepewa awali.
    4. Kukosa kuhudhuria karamu.
  10. Tabia ya mwewe ya kuruka juu ili kuwasaka vifaranga wa kuku inaonyesha tabia ya
    1. kuonyesha mapenzi.
    2. kutoa onyo.
    3. kulipiza kisasi.

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 131 hadi 140.

Je, ni mnyama yupi mwenye nyayo kama za kasuku, awezaye kutazama pande zote kwa wakati mmoja na mwenye ulimi wenye kasi isiyomithilika? Si ndege, si chura bali ni kinyonga. Kwa makini ukichunguza vidole vya kinyonga, utagundua kuwa, kiaina, vinafanana na vya kasuku. Kila mguu unavyo vidole vitano vyenye upekee wa kuyakamata matawi sawasawa. Aidha, kila kidole kinao ukucha, hivyo, kuwafanya vinyonga wakwezi hodari.

Si miguu yao tu ambayo huajabiwa katika miili yao. Kwa mtazamo wa makini, itadhihirika kuwa katika kila moja ya macho yao, ukope wa juu na wa chini hukaribiana kiasi cha kuacha nafasi ya mboni pekee. Kinyume na binadamu, kinyonga huweza kutazama na kuona pande mbili tofauti mara moja, kwa wakati mmoja. Hili humwezesha kuona kwa nyuzi mia tatu na sitini bila tatizo. Vile vile, wao huwa na uwezo mkubwa wa kuona hususan wakiyaelekeza macho yao yote mawili katika azma moja. Wana uwezo wa kuwaona wadudu wadogo wadogo hata wakiwa mbali. Hili huwasaidia sana wakati wa mawindo.

Ili kulipiza katika utaratibu wao wa kutembea, vinyonga huwa na ndimi ndefu ajabu. Wakati mwingine, ndefu kuliko urefu wa miili yao kwa jumla! Yasemekana kuwa ndimi hizo zao huwa na kasi kiasi kuwa ni vugumu binadamu kuufuatilia mwondoko huo kwa macho. Ni kwa vipi ambavyo ndimi zao huwa na kasi hivyo? Hakika, ndimi zao huwa kama upote na mshale au manati. Jinsi ambavyo upote hurusha mshale ndivyo ambavyo ulimi wa kinyonga hutoka na kuingia kinywani mwake na hivyo kumsaidia kulinasa windo lake.

Talanta nyingine maarufu ya kinyonga ni uwezo wake wa kubadilibadili rangi ya ngozi yake. Anao uwezo wa kujibadili hadi rangi zote za upinde wa mvua na hata zambarau, waridi, nyeusi na hudhurungi. Uwezo huu huwasaidia kujificha kwa kujifananisha na mazingira waliyomo. Hata hivyo, sababu kuu ya uwezo huu huwa kudhibiti kiwango cha joto mwilini na kuelekeza hisia zao. Wao hutumia mabadiliko haya ya rangi kuonyesha hali ya kutamalaki na utetezi katika maeneo wanamoishi. Mabadiliko haya ya rangi aidha hutumika kuwavutia vinyonga wa jinsia tofauti.

Vinyonga wengi hupatikana Afrika. Hata hivyo, matabaka mengine machache yamewahi kushuhudiwa kwingineko kama vile Asia na pia majangwani. Maadamu vinyonga hawana masikio, wao hutumia hisia za mirindimo katika mazingira yao. Hayo yote ya kuajabia kuhusu kinyonga humfanya awe mwanajamii wa kuvutia mno miongoni mwa wanyama jamii ya mamba na mburukenge.

  1. Ni gani hapa si kweli kuhusu kinyonga?
    1. Anao ulimi wenye kasi ya juu.
    2. Nyayo zake hufanana na za kasuku.
    3. Huweza kutazama pande nyingi kwa wakati mmoja.
    4. kwa kiwango fulani, hufanana na chura.
  2. Badala ya kutumia neno lililopigiwa mstari katika aya ya kwanza, mwandishi angetumia
    1. nyoka
  3. Ni nini huwafanya vinyonga kuwa wakwezi hodari?
    1. Miili yao miembamba.
    2. Vidole vyao vitano.
    3. Kucha zao.
    4. Utaratibu wao katika kutembea.
  4. Kwa maoni yako, nafasi za mboni hubakia kwa nini? Ili
    1. kudhibiti kiwango cha nuru.
    2. kuwawezesha vinyonga kuona.
    3. kutenganisha kope za juu na za chini.
    4. kuajabiwa na mwanadamu.
  5. Ni uwezo gani wa vinyonga ambao mwanadamu anaweza kuiga?
    1. Kutazama pande kadhaa kwa wakati mmoja.
    2. Kasi ya ulimi.
    3. Kujibadili rangi.
    4. Utaratibu katika kutembea.
  6. Je, ni gani hapa si sababu ya vinyonga kujibadili rangi?
    1. Kutambulisha hisia zao.
    2. Kupima viwango vyao vya jotomwili.
    3. Kujitofautisha na mazingira wanamoishi.
    4. Kutafuta wenza.
  7. Mwandishi ametaja mambo mangapi ya kuajabia kuhusu kinyonga?
    1. Manane
    2. Saba
    3. Matano
    4. Sita
  8. Sababu kuu ya kinyonga kubadilibadili rangi ni
    1. kujifananisha na mazingira.
    2. kuvutia jinsia tofauti.
    3. kuonyesha hisia zao.
    4. kudhibiti jotomwili.
  9. Mwandishi ametaja uwezo gani wa vinyonga unaowafanya kuwa maarufu?
    1. Uwezo wao wa kukwea miti.
    2. Kasi ya ndimi zao.
    3. Uwezo wao wa kujibadili rangi.
    4. Urefu wa ndimi zao.
  10. Kulingana na msemaji, vinyonga huweza kupatikana katika mabara yapi?
    1. Majangwani na misituni.
    2. Asia na Marekani.
    3. Asia, Afrika, Marekani, misituni na majangwani.
    4. Asia na Afrika.

Soma taarifa ifuatayo kisha ujibu maswali 141-150:-

Ilikuwa Jumamosi. Nilifika nyumbani kwangu saa moja jioni. Tangu nistaafu miaka miwili awali sikupenda kuchelewa Taarifa ya Habari.

Mwezi mmoja ukawa umepita tangu nipewe pesa za kiinua mgongo. Mwezi mmoja mzima nilkuwa katika shughuli za kulipa karo huku. Kuwekeza kwenye mradi ule na kununua hili. Sasa shilingi laki mbili tu zilikuwa zimesalia katika benki.

Watu wengi walinishawishi nijaribu kilimo cha mahindi. Bei ilikuwa imeanza kuimarika. Katika taarifa ya habari jioni hiyo, Waziri wa Kilimo alitangaza bei mpya. Shilingi 1,500 kwa kila gunia. Nami nilikuwa naaza kuumakinikia mradi huu.

Baada ya taarifa, nilikoga, nikala na nikaenda kulala. Kwa sababu ya uchovu, usingizi ulinichukua mara moja. Usingizini niliota. Katika ndoto niliutekeleza mradi wangu. Msimu huo wa kulima nilitenga ekari kumi za shamba langu. Wataalamu walinishauri kuwa wakati mzuri wa kulima ni wa kiangazi. Mwezi wa Januari ulipoanza tu nilitafuta trekta na kulima. Malipo yalikuwa shilingi 1,200 kila ekari. Katikati ya mwezi wa Machi, nilitafuta treka la kutifua shamba tena kwa gharama ya shilingi 15,000 ekari zote kumi. Kufuatia ushauri wa manyakanga wa kilimo, nililipa shilingi elfu kumi na tatu kupiga shamba lote haro.

Mwishoni mwa mwezi huo, nilienda mjini kutafuta pembejeo. Kwanza, nililipa shilingi 20,500 kwa magunia 15 ya mbolea. Kisha nilinunua magunia manne ya mbegu ya mahindi yenye uzani wa kilo 25 kwa shilingi 3,300 kila gunia. Mwezi wa Aprili ulipotimia tu, niliamua kupanda. Ili nipate mazao bora, nilipanda kwa tandazi. Gharama ilikuwa shilingi 1,000 kila ekari. Mvua ilinyesha vizuri na baada ya siku saba, mahindi yalianza kuota. Ilifurahisha kuhesabu mistari ya kijani iliyonyooka. Hali hii iliwezekana tu baada ya kuajiri vijana wa kuwafukuza korongo na vidiri ili wasifukue mbegu mchangani.

Baada ya mwezi mmoja, hatua ya kupalilia ilifika. Nilitafuta vibarua wa kupalilia. Malipo yalikuwa shilingi 700 kila ekari. Kumbe kupalilia kulichochea mtifuko wa mahindi. Punde yakawa yananifikia magotini, Hii ikawa ishara kuwa yanahitaji kumwagiwa mbolea ya kunawirisha iitwayo ‘amonia’. Gharama yake ikawa shilingi 1,300 kila gunia. Hivyo, nikalipa shilingi 19,500 kwa magunia kumi na matano.

Mahindi yalibadilika kimiujiza. Ghafla tu yalirefuka na kunenepa mashina. Yalibadilika rangi yakapiga weusi. Shamba liligeuka likawa kama msitu wa rangi ya kijani iliyokolea. Wapita njia walistajabia mimea na juhudi zangu. Shamba langu sasa likawa kielelezo. Maafisa wa kilimo wakawa kila siku wanawaleta wakulima wengine kujifunza siri ya ufanisi wangu. Hapo nikaanza kuhesabu mavuno nitakayopata na kukadiria faida. Nilipuuza kabisa ushauri wa wahenga kuwa ‘Usikate majani, mnyama hajauawa.

Bila taarifa wala tahadhari mvua ilitoweka. Hayakupita majuma mawili mahindi yakaanza kubadilika. Juma moja baadaye mahindi yalinyauka. Badala ya mahindi, shamba likageuka la vitunguu vilivyochomwa na jua. Makisio yangu ya faida yaliyeyuka jinsi ufanyavyo moshi.

Lakini ‘Muumba ndiye Muumbua.’ Siku moja mawingu yalitanda na mvua ikanyesha. Muda si muda mahindi yalianza kunawiri. Kumbe tukio lililonivunja moyo lilikuwa laja. Siku moja mvua kubwa ilinyesha. Asubuhi nilipotoka nje nilipigwa na butwaa. Barafu ilitapakaa pote. Shamba lilikuwa limetapakaa barafu huku majani ya mahindi yamechanika kama nyuzi. Niliugua. Baada ya wiki moja, nilipata nafuu. Nilipotazama upande wa shamba niliona dalili za majani mapya ya mahindi yakianza kuchomoza. Maumbile ni kitu cha ajabu kweli.

Muda si mrefu mahindi yalirudia hali yake tena, kisha yakakomaa. Harakati za kutafuta watu wa kuyakata na kuyakusanya zilianza. Gharama ya shughuli hii ikawa shilingi 5,000. Kuvuna, kusafirisha kutoka shamba na kukoboa kwa mashine magunia 200 yakachukua shilingi 20,500.

Kufikia hapo nilikuwa nimetumia takribani shilingi 192,700. Gharama nyingine zilikuwa za usafiri, gharama ya dharura na usimamizi, usumbufu wangu binafsi, gharama ya magunia na kadhalika. Mahindi yalipokuwa tayari kwenye magunia, nilifunga safari kwenda mjini kutafuta soko.. Niliposhuka tu niliona gazeti. Habari motomoto siku hiyo ilikuwa: ‘MAHINDI GUNIA 900/= Niligutuka usingizini

  1. Andika kichwa mwafaka kwa kifungu hiki
    1. Mahindi gunia
    2. Mashaka ya kilimo cha gunia
    3. Kiinua mgongo
    4. Usingizi
  2. Msimulizi alikuwa na kiasi gani cha fulusi baada ya mradi kukamilika? Elfu mbili tu
    1. Laki mbili tu
    2. Elfu saba mia tatu
    3. Laki moja mia tisa, mia saba
  3. Kwa mujibu wa kifungu hiki msimulizi alikuwa na matatizo matatu makuu katika zaraa ila
    1. tishio la korongo
    2. tishio la kiangazi
    3. mvua ya barafu
    4. gharama ndogo
  4. Kwa mujibu wa kifungu methali “Muumba ndiye muumba” imetumika. Ni methali ipi iliyo na maana sawa na hiyo?
    1. Aliyekupa wewe kiti ndiye aliyenipa kumbi
    2. Hulka njema sawa na mali
    3. Bahati ya mwenzio usiilalie mlango wazi
    4. Baada ya dhiki faraja
  5. Pamoja na kiwango cha chini cha mavuno ni jambo lipi jingine lililosababisha msimulizi kutopata faida?
    1. Gharama ya kilimo
    2. Kushuka kwa bei
    3. Kutoweka kwa mvua
    4. Tangazo lililokuwa gazetini
  6. Eleza maana ya kiinua mgongo kama lilivyotumika katika kifungu
    1. Mshahara wa mwezi
    2. Mkopo wa kilimo.
    3. Malipo ya kustaafu
    4. Kuinuliwa mgongo juu
  7. Kwa mujibu wa aya ya tano jambo lipi ambalo lilikuwa la mwisho kutendewa na msimulizi
    1. Kuhesabu mistari ya kijani iliyonyoka
    2. Kuenda mjini kutafuta pembejeo
    3. Kuajiri vijana kuwafukuza vidiri na korongo
    4. Kupanda kwa tandazi ili apate mazao bora
  8. Maana ya yalinyauka ni
    1. kauka
    2. kufa
    3. nawiri
    4. stawi
  9. Katika aya ya nane maoni ya msimulizi ni kuwa faida yaliyeyuka ufanyavyo moshi. Huu ni mfano wa
    1. tashbihi
    2. tashdidi
    3. istiari
    4. tanakali
  10. Kulingana na kifungu ni kweli kusema kuwa
    1. mavuno hayakuwa mema
    2. mavuno yalikuwa haba
    3. msimulizi hakutumia ngwenje nyingi
    4. msimulizi alikuwa amestaafu

Soma habari ifuatayo kisha ujibu maswali 151 – 160:- 

Ama kwa hakika, dunia uwanja wa fujo. Vituko vya ulimwengu haviishi. Huzuka kama mizuka kila kunapokucha. Maajabu yaja yakienda. Yote hayo ni mawimbi ya maisha yanayomkumba mwanadamu katika kuishi na kuisha kwake. Lo! Hayo ndiyo malimwengu ulimwenguni.

Nikikaa na kutafakari, huku nikivuta taswira ya mambo kuhusu haya na yale nywele hunisimama, moyo hunidunda, mifupa hunikengeta, nayo damu hunisisimka. Na damu isipowasha hunyeza! Lakini tufanyeje sisi waja wa Mungu ilhali tunajua na kuelewa fika kuwa mja hana hiari na liandikwalo ndilo liwalo? Tunaishi na tuishi kwa rehema na majaliwa ya Jalali. Ewe Mola tunakuhimidi!

Kisa na maana? Hebu nikukumbushe machache tu. Akali ya vituko na vitushi vya hivi karibuni. Bila shaka  nitakuwa nimekusaidia na kukufaa ushughulishe kumbukumbu zako nawe urejee nyuma kidogo. Wazee hukumbuka,  vijana hukumbushwa.

Si miaka mingi sana ulimwengu wetu ulipokumbwa na mvua za mafuriko ya Elnino. Maafa mangapi kama si misiba iliyotusibu. Baadaye tukakumbwa na uhasama wa Osama! Roho nyonge zikanyongwa. Yakaja mawimbi ya kabobo, nyinyi mnayaita Sunami! Vifo vilifisha wengi. Baada ya kidonda moyoni, msumari wa moto juu ya dondandugu. Kabla ya kupona wakazuka ndugu wawili Artur magariani na mwenzake. Nyinyi mkawaita mamluki. Shangaa. Kesho yatazuka yapi? Tahadhari iko wapi? Roho mikononi. Ndugu amkeni tulale tukiwa macho.

  1. Dunia imemithilishwa na uwanja wa fujo kwa nini? Kwa sababu
    1. Kuna vituko vingi mno vya kushangaza
    2. Fujo hutokea duniani
    3. Watu wanafurahishwa na fujo za dunia
    4. Furaha za watu ni kufanya fujo
  2. Tunaambiwa kuwa
    1. vituko vina mwisho, vimeisha
    2. maajabu hayana mwisho, huja yakienda
    3. maajabu ni malimwengu
    4. vituko vya dunia havimtishi mwanadamu 153. “Kuishi na kuisha” kuna mantiki gani?
    5. Kufurahia kuishi na kuisha
    6. Huwezi kuisha bila kuishi
    7. Ukiisha utaishi
    8. Watu wanakuwa hai huku wengine wakifa.
  3. Kulingana na kifungu, nini maana kuvuta taswira?
    1. Kuona picha
    2. Kupiga mambo picha
    3. Kusoma na kuelewa
    4. Kuyakumbuka matukio kwa makini
  4. Nywele husimama, moyo hudunda. Kichwa _________________ ilhali tumbo

__________________

  1. huvuma, hudorota
  2. hutafuna, huzunguka
  3. huwanga, husokota
  4. huruka, huchanganya
  1. Taarifa inatuambia kwamba tunaishi
    1. kwa kudra za Mwenyezi Mungu
    2. kwa kuwa tuna nguvu nyingi
    3. kwa kutumia ujanja
    4. ili Mungu atusaidie
  2. Baadhi ya maafa yaliyowahi kutokea ni pamoja na
    1. yote yaliyosababishwa na uzembe wetu
    2. yaliyo zaidi ya uwezo wetu kuzuia
    3. mengi ambayo tungezuia
    4. dhambi za wanadamu wenyewe
  3. Maafa yaliyosababishwa na nguvu za maji ni kama vile
    1. Elnino na uhasama
    2. Kabobo na Artur
    3. Osama na Artur
    4. Kabobo na Elnino
  4. Miongoni mwa walioaga dunia walikuwepo
    1. Mamluki
    2. Wenye hatia
    3. Wasio na hatia
    4. Waliosababisha kabobo
  5. Bila shaka taarifa hii ni
    1. Kuhusu msiba na huzuni ya maafa
    2. ya kuchekesha
    3. hadithi ya porojo tu
    4. mambo yaliyopita ambayo hayana umuhimu.

Soma taarifa ifuatayo kisha uiibu maswali 161- 170

Akiba ni nini? Kwa kifupi, akiba ni kitu kilichotengwa kwa ajili ya manufaa ya baadaye. Watu wanaoamini akiba huwa wanafahamu kuwa maisha yana nyuso mara mbili: wakati wa mavuno mema na wakati wa mavuno hafifu. Wanazaraa hawa wanafahamu fika kuwa kuna uwezekano wa kupata mavuno kama hayo mbeleni. Taifa linalowajali wazalendo wake huhakikisha kuwa maghala yamejaa vyakula nomi. Akiba maarufu zaidi ni ya kuhifadhi pesa benkini.

Watu wengi duniani wamebakia kuwa walalahoi kwa kutojua wala kutambua namna ya kuweka akiba. Utawasikia wengi wakisema kuwa hakiba huwekwa na waja wenye vipato vikubwa. Kabla ya kufikiria hivyo ni vyema ujue kuwa waliokuwa au walionavyo, mwanzoni hawakuwa navyo. Mtu anaweza kuweka akiba hata kama kipato chake ni cha chini kabisa. Kumbuka kuwa hakiba haiozi na kidogo kidogo hujazaa kibaba.

Wengine hulalamika eti hawawezi kuweka akiba kwani mapato yao huishia tu wanapokidhi matakwa yao ya lazima. Hawajui kwamba iwapo wanataka kuwa na uchumi thabiti katika siku za usoni ni sharti kujinyima. Kukosa kuweka akiba eti kwa kusingizia mshahara mdogo ni kujipumbaza tu. Kuna baadhi ya watu vilevile wanaodhani kuwa wao ni wachanga zaidi kuanza kuweka hifadhi. Kuna wanaofanya mipango mizuri zaidi ya kuzitumia pesa zao lakini tamaa na uchu huwafanya tena kupotoka kabisa. Kupanga kufanya jambo na kisha ukakosa kulitekeleza ni kupoteza muda. Utawaona watu wanalipwa mshahara, wanatumia kila kitu na kuendelea kufanya kazi kungojea mshahara mwingine. Huku ni kuzungukia sehemu moja kama tiara bila kupiga hatua.

Ni jambo la busara sana kuanza kuweka akiba kutoka utotoni. Akiba hizi zinaweza kufanywa kwa njia ayami. Mwanzo mtu anaweza kuwa na mkebe mdogo uliotengenezwa kwa njia ya kipekee. Mkebe huo huwa na kishimo kidogo kinachomwezesha mtu kuweka pesa bila kutoa. Njia nyingine ni kuwa wazazi au walezi wao kuwawekea. Wazazi na walezi wanaweza kuwafungulia watoto wao akaunti kwenye benki. Kuweka pesa benkini ni bora zaidi kuliko akiba nyingine zozote. Hii ni kwa sababu ya ulinzi wa pesa pale benkini. Isitoshe, pesa zinazowekwa kwenye benki huzaa riba. Vilevile pesa hizo zinaweza kuwekezwa kwa njia ambazo faida zitaonekana na mtoto mwenyewe. Mtoto anaweza kununuliwa mifugo kama vile; kuku, sungura, mabata ambao watazaana na kumletea mtoto faida zaidi.

Mtoto anapoona kuwa pesa zake zinaweza kuendelea kuzaa huwa na motisha wa kuendelea kuweka akiba. Mwana akilelewa kwa tamaduni hizi za kuwekeza, kamwe hataacha hata akiwa mtu mzima. Atakuwa na mshawasha wa kuendelea kuzalisha milele. Kuweka akiba kutoka utotoni humfanya mtoto kuwa na pesa za kutosha hata kuyaendeleza masomo yake bila kutegemea wafadhili. Huku ndiko kujitegemea. Mtu anayejitegemea huishi maisha ya amani na raha mstarehe.

Je, wewe tayari una akiba au utaanza kuweka leo? Kumbuka kuwa kuweka akiba ni ishara kubwa zaidi ya kuwa na nidhamu.

  1. Kwa mujibu wa aya ya kwanza,
    1. akiba muhimu zaidi ni za vyakula vya wakulima
    2. akiba huwekwa baada ya kupata mapato mengi
    3. mtu anafaa kuweka akiba hata kama mapato yake ni finyu
    4. maisha kamwe hayana nyuso mbili
  2. Ni kwa nini watu wengi wameishia kuwa maskini kulingana na taarifa uliyoisoma?
    1. Mapato yao ni machache
    2. Wanafahamu fika maana ya kuweka akiba
    3. Wanachelea kuweka akiba wakidhani hawana vya kutosha
    4. Walalahai wameyachukua mapato makubwa wakawamalizia
  3. Chagua methali iliyo kinyume na methali iliyotumiwa katika sentensi ya mwisho wa aya ya pili
    1. Chururu si ndo! ndo! ndo!
    2. Papo kwa papo kamba hukata jiwe
    3. Haba na haba hujaza kibaba
    4. Mchumia juani hulia kivulini
  4. Serikali inawezaje kuwahakikishia watu wake uthabiti wa kiuchumi kulingana na ufahamu?
    1. Kuwashauri watu wake kuweka akiba
    2. Kuwalazimisha wananchi wake kuweka akiba
    3. Kuwapa wananchi wake mapato makubwa ili waweke akiba
    4. Kuwawekea wananchi wake vyakula vya kutosha kwenye maghala
  5. Watu wengi hawapendi kuweka akiba kwa sababu zote hizi ila
    1. wanadhani kuwa mapato yao hayatoshi
    2. wanaona kuwa umri wao ni mdogo mno
    3. wanafanya mipango mizuri lakini hawaitekelezi
    4. mapato yao yanawaruhusu kuweka akiba ndogo mno
  6. Huku ni kuzungukia sehemu moja kama tiara… Ni tamathali gani ya lugha iliyotumiwa hapa?
    1. Tashbihi
    2. Methali
    3. Istiara
    4. Semi
  7. Ni ijambo lipi linalowazuia watu wenye mipango mizuri kuweka akiba?
    1. Mipango yao huwa na kasoro fulani.
    2. Wanayapangia mapato bila kufahau kuwa hayatoshi
    3. Mshahara wao mdogo kukosa kuwaruhusu kuitekeleza mipango yao
    4. Hulka zao za kuvitamani sana vitu vingine
  8. Kati ya mbinu zifuatazo, ni mbinu gani si bora
    1. Kuweka pesa kwenye mkebe maalum
    2. Kuwapa wazazi wao pesa wawawekee
    3. Kuzitumia pesa ili kukirimia matakwa yao
    4. Kuweka pesa kwenye akaunti za benki
  9. Ni kwa nini mtu anafaa kuanza kuweka akiba akiwa na umri mdogo?
    1. Atakuwa tajiri kwa haraka mno
    2. Atakuwa na utamaduni huo maishani
    3. Pesa zake zitakuwa maradufu
    4. Mtu hahitaji kujipanga akiwa ameweka akiba
  10. Mtu anayepoteza kazi yake ilhali ameweka akiba;
    1. atakuwa mtegemeaji wa wengine
    2. anaweza kuanzisha biashara
    3. ataanza kuweka akiba kidogo kidogo
    4. ataweza kwenda ziarani kujivinjari na familia

Soma ufahamu ufuatao kisha ujibu maswali 171-180

Nyanya Matinda alikuwa ametualika twende kumsalimia. Mwanzo aliwauliza wazazi wetu iwapo sote tungepatikana wakati wa sikukuu ya Krismasi. Wengi waliitikia ualishi huo isipokuwa shangazi ambaye aljitetea kuwa binamu yetu Juma angekuwa na shughuli muhimu chuoni. Baada ya majadiliano ya kina na watu wote wa ukoo, uamuzi ulitolewa kuwa twende kumtembelea wakati wa kiburunzi.

Mimi sikuwa nimemwona bibi huyu kwa zaidi ya nusu mwongo. Nilikuwa na mchanganyiko wa furaha na maswali. Furaha kwa kuwa ningepata nafasi ya kuzuru watu wa nyumbani na maswali ya kujua tuliloitiwa. “Je, nyanya anataka kuishia ahera ama vipi? Niliwaza na kuwazua. Nilitaka kuingojea siku hiyo ili nijue dhahiri shahiri. Bibi alikuwa ametayarisha kuchinja ndume wake kuwa kitoweo chetu.

Kufikia saa tisa alasiri tarehe thelathini na moja Desemba, kila mmoja alikuwa amewasili. Mimi ndimi niliyefika karibu wa mwisho. Nilipofika kwa nyanya nilishangazwa na wingi wa watu. Ukweli ni kwamba, singewajua wala kuwatambua wote. Wengi walikuwa ajinabi machoni pangu. Kulikuwa na harufu nzuri ya vyakula hewani. Nilianza kudondokwa na mate bila kujua. Punde si punde, tuliombwa na ami mkuu tuingie ndani sote. Nyumba ya nyanya ilikuwa na bahari ya sebule. Tulimezwa sote na hakukuwa aliyetapikwa hata mmoja. Ilikuwani nyumba ya kisasa iliyojengwa kwa teknolojia mpya.

Pale sebuleni. kila mmoja alionekana akishughulika na simu za mkononi. Wengine walikuwa kwenye mtandao, wengine wakicheza michezo, wengine wakiandika jumbe na wengine wakipiga picha almaarufu ‘selfie”. Mara nyanya Matinda alinyerereka asteaste na kuingia ndani.

Cha ajabu ni kwamba, hakuna aliyemwona isipokuwa mimi. Wote walikuwa na shughuli.

Nyanya alionekana kukasirika. Alitoka shoti na kuingia katika chumba chake cha kulala. Aliporudi alikuwa amebeba gunia. Alikohoa. Kila mmoja aliinua kichwa na kumwangalia. “Hata hamna muda wa kuzungumza mjuane? Simu..simu.simu tu! Kila mmoja aiweke simu yake kwenye gunia hili.” Nyanya alifoka kwa ukali. Tulitii amri ingawa kwa shingo upande.

Sote hatukufurahia lakini tukajibu, “Pole nyanya Matinda kwa kukuudhi'”kwa kauli moja. “Ni kwa nini mmechangamkia elimu ya ulimwengu na huku elimu ya ukoo mmeipoteza? Ni kwa nini hamuwezi kuzungumza mkajuane? Hamjui kwamba dunia imeharibika siku hizi? Hamjawaona ndugu wa damu wakioana kwa kutojua? Ni kwa nini dunia hii inawapotosha wajukuu wangu? Ama nyote mnajuana?” Hapana nyanya,” tulijibu kwa pamoja. “Haya hebu sasa mwangalie mwenzako,” alitoa kauli nyingine.

“Ah! Wajukuu wangu, mmedanganyika na kupotoka kabisa. Hebu tazameni humu mwangu, ni kitu

gani cha kisasa ambacho hakiko? Angalieni runinga yangu na simu yangu. Hivi vyote si vya kisasa? Sasa hebu mniambie iwapo vimenikatiza kujua watu wa ukoo wangu?” Nyanya alisimulia kwa masikitiko.

“Vyombo hivi vyote vya teknolojia ni vyema. Nyinyi ndinyi mnavitumia isivyofaa. Mimi nilipozaliwa

nilipata kuwa kulikuwa na magazeti na televisheni. Baba yangu alikuwa na kijiredio cha mbao ambacho

hakuna hata mmoja aliyeruhusiwa kukigusa.” Tuliangua kicheko. “Acheni kucheka. Hata tulikuwa na

televisheni ya “Sanyo’ ambayo ilionyesha rangi nyeusi na nyeupe.”tulicheka tena. “Isitoshe, kijiji kizima kilifika kwetu wakati wa Magharibi kutazama taarifa ya habari!”

Wakati huo wote tulishindwa kuzuia vicheko. Nyanya pia aliongezea kuwa baba yake alikuwa na saa kubwa sana. Saa hiyo iliyotajwa kuwa ya “Majira’ iikuwa kubwa zaidi kiasi kwamba iliwekwa sakafuni.

Alidokeza kuwa saa hiyo haikutumia betri. Kila mara ungesikia ikitoa sauti kwaa krabu zake, ch!

ch! ch!

Saa ishirini na nne.

Wajukuu wangu, nimemaliza mizungu. Sasa karibuni tule na tufurahie kuwa watu wa ukoo mmoja.” Sinia za minofu zilianza kuletwa mezani.

  1. Familia ya nyanya Matinda ilimtembelea lini kulingana na aya ya kwanza?
    1. Wakati wa Krismasi
    2. Mkesha wa mwaka mpya
    3. Mkesha wa Krismasi
    4. Siku yake ya kuzaliwa
  2. Ni nani aliyetoa sababu ya mwanawe kutopata nafasi tarehe kamili za awali za ualishi?
    1. Binamu yake shangazi
    2. Mtoto wa kiume wa shangazi
    3. Ndugu wa kiume wa mama
    4. Ndugu wa kike wa baba
  3. Msimulizi hakuwa amemtembelea nyanya yake kwa muda wa
    1. zaidi ya miaka mitano
    2. takribani miaka kumi na miwili
    3. zaidi ya miaka kumi
    4. zaidi ya nusu ya mwaka
  4. Unafikiri ni kwa nini mwandishi wa makala haya alifurahia baada ya kupata ualishi?
    1. Alikuwa anajiuliza sababu kuu ya nyanya kuwaita
    2. Alidhani kuwa siku za nyanya zilikuwa zimeyoyoma
    3. Binamu yake alikuwa na shughuli na kwa hivyo hawangeenda
    4. Angepata nafasi ya kutembea nyumbani na kuwaona watu wao
  5. Kifungu, bahari ya sebule, kimepigiwa mstari. Kinamaanisha kuwa
    1. nyumba ya nyanya ilikuwa na bahari ndani
    2. sebuleni palikuwa na kidimbwi kikubwa
    3. sebule ilikuwa kubwa zaidi
    4. bahari iliyokuwapo ilitumeza sote tukapotea
  6. Kulingana na aya ya nne
    1. nyanya Matinda anaonyeshwa kutoipenda mitambo yoyote ya teknolojia
    2. nyanya Matinda anashangaa ni kwa nini wajukuu wamekuwa watumwa wa simu badala ya kujuana
    3. nyanya Matinda anadhani kuwa simutamba huhifadhiwa kwenye gunia
    4. wajukuu wale waliziweka simu zao kwenye gunia kwa hiari
  7. Ni jambo gani linaloonyesha kuwa wajukuu wale walikuwa na heshima?
    1. Hawakuwa wanazungumziana kwa hivyo waliheshimiana
    2. Walimwambia nyanya Matinda pole baada ya kumkasirisha
    3. Walikubali kuziweka simu zao kwenye magunia kwa furaha
    4. Wajukuu wote walikuwa wamemiliki simu ya mkononi.
  8. Kifungu ulichokisoma kimebainisha kwamba elimu ya ukoo
    1. hutuwezesha kufahamu jamaa na koo zetu
    2. hutuwezesha kufahamu ulimwengu wa tovuti
    3. huturahisishia kujua elimu ya dunia
    4. haijapuuzwa na vijana hata kidogo
  9. Kauli zifuatazo zinazotolewa na nyanya zinaonyesha ucheshi isipokuwa masimulizi kuhusu
    1. kuwepo kwa magazeti yaliyosomwa na wakongwe
    2. saa kubwa ajabu ambayo haikutumia betri
    3. runinga iliyotazamwa na karibu kijiji kizima
    4. kuwepo kwa kijiredio cha mbao ambacho hakikuguzwa na yeyote 180. Ni kauli gani iliyo sawa kulingana na makala uliyoyasoma?
    5. Elimu ya ukoo hufunzwa pamoja na elimu za dunia
    6. Hapakuwa na vyombo vya teknolojia hapo zamani
    7. Vyombo vya kiteknolojia ni vyema lakini vinatumiwa visivyo
    8. Vyombo vya teknolojia vililetwa ili kupoteza ukoo wa watu

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 181 mpaka 190.

Mawasiliano ni njia ya kupashana habari kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine. Sijui kama umewahi kuwazia namna watu wa kale walivyotekeleza mchakato huu wa mawasiliano. Kwangu ninaona njia za mawasiliano zilikuwa za ajabu mno. Hebu fikiria kufuka kwa moshi kama ishara ya ujumbe fulani. Je, unafahamu pia milio mbalimbali ilipitisha habari muhimu katika jamii hizo? Kumbuka mbiu ya mgambo wanasema ikilia kuna jambo. Hakika suala la mawasiliano ni nguzo muhimu katika maisha ya binadamu.

Ulimwengu wa sasa umepiga hatua kubwa sana kimaendeleo. Maendeleo hayo yameleta mabadiliko makuu katika mawasiliano. Mfumo wa mawasiliano umewaunganisha waja katika shughuli zao za kila siku. Ilikufanikisha a mawasiliano baina yao, jambo la kimsingi huwa ni kupitisha ujumbe. Wewe mwanafunzi, unapokuwa shuleni kunazo habari muhimu unazohitajika kumfikishia mzazi au mlezi wako. Je, unazifikisha vipi habari hizo?

Fikiria kuhusu wale wanaofanya kazi mbali na familia zao. Unadhani wanawafikishia wapendwa wao taarifa kwa njia gani? Kuna njia nyingi za kuwasilisha ujumbe. Kwa mfano kupiga simu. Vyombo vya habari navyo vinatuwezesha kupitisha ujumbe. Kila siku vinatupasha habari za kila aina. Ni vyema tufahamu kuwa ili mawasiliano yakamilike, basi ujumbe sharti umfikie mlengwa. Mlengwa naye anafaa kuufahamu ujumbe uliokusudiwa.

Tunapopokea ujumbe, tutafakari kuhusu yule aliyetuma ujumbe na ujumbe wenyewe. Sababu kuu ni kubaini lengo kuu la mawasiliano yake. Je, amekusudia nini? Wengi wanaopokea ujumbe wanashindwa kumwelewa aliyetuma ujumbe kutokana na hali ya ujumbe wake. Lugha aliyoitumia inaweza kuwa na utata ambao unatinga kueleweka kwa ujumbe huo. Wengine wanatumia lugha ya mafumbo ambayo labda haieleweki na mlengwa wa ujumbe. Wazia kuwa umemwomba rafiki yako akununulie mbuzi kwa kuwa unahitaji kumfuga nyumbani, kisha ujumbe huu umpige chenga akuletee  kifaa cha kukunia nazi.

Je, utamlaumu au utamcheka mpaka mbavu zivunjike? Iwapo tunahitaji kufanikisha mawasiliano, basi ni muhimu tutumie lugha inayoeleweka vyema. Tukumbuke kuwa, katika lugha, maneno huwa na maana mbalimbali katika muktadha.

Hali ya mpokezi wa ujumbe inaweza kuwa kikwazo cha mawasiliano. Huenda anayepokea ujumbe amekumbwa na hali ambazo zinamkosesha utulivu wa kimawazo. Hali hizo zinaweza kuwa matatizo ya kiafya, majukumu ya malezi na kazi miongoni mwa mengine. Hali hii inaweza kutatiza mkondo wake wa mawazo akakosa makini ya kuufahamu ujumbe uliokusudiwa. Mazingira aliyomo mpokezi wa ujumbe huo, huenda pia yakaathiri uelewa wa ujumbe. Chukulia kwa mfano, umetumwa gulioni kununua bidhaa. Kama ilivyo kawaida, maeneo kama hayo huwa na halaiki ya watu na kelele nyingi. Si muziki, si matangazo ya kibiashara, si mahubiri, yataje yote. Ukipigiwa simu wakati kama huo unaweza kukosa kuisikia.

Iwapo utaisikia upokee, mawasiliano yatatizika bila shaka.

Kufanikiwa kwa shughuli nzima ya mawasiliano kunategemea iwapo aliyetuma ujumbe amepokea majibu kwa mujibu wa ujumbe wake. Ni vyema basi tutafakari kuhusu vikwazo vyote ambavyo vinatatiza mawasiliano. Tukumbuke kuwa mawasiliano yetu hutegemea mahusiano yetu, viwango vyetu vya elimu, mila na desturi na chombo cha mawasiliano kinachotumika miongoni mwa mengine. Kila kipengele kitiliwe maanani kwa kuwa ufanisi wa mawasiliano utategemea uelewa wa ujumbe.

  1. Chagua jibu sahihi kwa mujibu wa aya ya kwanza:
    1. Mwandishi anawahurumia watu wa enzí ya zamani.
    2. Maisha bora ya jamii hutegemea namna tunavyowasiliana na watu wengine.
    3. Utaratibu wa sasa wa kupitisha habari ni bora kuliko wa zamani.
    4. Upashanaji wa habari wa kale uliwashangaza wengi.
  2. Kulingana na aya ya pili:
    1. Mahitaji mbalimbali ya wanajamii yamezua mbinu nyingi za kupashana habari.
    2. Taarifa kutoka shuleni zinachangia uelewa wa mambo ya nyumbani.
    3. Upashanaji wa habari katika jamii hutegemea wanahabari wenyewe.
    4. Ustawi wa jamii unategemea vifaa vya Akiteknolojia pekee. 183. Kulingana na kifungu:
    5. Wahenga waliulizana maswali mengi kuhusu upashanaji wa habari.
    6. Matarajio ya mpokezi wa ujumbe My huathiri ufahamu wa taarifa.
    7. Upataji wa habari kwa wepesi hutegemea ufahamu wa ujumbe.
    8. Lugha tofauti anazozijua mpokezi way ujumbe humwezesha kupokea habari. 184. Ni kauli ipi si sahihi kulingana na aya ya tatu?
    9. Msingi wa upashanaji habari ni kufahamu madhumuni ya anayetuma taarifa.
    10. Kutumia lugha fiche katika ujumbe huharibu uhusiano wa kijamii.
    11. Kiwango cha lugha katika ujumbe huweza kutatiza uelewa wa habari.
    12. Kutoelewa ujumbe kuna madhara kwa anayetuma na kupokea habari.
  3. Kifungu kimebainisha kwamba:

Mawasiliano

  1. yanafaidi wenye simu.
  2. yanaleta familia pamoja.
  3. hufaulu mahali penye utulivu.
  4. humfanya mtu afikirie sana.
  1. Aya ya nne imebainisha kwamba:
    1. Utaratibu wa kupashana habari hutegemea namna mtu anavyofikiria kuhusu maisha.
    2. Kazi anazofanya mtu hutatiza jinsi anavyopokea ujumbe.
    3. Mahali alipo anayetuma ujumbe huweza kuathiri uelewa wa taarifa lengwa.
    4. Upokeaji ujumbe kwa usahihi hutegemea umakinifu wa mpokezi.
  2. Kwa mujibu wa kifungu, lugha ya mawasiliano inafaa
    1. iwe wazi na rahisi kwa mpokezi.
    2. iwe ya kumvutia mpokezi na yenye mafumbo.
    3. kuleta maana mbalimbali kwa mpokezi.
    4. kutuliza fikira za mpokezi wa ujumbe.
  3. Maoni ya mwandishi katika aya ya mwisho ni kwamba:
    1. Ukamilifu wa mawasiliano huamuliwa na muda anaochukua mpokezi kutoa jawabu.
    2. Mawasiliano baina ya binadamu katika jamii huathiriwa na utamaduni wao.
    3. Ujumbe unaopitishwa kwa vifaa vya mawasiliano pekee ni bora zaidi.
    4. Vizuizi vya mawasiliano hutokea pale tunapowaza kuhusu hali ya mpokezi.
  4. Kauli ‘umpige chenga’ imetumia tamathali gani ya usemi?
    1. sitiari
    2. tashbihi
    3. nahau
    4. tashihisi
  5. Maana ya, ‘halaiki ya watu’ kulingana na kifungu ni:
    1. Watu wenye mienendo inayofanana.
    2. Watu wengi waliokusanyika pamoja.
    3. Wataalamu wenye maarifa mengi.
    4. Wauzaji wa bidhaa sokoni.

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 191 mpaka 200.

 

Mimi na Mwamba tulijiunga na shule ya msingi ya Maarifa wakati mmoja. Tangu wakati huo nimemtambua Mwamba kama rafiki wa kuaminika. Tulisoma pamoja, tukacheza pamoja na kushirikiana katika mambo mengi. Alikuwa mmakinifu, msikivu na mchangamfu. Unadhifu wake uliwavutia wengi. Hata mimi aliniathiri nikamuiga. Walimu na wanafunzi walimshabikia na kumthamini hata wakamchagua kuwa kiongozi. Vipawa vya Mwamba vilianza kuchipuka mapema.Naye Mwamba alijitahidi kuvipalilia.

Bidii ya Mwamba inaweza kumithilishwa na ile ya mchwa kujenga kichuguu kwa mate. Mwamba alifahamu fika kuwa mja yeyote kujaliwa ni yeye mwenyewe kujipa uvumilivu, kutia bidii na kushirikiana na wenzake. Alifanya juu chini kuelewa yote tuliyofundishwa na walimu wetu. Ingawa akili yake ilikuwa kama sumaku, pale ambapo alitatizika kuelewa hakufa moyo. Alikuwa tayari wakati wote kujadiliana na wenzake katika vikundi. Alitambua kuwa jifya moja haliinjiki chungu. Pamoja na hayo, Mwamba alijaliwa moyo wa kusaidia. Wakati mwingine katika kundi letu alitufafanulia mada ambazo hatukuzielewa vizuri. Aliwafaa hata wale waliokuwa na changamoto ya kuelewa yaliyofunzwa na walimu. Ama kwa hakika, tulishangazwa na subira na unyenyekevu wake.

Mimi na rafiki yangu Mwamba tulijiunga na timu ya soka ya shule yetu. Alichukua nafasi ya mshambulizi nami nikawa mlinda lango. Kila tuliposhiriki kwenye mashindano, Mwamba aliifungia timu yetu mabao mengi. Mara nyingi, tuliibuka washindi na kuwaacha wapinzani wetu vinywa wazi. Nyota ya Mwamba ilianza kung’aa michezoni. Alipokea tuzo ya mwanasoka bora zaidi katika gatuzi letu. Nayo timu yetu ilinyakua kombe la ushindi na sare kamili za kandanda. Shule yetu ilisifika na kutambulika kama kitovu cha wachezaji kandanda chipukizi. Hata baadhi yetu tulichaguliwa kujiunga na timu ya kitaifa ya vijana.

Mwaka huu, Mwamba amegundua kipawa chake kingine katika rubaa ya muziki baada ya kujiunga na bendi ya muziki shuleni. Wakati wa gwaride na pia sherehe mbalimbali shuleni ameweza kupata nafasi ya kututumbuiza. Sauti yake ya kinanda na nyimbo zake zimevuma kotekote. Kuvuma kwa nyimbo hizo kunatokana na ujumbe wa nyimbo zake. Nyimbo hizo huwahimiza watu kukuza maadili na bidii kila uchao. Hakika, zinatuliza mioyo, zinahimiza, zinachochea watu kuwa na upendo, amani na ushirikiano. Katika siku za hivi majuzi bendi yao imetunga nyimbo ambazo zimevutia wafuasi wengi mitandaoni. Baadhi ya vituo vya mawasiliano vimetuma maombi kualika bendi hiyo kwenye studio zao. Azma yao ni kurekodi baadhi ya nyimbo zao ili zitumike kama milio kwenye simu zinapopigwa au kukiriza. Aidha nyimbo zao huchezwa kwenye vituo mbalimbali vya redio na runinga. Chini ya uongozi wa mwalimu wao, ambaye ni mlezi wa bendi yao, wameweza kujipatia hela ambazo zimetumika kununulia vyombo zaidi vya muziki. Mwalimu huyu wao huhakikisha kuwa bendi hiyo ina nidhamu ya hali ya juu.

Juma lililopita, mwalimu wa zamu aliwapa nafasi wanafunzi kadha kutoa nasaha kuhusu namna ya kufanikiwa masomoni. Mwamba alikuwa miongoni mwao. Hotuba yake ililenga ndipo. Alisema, “Wanafunzi wenzangu, kufaulu kwetu masomoni na pia maishani hakutegemei kule tulikotoka bali nidhamu ya mtu mwenyewe”. Alituambia kuwa achanikaye kwenye mpini hafi njaa. Kwa hivyo, tujitahidi masomoni. Aliongezea kusema kuwa, kila mtu amejaliwa muda wa saa ishirini na nne kila siku. Alituhimiza tuuratibu muda wetu vyema. Katika kuhitimisha hotuba yake alisisitiza tuwaheshimu wakubwa wetu ili tuweze kufanikiwa maishani. Hotuba yake hupigiwa debe shuleni hadi leo.

  1. Chagua jibu sahihi kulingana na aya ya kwanza:
  1. Sifa nzuri za mtu humfanya kutambulikana na wengi.
  2. Wanafunzi wote shuleni walifuata mienendo ya Mwamba.
  3. Viwango vya usafi shuleni viliimarishwa na Mwamba.
  4. Vipaji vya Mwamba vilikuzwa na wenzake wakiwa shuleni.     Aya ya pili imebainisha kwamba:
  5. Mpango wa Mwamba wa kutoa mafunzo ya ziada uliwavutia wote shuleni.
  6. Kufanya jambo kwa pamoja shuleni kulileta mafanikio kwa Mwamba na wenzake.
  7. Mwamba alikuwa na uwezo wa kufahamu yote yaliyofunzwa shuleni kwa wepesi.
  8. Kustaajabia ujuzi wa Mwamba kuliwafanya wanafunzi wote wam- heshimu zaidi.
  9. Chagua jibu lisilo sahihi’ kwa mujibu wa aya ya tatu:

Ushindi wa timu ya soka ya shule ya Maarifa

  1. uliwapa wachezaji nafasi ya kukuza vipawa vyao.
  2. uliwawezesha wachezaji kutambuliwa katika kiwango cha gatuzi lao.
  3. ulifanya shule ya Maarifa kujulikana na wengi.
  4. ulitegemea ustadi wa soka aliokuwa nao Mwamba pekee.     Kifungu kimebainisha kwamba:
  5. Matumaini ya mtu maishani huchangia kufanikiwa kwake.
  6. Uongozi hutegemea idadi ya talanta alizonazo mtu.
  7. Kutambua talanta moja mapema kunamwezesha mtu kuwasaidia wengine kuzua vipaji vyao.
  8. Kuvuma kwa shule ya Maarifa kulito- kana na nyimbo za bendi yake.          Chagua jibu sahihi kwa mujibu wa aya ya nne:
  9. Kila mwaka, Mwamba na wenzake walishirikiana kutambua vipaji vyao.
  10. Vyombo vya habari viliongezea mapato yake kutokana na nyimbo za Mwamba.
  11. Walimu wana jukumu la kuweka msingi mzuri kukuza vipaji vya vijana.
  12. Kualikwa kwa wanabendi studioni kulitegemea vifaa vingi vya muziki walivyonunua.
  13. Mwamba ni mfano bora kwa wenzake kwa kuwa:
    1. Walifuata matendo yake mema.
    2. Walijiunga na bendi ya shule.
    3. Alialikwa kwenye vituo vya habari.
    4. Alihifadhi fedha alizopata kutokana na muziki.
  14. Lipi si jibu sahihi kulingana na aya ya mwisho.

Kufaulu masomoni kunategemea:

  1. Matumizi ya muda wetu.
  2. Mazingira ambayo tumelelewa.
  3. Maamuzi tunayofanya kuhusu elimu yetu.
  4. Mawaidha tunayopata kutoka kwa wenzetu.
  1. Chagua mfuatano sahihi wa matukio yafuatayo kulingana na kifungu.

i.Mwamba kupokea tuzo.

ii.Mwamba kujiunga na bendi ya muziki.

iii.Nyimbo za Mwamba kuvuma. iv.Mwamba kujiunga na timu ya soka.

  1. Nyimbo za Mwamba kuchezwa kwenye vituo vya habari.
    1. (ii) (iii) (v) (iv) (i)
    2. (iv) (iii) (v) (ii) (i)
    3. (ii) (iv) (i) (iii) (v)
    4. (iv) (i) (ii) (iii) (v)
  2. . Kauli, ‘akili yake ilikuwa kama sumaku’ imetumia tamathali gani ya usemi? sitiari
    1. tashbihi
    2. nahau
    3. chuku
  3. Hotuba ya Mwamba hupigiwa debe shuleni mwetu hadi leo ina maana kuwa:
    1. Inasisitizwa kila wakati.
    2. Inashangiliwa mara nyingi.
    3. Inafurahiwa na wote shuleni.
    4. Inafundishwa katika kila darasa.

EXPECTED QUESTIONS IN KCPE 2023

KISWAHILI: SEHEMU BINSHA

Kila mtahiniwa amepewa dakika 40 kwa kila swali kuandika insha ya kusisimua

 

  1. ……….kwa kweli hiyo iliwuwa ni ndoto ya ajabu. (Alama 40)

 

  1. Mwandikie rafiki yako barua ukimwelezea ubora wa utunzaji wa mazingira. Insha yako

isipungue ukurasa mmoja na nusu.                                                                      (Alama 40)

 

  1. ……..Hakika, mtu anapofanya bidi katika jambo lolote hufanikiwa. Mgaagaa na upwa

hali wali mkavu.                                                                                                  (Alama 40) 

  1. Wewe ni mmojawapo wa wanafunzi wa darasa la nane shuleni mwako. Andika hotuba utakayowatolea wanafunzi wengine shuleni kuhusu jinsi ya kuimarisha matokeo yao

katika mithihani.                                                                                                  (Alama 40) 

  1. Wachezaji wat imu zote waliingia uwanjani…………….. (Alama 40)

 

  1. …………….Ni vizuri tuachane na mila ambazo zimwepitwa na wakati. (Alama 40)

 

  1. Ilikuwa siku ya Ijumaa asubuhi na tulikuwa tunaendelea na somo la hisabati. Mara

tukasiskia mayowe kutoka……….                                                                      (Alama 40)

 

  1. …………..Siku hiyo nilielekea nyumbani huku nikielewa kuwa maisha yangu

yangebadilika kabisa.                                                                                          (Alama 40) 

  1. Kuna njia nyingi ambazo vijana wanaweza kutumia kujipatia riziki badala ya kutegemea kazi za ajira pekee……………………. (Alama 40)

 

  1. ………………….nilitanabahi kuwa dawa za kulevya huleta hasara mingi mno.

                                                                                                                             (Alama 40)  ………………………………………………………………………………………………………

………………………………………………………………………………………………………

………………………………………………………………………………………………………

………………………………………………………………………………………………………

………………………………………………………………………………………………………

………………………………………………………………………………………………………

………………………………………………………………………………………………………

………………………………………………………………………………………………………

………………………………………………………………………………………………………

………………………………………………………………………………………………………

………………………………………………………………………………………………………

………………………………………………………………………………………………………

………………………………………………………………………………………………………

………………………………………………………………………………………………………

………………………………………………………………………………………………………

………………………………………………………………………………………………………

………………………………………………………………………………………………………

………………………………………………………………………………………………………

………………………………………………………………………………………………………

………………………………………………………………………………………………………

………………………………………………………………………………………………………

………………………………………………………………………………………………………

………………………………………………………………………………………………………

………………………………………………………………………………………………………

………………………………………………………………………………………………………

PRINT ATLEAST 3 PAGES OF WRITING SPACE FOR EACH COMPOSITION QUESTION.

EXPECTED QUESTIONS IN KCPE 2023

KISWAHILI: SEHEMU BINSHA

Kila mtahiniwa amepewa dakika 40 kwa kila swali kuandika insha ya kusisimua

 

  1. ……….kwa kweli hiyo iliwuwa ni ndoto ya ajabu. (Alama 40)

 

  1. Mwandikie rafiki yako barua ukimwelezea ubora wa utunzaji wa mazingira. Insha yako

isipungue ukurasa mmoja na nusu.                                                                      (Alama 40)

 

  1. ……..Hakika, mtu anapofanya bidi katika jambo lolote hufanikiwa. Mgaagaa na upwa

hali wali mkavu.                                                                                                  (Alama 40) 

  1. Wewe ni mmojawapo wa wanafunzi wa darasa la nane shuleni mwako. Andika hotuba utakayowatolea wanafunzi wengine shuleni kuhusu jinsi ya kuimarisha matokeo yao

katika mithihani.                                                                                                  (Alama 40) 

  1. Wachezaji wat imu zote waliingia uwanjani…………….. (Alama 40)

 

  1. …………….Ni vizuri tuachane na mila ambazo zimwepitwa na wakati. (Alama 40)

 

  1. Ilikuwa siku ya Ijumaa asubuhi na tulikuwa tunaendelea na somo la hisabati. Mara

tukasiskia mayowe kutoka……….                                                                      (Alama 40)

 

  1. …………..Siku hiyo nilielekea nyumbani huku nikielewa kuwa maisha yangu

yangebadilika kabisa.                                                                                          (Alama 40) 

  1. Kuna njia nyingi ambazo vijana wanaweza kutumia kujipatia riziki badala ya kutegemea kazi za ajira pekee……………………. (Alama 40)

 

  1. ………………….nilitanabahi kuwa dawa za kulevya huleta hasara mingi mno.

                                                                                                                             (Alama 40)  ………………………………………………………………………………………………………

………………………………………………………………………………………………………

………………………………………………………………………………………………………

………………………………………………………………………………………………………

………………………………………………………………………………………………………

………………………………………………………………………………………………………

………………………………………………………………………………………………………

………………………………………………………………………………………………………

………………………………………………………………………………………………………

………………………………………………………………………………………………………

………………………………………………………………………………………………………

………………………………………………………………………………………………………

………………………………………………………………………………………………………

………………………………………………………………………………………………………

………………………………………………………………………………………………………

………………………………………………………………………………………………………

………………………………………………………………………………………………………

………………………………………………………………………………………………………

………………………………………………………………………………………………………

………………………………………………………………………………………………………

………………………………………………………………………………………………………

………………………………………………………………………………………………………

………………………………………………………………………………………………………

………………………………………………………………………………………………………

………………………………………………………………………………………………………

PRINT ATLEAST 3 PAGES OF WRITING SPACE FOR EACH COMPOSITION QUESTION.