KCPE 2023 Kiswahili Commonly Tested Questions
COMMONLY KCPE TESTED QUESTIONS
KISWAHILI
200 PREDICTION QUESTIONS
Time: 2 Hours 30 Mins
Soma vifungu vifuatavyo. Vina nafasi 1 mpaka 15. Jaza mapengo.
Tunapotia guu katika __1__ __2__, walimu wetu wapendwa wanaendelea kutupa__3__huku tukifunzwa mengi kama vile __4__ ambavyo hutoa taarifa kuhusu vitenzi, vivumishi na hata vielezi. Huku hayo yakiendelea, tumepata __5__ kufahamu akisami pia, __6__, __7__ ambayo ni sehemu moja ya saba. Kwa moyo wa shukrani, __8__ kuwapa kongole mzomzo.
Kristina alipojiangalia tena__9__ kioo, aligundua kuwa uso wake uliokuwa __10__na kufanya mabaka sasa ulianza kurudisha unyevuunyevu wa awali. __11__ mauti ya mume wake yapata majuma mawili __12__ yalimdhoofisha, __13__ kuwa __14__. Kwa vyovyote vile, ilimpasa kuyazika ya kale na kuendelea na safari ya maisha japo kwa kuuma __15__.
Jaza nafasi zilizoachwa wazi kuanzia 16 – 30 kukamilisha vifungu vifuatavyo:-
Nina uhakika __16__ mwendo wa usiku wa manane hivi. Mlio wa __17__ yangu ndio ulionigutusha. Niliinua __18__. Lo! Ilikuwa ni sauti ya Mluna wangu aliyekuwa akizimbua __19__ huko ughaibuni. Baada ya maamkizi, alitaka, bila kupoteza mwia, ni atumie maelezo fulani kwa njia ya faksi. Nami kwa kuwa sikuwa na huduma hiyo ya __20__, nilimweleza ningetuma kwa __21__ “Haidhuru.” alisema. Kutokana na ukosefu wa __22__ simu ilikatika. Hata hivyo, ujumbe ulikuwa umewasilishwa. Bila kupoteza wakati, nilichukua __23__ na kuanza kuandika maelezo yale. Kwa ndege nzuri, tarakilishi hiyo ilikuwa imeunganishwa na __24__. Papo hapo nikamtumia ujumbe.
Kukutana __25__ naye kulikuwa kwa sadfa. Nilikuwa __26__ kondeni __27__. __28__. Mara nikamwona kijana Skambe __29__ barasteni. Hali yake ilisikitisha kutokana na __30__ ulevi haramu
Soma vifungu vifuatavyo. Vina nafasi 31 hadi 15, Jaza mapengo yaliyomo kwenye vifungo.
Wahenga ______31_______ waliposema kuwa ______32______. Watahiniwa wengi huandika insha ______33______ mithili ya vipofu pasi na kutambua _______34______uandishi wa insha.
Kama yalivyo maswali mengine katika mitihani ______35______ uandishi wa insha vilevile ni ______36______ kujibiwa kwa kuzingatia ______37______ yanayotolewa kabla ya swali lenyewe. Jambo la ajabu ni kwamba, wengi wa wanafunzi huanza tu kuandika ______38______ ya kuisoma sehemu hii muhimu. Amri ya mtahini ni muhimu sana na ni sharti ifuatwe kikamilifu.
Fisi alikuwa amezoea _______39________ kwa muda mrefu sana. Maisha yake ya kuiparamia _______40______ na wanyama wengine yalikuwa yamemshinda. Hii ni ______41______ wanyama kama simba na chui waliyateketeza mabaki ya mawindo yao. Aliamua kuanza kufanya ______42______. Alitengeneza silaha kama mishale ili kuwawinda wanyama wengine,jambo ambalo lilikuwa limepingwa vikali na mfalme wao. Tendo hilo lilikuwa ______43______. Juhudi zake ______44______ kwani mishale yake ilikuwa ______45______ na haingemudu kumfuma mnyama yeyote.
Soma vifungu vifuatavyo. Vina nafasi 46 mpaka 60. Jaza mapengo.
Ijumaa 46 tulimtembelea Fauzia. Tulipofika kwake 47 kwa mikono miwili. 48 sebuleni ambapo tuliipata familia yake pamoja wakitazama kipindi fulani 49 runinga. Tuliandaliwa 50 wali, nyama, mboga na matunda. 51 mwenyeji kupiga dua, tulianza kula. Tulipomaliza chakula 52 tulishauriana na mwenyeji wetu na 53 kuhusu mradi wetu wa maji 54 utakinufaisha kijiji chetu. Kisha tukamuaga alamsiki naye akatujibu 55 .
Tunapaswa kuwa na moyo wakusaidiana 56 ilivyokuwa zamani. 57 mmoja wetu 58 msaada kwa ajili ya jambo fulani, inafaa tumsaidie bila 59 . Tukifanya hivyo, tutakuwa pia tunajiwekea akiba maishani kwani 60 .
Kutoka swali la 61 hadi 120, jibu swali kulingana na maagizo 61.Chagua maelezo yaliyo sahihi.
Mwalimu kwa hasira aliwaamuru wanafunzi wote wapige magoti na kumaliza kazi yao ya ziada. Mwalimu
Kauleni aliadhibiwa vikali ________________________ kufukuzwa shuleni.
Mzungu analala na ndevu ziko nie.
Ni heri nivumilie shida kuliko kuiba a.Ni bora niibe nikiwa na shida
Matilda-
Ninakipenda chakula hiki kwa sababu chenyewe ni kitamu.
i.Mvua ilinyesha ndogo ndogo ii.Mvua ilinyesha kidogo kidogo
Malkia wa kijiji ana macho ya kikon:be.
Mgeni anakuja kwangu
“Wanafunzi wawa hawa ndio waliotia fora mtihanini, “mwalimu mkuu alisema.
Wastaafu wote walilipwa zaidi ya karibu milioni moja.
Ni kwa nini umenmpa funguo za nyumba yako ________________ unajua kuwa yeye ni mwizi?
Mfanyakazi ambaye atafanya bidii atapandishwa madaraka.
Ubavu wa mnyama wangu umevunjwa na jirani mwenye wivu.
Ngoja ngoja huumiza mtu matumbo?
Mti ule wa mchungwa ulizaa tunda tamu.
‘Wachezaji wa soka huhimizana kufanya mazoezi kila siku’. ‘na’ imetumika kuonyesha:
Tamira alipika wali. Wali ulikuwa kwa Riziki.
i.Chanda chema huvikwa pete. ii.Chumia juani ulie kivulini. iii.Mcheza kwao hutuzwa.
iv.Mfuata nyuki hakosi asali.
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 121 hadi 130.
Hadithi! Hadithi! Hapo zamani za kale kabla ya majabali kukauka, kuku na mwewe walikuwa marafiki wa dhati. Usahibu wao ulikuwa ule wa kufa kuzikana. Waliishi pamoja kwa miaka na mikaka. Walishirikiana na kusaidiana katika lolote lililotokea, la furaha na la majonzi.
Walifanya kazi pamoja. Kila mmoja alijitahidi kadiri ya uwezo wake. Walishirikiana kama kinu na mchi. Bega kwa bega, walifanya kazi zao. Mwewe alijitwika jukumu la kulisha familia zote mbili naye kuku alikuwa na jukumu la kuwalinda watoto wao. Kuku alihakikisha wameshiba na kutulia.
Ndege hawa waliishi kwa amani na utulivu bila kukumbwa na tatizo lililowashinda kutatua. Urafiki wao ulifanya wakati mwingine walale njaa ili watoto wao washibe.
Siku moja walipata barua ya ualishi kutoka kwa ndege wenzao. Karamu ya kukata kwa shoka ilikuwa iandaliwe. Mwewe aliwatayarisha wanawe kwa sherehe. Kuku aligundua kuwa vifaranga wake walikuwa na kucha ndefu zilizowaaibisha. Hivyo, aliamua kumwomba mwewe wen.be. Mwewe alimpa wembe bila kusita kisha akamwambia, “Hakikisha kwamba umerudisha wembe wangu mara moja.”
Kuku alitekeleza wajibu wake kwa haraka. Muda si muda, familia hizo mbili zikang’oa nanga kwa furaha. Karamun, kila mmoja na watoto wake alibugia mapochopocho. Vinywaji vilikuwa tele. Baada ya sherehe, walirejea nyumbani.
Siku iliyofuata, mwewe alimtuma mtoto wake kwa kuku kuuchukua wembe ili wanyolewe. Kuku alipigwa na butwaa alipogundua kwamba wembe wa mwewe haukuwapo. Wasiwasi ulimvamia mara moja. Huku na kule, alianza kuchakurachakura. Jasho lilimtiririka lakini wapi! Juhudi zake hazikumfaa.
Mtoto wa mwewe aliripoti haya kwa mama yake. Bila kungoja, mwewe alifika nyumbani kwa kuku. “Aka! Hujui wewe kuwa wembe huo ni mmoja kama moyo? Lazima nitwae fidia. Nitawala vifaranga wako mmoja mmoja hadi unirejeshee wembe wangu.” Maneno hayo yalimchoma kuku moyoni kama mkuki. Tangu siku hiyo, kuku huchakurachakura huku na kule akiutafuta wembe wa mwewe. Naye mwewe huruka juu akiwasaka vifaranga wa kuku.
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 131 hadi 140.
Je, ni mnyama yupi mwenye nyayo kama za kasuku, awezaye kutazama pande zote kwa wakati mmoja na mwenye ulimi wenye kasi isiyomithilika? Si ndege, si chura bali ni kinyonga. Kwa makini ukichunguza vidole vya kinyonga, utagundua kuwa, kiaina, vinafanana na vya kasuku. Kila mguu unavyo vidole vitano vyenye upekee wa kuyakamata matawi sawasawa. Aidha, kila kidole kinao ukucha, hivyo, kuwafanya vinyonga wakwezi hodari.
Si miguu yao tu ambayo huajabiwa katika miili yao. Kwa mtazamo wa makini, itadhihirika kuwa katika kila moja ya macho yao, ukope wa juu na wa chini hukaribiana kiasi cha kuacha nafasi ya mboni pekee. Kinyume na binadamu, kinyonga huweza kutazama na kuona pande mbili tofauti mara moja, kwa wakati mmoja. Hili humwezesha kuona kwa nyuzi mia tatu na sitini bila tatizo. Vile vile, wao huwa na uwezo mkubwa wa kuona hususan wakiyaelekeza macho yao yote mawili katika azma moja. Wana uwezo wa kuwaona wadudu wadogo wadogo hata wakiwa mbali. Hili huwasaidia sana wakati wa mawindo.
Ili kulipiza katika utaratibu wao wa kutembea, vinyonga huwa na ndimi ndefu ajabu. Wakati mwingine, ndefu kuliko urefu wa miili yao kwa jumla! Yasemekana kuwa ndimi hizo zao huwa na kasi kiasi kuwa ni vugumu binadamu kuufuatilia mwondoko huo kwa macho. Ni kwa vipi ambavyo ndimi zao huwa na kasi hivyo? Hakika, ndimi zao huwa kama upote na mshale au manati. Jinsi ambavyo upote hurusha mshale ndivyo ambavyo ulimi wa kinyonga hutoka na kuingia kinywani mwake na hivyo kumsaidia kulinasa windo lake.
Talanta nyingine maarufu ya kinyonga ni uwezo wake wa kubadilibadili rangi ya ngozi yake. Anao uwezo wa kujibadili hadi rangi zote za upinde wa mvua na hata zambarau, waridi, nyeusi na hudhurungi. Uwezo huu huwasaidia kujificha kwa kujifananisha na mazingira waliyomo. Hata hivyo, sababu kuu ya uwezo huu huwa kudhibiti kiwango cha joto mwilini na kuelekeza hisia zao. Wao hutumia mabadiliko haya ya rangi kuonyesha hali ya kutamalaki na utetezi katika maeneo wanamoishi. Mabadiliko haya ya rangi aidha hutumika kuwavutia vinyonga wa jinsia tofauti.
Vinyonga wengi hupatikana Afrika. Hata hivyo, matabaka mengine machache yamewahi kushuhudiwa kwingineko kama vile Asia na pia majangwani. Maadamu vinyonga hawana masikio, wao hutumia hisia za mirindimo katika mazingira yao. Hayo yote ya kuajabia kuhusu kinyonga humfanya awe mwanajamii wa kuvutia mno miongoni mwa wanyama jamii ya mamba na mburukenge.
Soma taarifa ifuatayo kisha ujibu maswali 141-150:-
Ilikuwa Jumamosi. Nilifika nyumbani kwangu saa moja jioni. Tangu nistaafu miaka miwili awali sikupenda kuchelewa Taarifa ya Habari.
Mwezi mmoja ukawa umepita tangu nipewe pesa za kiinua mgongo. Mwezi mmoja mzima nilkuwa katika shughuli za kulipa karo huku. Kuwekeza kwenye mradi ule na kununua hili. Sasa shilingi laki mbili tu zilikuwa zimesalia katika benki.
Watu wengi walinishawishi nijaribu kilimo cha mahindi. Bei ilikuwa imeanza kuimarika. Katika taarifa ya habari jioni hiyo, Waziri wa Kilimo alitangaza bei mpya. Shilingi 1,500 kwa kila gunia. Nami nilikuwa naaza kuumakinikia mradi huu.
Baada ya taarifa, nilikoga, nikala na nikaenda kulala. Kwa sababu ya uchovu, usingizi ulinichukua mara moja. Usingizini niliota. Katika ndoto niliutekeleza mradi wangu. Msimu huo wa kulima nilitenga ekari kumi za shamba langu. Wataalamu walinishauri kuwa wakati mzuri wa kulima ni wa kiangazi. Mwezi wa Januari ulipoanza tu nilitafuta trekta na kulima. Malipo yalikuwa shilingi 1,200 kila ekari. Katikati ya mwezi wa Machi, nilitafuta treka la kutifua shamba tena kwa gharama ya shilingi 15,000 ekari zote kumi. Kufuatia ushauri wa manyakanga wa kilimo, nililipa shilingi elfu kumi na tatu kupiga shamba lote haro.
Mwishoni mwa mwezi huo, nilienda mjini kutafuta pembejeo. Kwanza, nililipa shilingi 20,500 kwa magunia 15 ya mbolea. Kisha nilinunua magunia manne ya mbegu ya mahindi yenye uzani wa kilo 25 kwa shilingi 3,300 kila gunia. Mwezi wa Aprili ulipotimia tu, niliamua kupanda. Ili nipate mazao bora, nilipanda kwa tandazi. Gharama ilikuwa shilingi 1,000 kila ekari. Mvua ilinyesha vizuri na baada ya siku saba, mahindi yalianza kuota. Ilifurahisha kuhesabu mistari ya kijani iliyonyooka. Hali hii iliwezekana tu baada ya kuajiri vijana wa kuwafukuza korongo na vidiri ili wasifukue mbegu mchangani.
Baada ya mwezi mmoja, hatua ya kupalilia ilifika. Nilitafuta vibarua wa kupalilia. Malipo yalikuwa shilingi 700 kila ekari. Kumbe kupalilia kulichochea mtifuko wa mahindi. Punde yakawa yananifikia magotini, Hii ikawa ishara kuwa yanahitaji kumwagiwa mbolea ya kunawirisha iitwayo ‘amonia’. Gharama yake ikawa shilingi 1,300 kila gunia. Hivyo, nikalipa shilingi 19,500 kwa magunia kumi na matano.
Mahindi yalibadilika kimiujiza. Ghafla tu yalirefuka na kunenepa mashina. Yalibadilika rangi yakapiga weusi. Shamba liligeuka likawa kama msitu wa rangi ya kijani iliyokolea. Wapita njia walistajabia mimea na juhudi zangu. Shamba langu sasa likawa kielelezo. Maafisa wa kilimo wakawa kila siku wanawaleta wakulima wengine kujifunza siri ya ufanisi wangu. Hapo nikaanza kuhesabu mavuno nitakayopata na kukadiria faida. Nilipuuza kabisa ushauri wa wahenga kuwa ‘Usikate majani, mnyama hajauawa.
Bila taarifa wala tahadhari mvua ilitoweka. Hayakupita majuma mawili mahindi yakaanza kubadilika. Juma moja baadaye mahindi yalinyauka. Badala ya mahindi, shamba likageuka la vitunguu vilivyochomwa na jua. Makisio yangu ya faida yaliyeyuka jinsi ufanyavyo moshi.
Lakini ‘Muumba ndiye Muumbua.’ Siku moja mawingu yalitanda na mvua ikanyesha. Muda si muda mahindi yalianza kunawiri. Kumbe tukio lililonivunja moyo lilikuwa laja. Siku moja mvua kubwa ilinyesha. Asubuhi nilipotoka nje nilipigwa na butwaa. Barafu ilitapakaa pote. Shamba lilikuwa limetapakaa barafu huku majani ya mahindi yamechanika kama nyuzi. Niliugua. Baada ya wiki moja, nilipata nafuu. Nilipotazama upande wa shamba niliona dalili za majani mapya ya mahindi yakianza kuchomoza. Maumbile ni kitu cha ajabu kweli.
Muda si mrefu mahindi yalirudia hali yake tena, kisha yakakomaa. Harakati za kutafuta watu wa kuyakata na kuyakusanya zilianza. Gharama ya shughuli hii ikawa shilingi 5,000. Kuvuna, kusafirisha kutoka shamba na kukoboa kwa mashine magunia 200 yakachukua shilingi 20,500.
Kufikia hapo nilikuwa nimetumia takribani shilingi 192,700. Gharama nyingine zilikuwa za usafiri, gharama ya dharura na usimamizi, usumbufu wangu binafsi, gharama ya magunia na kadhalika. Mahindi yalipokuwa tayari kwenye magunia, nilifunga safari kwenda mjini kutafuta soko.. Niliposhuka tu niliona gazeti. Habari motomoto siku hiyo ilikuwa: ‘MAHINDI GUNIA 900/= Niligutuka usingizini
Soma habari ifuatayo kisha ujibu maswali 151 – 160:-
Ama kwa hakika, dunia uwanja wa fujo. Vituko vya ulimwengu haviishi. Huzuka kama mizuka kila kunapokucha. Maajabu yaja yakienda. Yote hayo ni mawimbi ya maisha yanayomkumba mwanadamu katika kuishi na kuisha kwake. Lo! Hayo ndiyo malimwengu ulimwenguni.
Nikikaa na kutafakari, huku nikivuta taswira ya mambo kuhusu haya na yale nywele hunisimama, moyo hunidunda, mifupa hunikengeta, nayo damu hunisisimka. Na damu isipowasha hunyeza! Lakini tufanyeje sisi waja wa Mungu ilhali tunajua na kuelewa fika kuwa mja hana hiari na liandikwalo ndilo liwalo? Tunaishi na tuishi kwa rehema na majaliwa ya Jalali. Ewe Mola tunakuhimidi!
Kisa na maana? Hebu nikukumbushe machache tu. Akali ya vituko na vitushi vya hivi karibuni. Bila shaka nitakuwa nimekusaidia na kukufaa ushughulishe kumbukumbu zako nawe urejee nyuma kidogo. Wazee hukumbuka, vijana hukumbushwa.
Si miaka mingi sana ulimwengu wetu ulipokumbwa na mvua za mafuriko ya Elnino. Maafa mangapi kama si misiba iliyotusibu. Baadaye tukakumbwa na uhasama wa Osama! Roho nyonge zikanyongwa. Yakaja mawimbi ya kabobo, nyinyi mnayaita Sunami! Vifo vilifisha wengi. Baada ya kidonda moyoni, msumari wa moto juu ya dondandugu. Kabla ya kupona wakazuka ndugu wawili Artur magariani na mwenzake. Nyinyi mkawaita mamluki. Shangaa. Kesho yatazuka yapi? Tahadhari iko wapi? Roho mikononi. Ndugu amkeni tulale tukiwa macho.
__________________
Soma taarifa ifuatayo kisha uiibu maswali 161- 170
Akiba ni nini? Kwa kifupi, akiba ni kitu kilichotengwa kwa ajili ya manufaa ya baadaye. Watu wanaoamini akiba huwa wanafahamu kuwa maisha yana nyuso mara mbili: wakati wa mavuno mema na wakati wa mavuno hafifu. Wanazaraa hawa wanafahamu fika kuwa kuna uwezekano wa kupata mavuno kama hayo mbeleni. Taifa linalowajali wazalendo wake huhakikisha kuwa maghala yamejaa vyakula nomi. Akiba maarufu zaidi ni ya kuhifadhi pesa benkini.
Watu wengi duniani wamebakia kuwa walalahoi kwa kutojua wala kutambua namna ya kuweka akiba. Utawasikia wengi wakisema kuwa hakiba huwekwa na waja wenye vipato vikubwa. Kabla ya kufikiria hivyo ni vyema ujue kuwa waliokuwa au walionavyo, mwanzoni hawakuwa navyo. Mtu anaweza kuweka akiba hata kama kipato chake ni cha chini kabisa. Kumbuka kuwa hakiba haiozi na kidogo kidogo hujazaa kibaba.
Wengine hulalamika eti hawawezi kuweka akiba kwani mapato yao huishia tu wanapokidhi matakwa yao ya lazima. Hawajui kwamba iwapo wanataka kuwa na uchumi thabiti katika siku za usoni ni sharti kujinyima. Kukosa kuweka akiba eti kwa kusingizia mshahara mdogo ni kujipumbaza tu. Kuna baadhi ya watu vilevile wanaodhani kuwa wao ni wachanga zaidi kuanza kuweka hifadhi. Kuna wanaofanya mipango mizuri zaidi ya kuzitumia pesa zao lakini tamaa na uchu huwafanya tena kupotoka kabisa. Kupanga kufanya jambo na kisha ukakosa kulitekeleza ni kupoteza muda. Utawaona watu wanalipwa mshahara, wanatumia kila kitu na kuendelea kufanya kazi kungojea mshahara mwingine. Huku ni kuzungukia sehemu moja kama tiara bila kupiga hatua.
Ni jambo la busara sana kuanza kuweka akiba kutoka utotoni. Akiba hizi zinaweza kufanywa kwa njia ayami. Mwanzo mtu anaweza kuwa na mkebe mdogo uliotengenezwa kwa njia ya kipekee. Mkebe huo huwa na kishimo kidogo kinachomwezesha mtu kuweka pesa bila kutoa. Njia nyingine ni kuwa wazazi au walezi wao kuwawekea. Wazazi na walezi wanaweza kuwafungulia watoto wao akaunti kwenye benki. Kuweka pesa benkini ni bora zaidi kuliko akiba nyingine zozote. Hii ni kwa sababu ya ulinzi wa pesa pale benkini. Isitoshe, pesa zinazowekwa kwenye benki huzaa riba. Vilevile pesa hizo zinaweza kuwekezwa kwa njia ambazo faida zitaonekana na mtoto mwenyewe. Mtoto anaweza kununuliwa mifugo kama vile; kuku, sungura, mabata ambao watazaana na kumletea mtoto faida zaidi.
Mtoto anapoona kuwa pesa zake zinaweza kuendelea kuzaa huwa na motisha wa kuendelea kuweka akiba. Mwana akilelewa kwa tamaduni hizi za kuwekeza, kamwe hataacha hata akiwa mtu mzima. Atakuwa na mshawasha wa kuendelea kuzalisha milele. Kuweka akiba kutoka utotoni humfanya mtoto kuwa na pesa za kutosha hata kuyaendeleza masomo yake bila kutegemea wafadhili. Huku ndiko kujitegemea. Mtu anayejitegemea huishi maisha ya amani na raha mstarehe.
Je, wewe tayari una akiba au utaanza kuweka leo? Kumbuka kuwa kuweka akiba ni ishara kubwa zaidi ya kuwa na nidhamu.
Soma ufahamu ufuatao kisha ujibu maswali 171-180
Nyanya Matinda alikuwa ametualika twende kumsalimia. Mwanzo aliwauliza wazazi wetu iwapo sote tungepatikana wakati wa sikukuu ya Krismasi. Wengi waliitikia ualishi huo isipokuwa shangazi ambaye aljitetea kuwa binamu yetu Juma angekuwa na shughuli muhimu chuoni. Baada ya majadiliano ya kina na watu wote wa ukoo, uamuzi ulitolewa kuwa twende kumtembelea wakati wa kiburunzi.
Mimi sikuwa nimemwona bibi huyu kwa zaidi ya nusu mwongo. Nilikuwa na mchanganyiko wa furaha na maswali. Furaha kwa kuwa ningepata nafasi ya kuzuru watu wa nyumbani na maswali ya kujua tuliloitiwa. “Je, nyanya anataka kuishia ahera ama vipi? Niliwaza na kuwazua. Nilitaka kuingojea siku hiyo ili nijue dhahiri shahiri. Bibi alikuwa ametayarisha kuchinja ndume wake kuwa kitoweo chetu.
Kufikia saa tisa alasiri tarehe thelathini na moja Desemba, kila mmoja alikuwa amewasili. Mimi ndimi niliyefika karibu wa mwisho. Nilipofika kwa nyanya nilishangazwa na wingi wa watu. Ukweli ni kwamba, singewajua wala kuwatambua wote. Wengi walikuwa ajinabi machoni pangu. Kulikuwa na harufu nzuri ya vyakula hewani. Nilianza kudondokwa na mate bila kujua. Punde si punde, tuliombwa na ami mkuu tuingie ndani sote. Nyumba ya nyanya ilikuwa na bahari ya sebule. Tulimezwa sote na hakukuwa aliyetapikwa hata mmoja. Ilikuwani nyumba ya kisasa iliyojengwa kwa teknolojia mpya.
Pale sebuleni. kila mmoja alionekana akishughulika na simu za mkononi. Wengine walikuwa kwenye mtandao, wengine wakicheza michezo, wengine wakiandika jumbe na wengine wakipiga picha almaarufu ‘selfie”. Mara nyanya Matinda alinyerereka asteaste na kuingia ndani.
Cha ajabu ni kwamba, hakuna aliyemwona isipokuwa mimi. Wote walikuwa na shughuli.
Nyanya alionekana kukasirika. Alitoka shoti na kuingia katika chumba chake cha kulala. Aliporudi alikuwa amebeba gunia. Alikohoa. Kila mmoja aliinua kichwa na kumwangalia. “Hata hamna muda wa kuzungumza mjuane? Simu..simu.simu tu! Kila mmoja aiweke simu yake kwenye gunia hili.” Nyanya alifoka kwa ukali. Tulitii amri ingawa kwa shingo upande.
Sote hatukufurahia lakini tukajibu, “Pole nyanya Matinda kwa kukuudhi'”kwa kauli moja. “Ni kwa nini mmechangamkia elimu ya ulimwengu na huku elimu ya ukoo mmeipoteza? Ni kwa nini hamuwezi kuzungumza mkajuane? Hamjui kwamba dunia imeharibika siku hizi? Hamjawaona ndugu wa damu wakioana kwa kutojua? Ni kwa nini dunia hii inawapotosha wajukuu wangu? Ama nyote mnajuana?” Hapana nyanya,” tulijibu kwa pamoja. “Haya hebu sasa mwangalie mwenzako,” alitoa kauli nyingine.
“Ah! Wajukuu wangu, mmedanganyika na kupotoka kabisa. Hebu tazameni humu mwangu, ni kitu
gani cha kisasa ambacho hakiko? Angalieni runinga yangu na simu yangu. Hivi vyote si vya kisasa? Sasa hebu mniambie iwapo vimenikatiza kujua watu wa ukoo wangu?” Nyanya alisimulia kwa masikitiko.
“Vyombo hivi vyote vya teknolojia ni vyema. Nyinyi ndinyi mnavitumia isivyofaa. Mimi nilipozaliwa
nilipata kuwa kulikuwa na magazeti na televisheni. Baba yangu alikuwa na kijiredio cha mbao ambacho
hakuna hata mmoja aliyeruhusiwa kukigusa.” Tuliangua kicheko. “Acheni kucheka. Hata tulikuwa na
televisheni ya “Sanyo’ ambayo ilionyesha rangi nyeusi na nyeupe.”tulicheka tena. “Isitoshe, kijiji kizima kilifika kwetu wakati wa Magharibi kutazama taarifa ya habari!”
Wakati huo wote tulishindwa kuzuia vicheko. Nyanya pia aliongezea kuwa baba yake alikuwa na saa kubwa sana. Saa hiyo iliyotajwa kuwa ya “Majira’ iikuwa kubwa zaidi kiasi kwamba iliwekwa sakafuni.
Alidokeza kuwa saa hiyo haikutumia betri. Kila mara ungesikia ikitoa sauti kwaa krabu zake, ch!
ch! ch!
Saa ishirini na nne.
Wajukuu wangu, nimemaliza mizungu. Sasa karibuni tule na tufurahie kuwa watu wa ukoo mmoja.” Sinia za minofu zilianza kuletwa mezani.
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 181 mpaka 190.
Mawasiliano ni njia ya kupashana habari kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine. Sijui kama umewahi kuwazia namna watu wa kale walivyotekeleza mchakato huu wa mawasiliano. Kwangu ninaona njia za mawasiliano zilikuwa za ajabu mno. Hebu fikiria kufuka kwa moshi kama ishara ya ujumbe fulani. Je, unafahamu pia milio mbalimbali ilipitisha habari muhimu katika jamii hizo? Kumbuka mbiu ya mgambo wanasema ikilia kuna jambo. Hakika suala la mawasiliano ni nguzo muhimu katika maisha ya binadamu.
Ulimwengu wa sasa umepiga hatua kubwa sana kimaendeleo. Maendeleo hayo yameleta mabadiliko makuu katika mawasiliano. Mfumo wa mawasiliano umewaunganisha waja katika shughuli zao za kila siku. Ilikufanikisha a mawasiliano baina yao, jambo la kimsingi huwa ni kupitisha ujumbe. Wewe mwanafunzi, unapokuwa shuleni kunazo habari muhimu unazohitajika kumfikishia mzazi au mlezi wako. Je, unazifikisha vipi habari hizo?
Fikiria kuhusu wale wanaofanya kazi mbali na familia zao. Unadhani wanawafikishia wapendwa wao taarifa kwa njia gani? Kuna njia nyingi za kuwasilisha ujumbe. Kwa mfano kupiga simu. Vyombo vya habari navyo vinatuwezesha kupitisha ujumbe. Kila siku vinatupasha habari za kila aina. Ni vyema tufahamu kuwa ili mawasiliano yakamilike, basi ujumbe sharti umfikie mlengwa. Mlengwa naye anafaa kuufahamu ujumbe uliokusudiwa.
Tunapopokea ujumbe, tutafakari kuhusu yule aliyetuma ujumbe na ujumbe wenyewe. Sababu kuu ni kubaini lengo kuu la mawasiliano yake. Je, amekusudia nini? Wengi wanaopokea ujumbe wanashindwa kumwelewa aliyetuma ujumbe kutokana na hali ya ujumbe wake. Lugha aliyoitumia inaweza kuwa na utata ambao unatinga kueleweka kwa ujumbe huo. Wengine wanatumia lugha ya mafumbo ambayo labda haieleweki na mlengwa wa ujumbe. Wazia kuwa umemwomba rafiki yako akununulie mbuzi kwa kuwa unahitaji kumfuga nyumbani, kisha ujumbe huu umpige chenga akuletee kifaa cha kukunia nazi.
Je, utamlaumu au utamcheka mpaka mbavu zivunjike? Iwapo tunahitaji kufanikisha mawasiliano, basi ni muhimu tutumie lugha inayoeleweka vyema. Tukumbuke kuwa, katika lugha, maneno huwa na maana mbalimbali katika muktadha.
Hali ya mpokezi wa ujumbe inaweza kuwa kikwazo cha mawasiliano. Huenda anayepokea ujumbe amekumbwa na hali ambazo zinamkosesha utulivu wa kimawazo. Hali hizo zinaweza kuwa matatizo ya kiafya, majukumu ya malezi na kazi miongoni mwa mengine. Hali hii inaweza kutatiza mkondo wake wa mawazo akakosa makini ya kuufahamu ujumbe uliokusudiwa. Mazingira aliyomo mpokezi wa ujumbe huo, huenda pia yakaathiri uelewa wa ujumbe. Chukulia kwa mfano, umetumwa gulioni kununua bidhaa. Kama ilivyo kawaida, maeneo kama hayo huwa na halaiki ya watu na kelele nyingi. Si muziki, si matangazo ya kibiashara, si mahubiri, yataje yote. Ukipigiwa simu wakati kama huo unaweza kukosa kuisikia.
Iwapo utaisikia upokee, mawasiliano yatatizika bila shaka.
Kufanikiwa kwa shughuli nzima ya mawasiliano kunategemea iwapo aliyetuma ujumbe amepokea majibu kwa mujibu wa ujumbe wake. Ni vyema basi tutafakari kuhusu vikwazo vyote ambavyo vinatatiza mawasiliano. Tukumbuke kuwa mawasiliano yetu hutegemea mahusiano yetu, viwango vyetu vya elimu, mila na desturi na chombo cha mawasiliano kinachotumika miongoni mwa mengine. Kila kipengele kitiliwe maanani kwa kuwa ufanisi wa mawasiliano utategemea uelewa wa ujumbe.
Mawasiliano
Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali 191 mpaka 200.
Mimi na Mwamba tulijiunga na shule ya msingi ya Maarifa wakati mmoja. Tangu wakati huo nimemtambua Mwamba kama rafiki wa kuaminika. Tulisoma pamoja, tukacheza pamoja na kushirikiana katika mambo mengi. Alikuwa mmakinifu, msikivu na mchangamfu. Unadhifu wake uliwavutia wengi. Hata mimi aliniathiri nikamuiga. Walimu na wanafunzi walimshabikia na kumthamini hata wakamchagua kuwa kiongozi. Vipawa vya Mwamba vilianza kuchipuka mapema.Naye Mwamba alijitahidi kuvipalilia.
Bidii ya Mwamba inaweza kumithilishwa na ile ya mchwa kujenga kichuguu kwa mate. Mwamba alifahamu fika kuwa mja yeyote kujaliwa ni yeye mwenyewe kujipa uvumilivu, kutia bidii na kushirikiana na wenzake. Alifanya juu chini kuelewa yote tuliyofundishwa na walimu wetu. Ingawa akili yake ilikuwa kama sumaku, pale ambapo alitatizika kuelewa hakufa moyo. Alikuwa tayari wakati wote kujadiliana na wenzake katika vikundi. Alitambua kuwa jifya moja haliinjiki chungu. Pamoja na hayo, Mwamba alijaliwa moyo wa kusaidia. Wakati mwingine katika kundi letu alitufafanulia mada ambazo hatukuzielewa vizuri. Aliwafaa hata wale waliokuwa na changamoto ya kuelewa yaliyofunzwa na walimu. Ama kwa hakika, tulishangazwa na subira na unyenyekevu wake.
Mimi na rafiki yangu Mwamba tulijiunga na timu ya soka ya shule yetu. Alichukua nafasi ya mshambulizi nami nikawa mlinda lango. Kila tuliposhiriki kwenye mashindano, Mwamba aliifungia timu yetu mabao mengi. Mara nyingi, tuliibuka washindi na kuwaacha wapinzani wetu vinywa wazi. Nyota ya Mwamba ilianza kung’aa michezoni. Alipokea tuzo ya mwanasoka bora zaidi katika gatuzi letu. Nayo timu yetu ilinyakua kombe la ushindi na sare kamili za kandanda. Shule yetu ilisifika na kutambulika kama kitovu cha wachezaji kandanda chipukizi. Hata baadhi yetu tulichaguliwa kujiunga na timu ya kitaifa ya vijana.
Mwaka huu, Mwamba amegundua kipawa chake kingine katika rubaa ya muziki baada ya kujiunga na bendi ya muziki shuleni. Wakati wa gwaride na pia sherehe mbalimbali shuleni ameweza kupata nafasi ya kututumbuiza. Sauti yake ya kinanda na nyimbo zake zimevuma kotekote. Kuvuma kwa nyimbo hizo kunatokana na ujumbe wa nyimbo zake. Nyimbo hizo huwahimiza watu kukuza maadili na bidii kila uchao. Hakika, zinatuliza mioyo, zinahimiza, zinachochea watu kuwa na upendo, amani na ushirikiano. Katika siku za hivi majuzi bendi yao imetunga nyimbo ambazo zimevutia wafuasi wengi mitandaoni. Baadhi ya vituo vya mawasiliano vimetuma maombi kualika bendi hiyo kwenye studio zao. Azma yao ni kurekodi baadhi ya nyimbo zao ili zitumike kama milio kwenye simu zinapopigwa au kukiriza. Aidha nyimbo zao huchezwa kwenye vituo mbalimbali vya redio na runinga. Chini ya uongozi wa mwalimu wao, ambaye ni mlezi wa bendi yao, wameweza kujipatia hela ambazo zimetumika kununulia vyombo zaidi vya muziki. Mwalimu huyu wao huhakikisha kuwa bendi hiyo ina nidhamu ya hali ya juu.
Juma lililopita, mwalimu wa zamu aliwapa nafasi wanafunzi kadha kutoa nasaha kuhusu namna ya kufanikiwa masomoni. Mwamba alikuwa miongoni mwao. Hotuba yake ililenga ndipo. Alisema, “Wanafunzi wenzangu, kufaulu kwetu masomoni na pia maishani hakutegemei kule tulikotoka bali nidhamu ya mtu mwenyewe”. Alituambia kuwa achanikaye kwenye mpini hafi njaa. Kwa hivyo, tujitahidi masomoni. Aliongezea kusema kuwa, kila mtu amejaliwa muda wa saa ishirini na nne kila siku. Alituhimiza tuuratibu muda wetu vyema. Katika kuhitimisha hotuba yake alisisitiza tuwaheshimu wakubwa wetu ili tuweze kufanikiwa maishani. Hotuba yake hupigiwa debe shuleni hadi leo.
Ushindi wa timu ya soka ya shule ya Maarifa
Kufaulu masomoni kunategemea:
i.Mwamba kupokea tuzo.
ii.Mwamba kujiunga na bendi ya muziki.
iii.Nyimbo za Mwamba kuvuma. iv.Mwamba kujiunga na timu ya soka.
EXPECTED QUESTIONS IN KCPE 2023
isipungue ukurasa mmoja na nusu. (Alama 40)
hali wali mkavu. (Alama 40)
katika mithihani. (Alama 40)
tukasiskia mayowe kutoka………. (Alama 40)
yangebadilika kabisa. (Alama 40)
(Alama 40) ………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………
PRINT ATLEAST 3 PAGES OF WRITING SPACE FOR EACH COMPOSITION QUESTION.
EXPECTED QUESTIONS IN KCPE 2023
isipungue ukurasa mmoja na nusu. (Alama 40)
hali wali mkavu. (Alama 40)
katika mithihani. (Alama 40)
tukasiskia mayowe kutoka………. (Alama 40)
yangebadilika kabisa. (Alama 40)
(Alama 40) ………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………
PRINT ATLEAST 3 PAGES OF WRITING SPACE FOR EACH COMPOSITION QUESTION.
Get the latest Mwalimu National Sacco BOSA Loans Application Form {Free Download}, here. PDF Latest…
Here is the revised and latest Mwalimu National Sacco FOSA Salary Advance Application Form {Free…
Here is the latest Mwalimu National Sacco FOSA Instant Loan Application Form {Free Download}. Download…
The landscape of digital gambling has shifted toward high-octane mechanics that prioritize volatility and massive…
The Teachers Service Commission (TSC) has advertised 170 job vacancies across, covering senior, mid‑level, and…
Health Cabinet Secretary Aden Duale has ordered immediate changes to the Social Health Authority (SHA)…