• Mon. Jun 24th, 2024

Your Best TSC, Education & General News Website

KISWAHILI LUGHA NOTES FORM 1, 2, 3 & 4

Jun 24, 2024

MATUMIZI YA LUGHA

Kiimbo

 • Jinsi sauti inavyopanda na kushuka mtu anapoongea.
 • Huibua maana halisi ya maneno yanayosemwa kama ifuatavyo:
 • Sentensi za taarifa
 • Mtoto anaandika barua.
 • Sentensi za maswali
 • Mtoto anaandika barua?
 • Sentensi za mshangao
 • Mtoto anaandika barua!
 • Sentensi za amri
 • Kachezeeni nje!
 • Sentensi za rai/ombi
 • Nisaidie/eni.

SEE FREE PDF NOTES HERE; Free Kiswahili notes, revision questions, KCSE past Papers, Exams, Marking Schemes, Topical revision materials, Syllabus and Many more

        Zoezi

 1. Eleza maana ya kiimbo kwa kutoa mifano.
 2. Tambua sentensi zifuatazo ni za aina gani kutokana na kiimbo.
  1. Watu wanakula nyoka?
  2. Watu wanakula nyoka.
 • Watu wanakula nyoka.
 1. Tafadhali nisaidie.

Silabi

 • Tamko moja katika neno/herufi moja au zaidi ambazo hutamkwa pamoja.

        Miundo Miwili ya Silabi za Kiswahili

 • Silabi wazi
 • Huishia kwa irabu k.m. o-a, (I) i-ga (KI), mbu-zi (KKI) na u-ngwa (KKKI)
 • Silabi funge
 • Huishia kwa konsonanti k.m. m-tu (K)

        Zoezi

 1. Ukitoa mifano, fafanua miundo miwili ya silabi za Kiswahili.
 2. Tenganisha silabi katika maneno yafuatayo:
  1. inkisari

Shadda/Mkazo

 • Mkazo unaowekwa kwenye silabi fulani ya neno ikiwa imetamkwa kwa msisitizo.
 • Alama ya ritifaa hutumiwa kutambulisha shadda.
 • Huwekwa kwenye silabi ya pili kutoka ya mwisho, kwenye vitenzi vishirikishi vya silabi moja au kubadilisha maana ya neno.
 • ka’lamu, I’mba, thu’mni, ‘leta, n.k.
 • Kitabu ‘ki mezani.
 • Bara’bara (njia), ba’rabara (sawasawa), wala’kini (lakini), wa’lakini (kasoro/dosari/ila)

Zoezi

 1. Weka shada katika maneno haya:
 2. imba
 3. baba
 4. Onyesha kwa kupiga mstari iliko shada katika maneno yafuatayo:
 5. malaika
 6. nge

Sauti za Kiswahili

 • Kuna makundi mawili ya sauti za kiswahili:
 1. Irabu
 • Sauti ambazo hutamkwa kwa ulaini bila hewa kuzuiliwa katika ala za sauti.
 1. Konsonanti
 • Sauti ambazo wakati wa kutamkwa hewa huzuiliwa katika ala za sauti.
 • Aina za Ala za Sauti
 1. Ala tuli
 • Ambazo hazisogei mtu akitamka k.m. meno, ufizi, kaa kaa gumu, kaa kaa laini na koo/koromeo.
 1. Ala sogezi
 • Ambazo husogea mtu akitamka k.m. midomo na ulimi.

Matamshi/Uainishaji wa Irabu

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 1. a ni ya katikati na chini kinywani na midomo ikiwa imeviringa.
 2. e ni ya mbele na kati kinywani na midomo ikiwa imetandazwa.
 3. i ni ya mbele na juu kinywani na midomo ikiwa imetandazwa.
 4. o ni ya nyuma na kati kinywani na midomo ikiwa imeviringa.
 5. u ni ya nyuma na juu kinywani na midomo ikiwa imeviringa.

        Zoezi

 1. Taja makundi mawili ya sauti za Kiswahili.
 2. Yatofautishe makundi ya sauti za Kiswahili uliyotaja katika (a)
 3. Toa mifano miwili miwili ya irabu ambazo hutamkwa:
 1. midomo ikiwa imeviringa
 2. midomo ikiwa imetandazwa
  1. Eleza jinsi irabu /e/ inavyotamkwa.
  2. Taja aina mbili za ala za kutamkia na utoe mfano mfano mmoja mmoja.

     Matamshi/Uainishaji wa Konsonanti

                        MAHALI

AINA

MIDOMO MDOMO

MENO

MENO UFIZI KAAKAA

GUMU

KAAKAA

LAINI

KOROMEO
VIPASUO            (H)

(GH)

p

b

    t

d

 

 

k

g

 
VIPASUO         (GH)

KWAMIZO          (H)

        ch

j

   
NAZALI            (GH)

(VING’ONG’O)

m     n ny ng’  
VIKWAMIZO      (H)

(VIKWARUZO)(GH)

  f

v

th

dh

s

z

sh gh h
KITAMBAZA       l      
KIMADENDE       r      
NUSU IRABU

VIYEYUSHO

w       y    
 • Huainishwa kulingana na inapotamkiwa, kuwepo au kutokuwepo kwa mtetemeko katika nyuzi za sauti na jinsi hewa inavyozuiliwa katika ala k.m. /p/ ni ya midomo, kipasuo na sighuna.
 • Vipasuo
 • Konsonanti ambazo wakati wa kutamkwa hewa husukumwa, huzuiliwa kabisa na kuachiliwa kwa ghafla na mpasuko mdogo kutokea.
 • Vikwamizo/Vikwaruzo
 • Konsonanti ambazo wakati wa kutamkwa hewa hupitishwa katikati ya ala kwa kukwamizwa.
 • Vipasuo kwamizo/kwaruzo
 • Konsonanti ambayo wakati wa kutamkwa hewa husukumwa nje kwa nguvu, huzuiliwa kabisa halafu mwanya mdogo huachwa hewa ipite kwa kukwamizwa.
 • Nazali/Ving’ong’o
 • Konsonanti ambazo wakati wa kutamkwa kuna kiasi cha hewa huachiliwa na kupitia puani
 • Kitambaza
  • Konsonanti ambayo wakati wa kutamkwa hewa husukumwa kwa nguvu, kuzuiliwa na kuachiliwa ipite kando ya ulimi
 • Kimadende
 • Konsonanti ambayo wakati wa kutamkwa hewa husukumwa, kuzuiliwa na kuachiliwa na kusababisha ncha ya ulimi kupigapiga ufizi mfululizo.
 • Nusu irabu/Viyeyusho
  • Konsonanti ambazo wakati wa kutamkwa hewa hupitishwa katikati ya ala kwa ulaini kama katika utamkaji wa irabu.

        Zoezi

 1. Tambua kikwamizo cha kaakaa laini na kiyeyusho cha midomo.
 2. Tambua konsonanti ambazo si za orodha hii na ueleze kwa nini: /m/, /n/, /ny/,/ng’/, /f/, /b/
 3. Tofautisha konsonanti /p/ na /dh/.
 4. Taja konsonanti mbilimbili ambazo hujulikana kama:
  1. viyeyusho
  2. vikwaruzo

Aina za Maneno

Nomino (N)

 • Neno linalotaja kiumbe, kitu, hali, mahali, tendo, dhana, n.k.

        Aina

 • Nomino za Pekee
 • Ambazo hutaja kitu kwa kutumia jina lake/ambazo hutambulisha upekee wa kitu hicho.
 • Mwanzoni huandikwa kwa herufi kubwa.

 

 • majina ya watu k.m. Kamau
 • mahali k.m. Mombasa
 • siku k.m. Alhamisi
 • miezi k.m. Disemba
 • miaka k.m. 1930
 • milima k.m. Kilimanjaro
 • Mito k.m. Tana
 • maziwa k.m. Victoria
 • bahari k.m. Hindi
 • Mabara k.m. Africa

 

 • Nomono za Kawaida/Jumla
 • Majina ya jumla ya viumbe/vitu vinavyoonyesha umbile la jinsi moja k.m. mtu, gari, kalamu, n.k.
 • Nomino za Jamii
 • Majina ya makundi ya viumbe au vitu k.m. bunge, jamii, halaiki, bunda n.k.
 • Nomino za Wingi
 • Majina ya vitu vitokeavyo kwa wingi japo kimsingi hazina umoja au wingi k.m. maji, mate, maziwa, mahubiri, marashi, mchanga, ngeu, poda, unga, n.k.
 • Nomino za Dhahania
 • Majina ya viumbe au mambo ya kudhani/yasiyoweza kugusika k.m. k.m ujinga, werevu, malaika, shetani, amani, imani, roho, wazo, dhana, n.k.
 • Nomino za Vitenzi Jina
 • Vitenzi vyenye kiambishi awali ku ambavyo huweza pia kutumika kama nomino k.m. Kucheza kwake kunaudhi.

        Zoezi

 1. Sahihisha jedwali lifuatalo
nomino aina
Juma

kisu

maziwa

bunda

amani

kuomba

wingi

dhahania

pekee

kitenzi jina

kawaida/jumla

wingi

 1. Bainisha nomino katika sentensi ifuatayo
  1. Kuendesha baiskeli kwa kasi kulimfanya Hasani aangushe bunda la noti alilokuwa anaenda kununulia mchanga.

Sentensi ya Kiswahili

 • Sentensi ni fungu la maneno linalojitosheleza kimaana linalotumiwa katika mawasiliano.

        Sifa

 1. Huwa na ujumbe uliokamilika.
 2. Huwa na mpangilio maalum wa maneno.
 3. Huwa na muundo wa kiima na kiarifu.

        Aina

 • Sentensi Sahili
  • Sentensi rahisi au nyepesi.

        Sifa

 1. Huwa fupi.
 2. Huwa na kitenzi kimoja pekee.
 3. Huwasilisha dhana moja.
 4. Yaweza kuwa ya neno moja au zaidi.
 5. Yaweza kuwa na kiima kilichododoshwa.
 • Watoto wawili wanaelekea uwanjani.
 • Gachiku ni msichana mtiifu.
  • Sentensi Ambatano
 • Inayoundwa kwa kuunganisha sentensi sahili mbili.

       Sifa

 1. Huwa na vishazi huru viwili.
 2. Huwa na kiunganishi.
 3. Huwa na vitenzi viwili au zaidi.
 4. Hutoa zaidi ya wazo moja.
 5. Yaweza kuwa na viima vilivyododoshwa.
 • Mwanafunzi alipita mtihani ingawa hakuwa anasoma kwa bidii.
 • Maria aliendelea kupika kwa utaratibu huku akiimba wimbo.
  • Sentensi Changamano
 • Ambayo huwa na kishazi tegemezi kilichochopekwa ndani.

        Sifa

 1. Huwa na kishazi tegemezi chenye kitenzi kinachovumisha nomino kwa kuirejelea.
 2. Huwa na kishazi huru kimoja au zaidi.
 3. Huwa na virejeshi (amba na O) au –enye.
 • Tunda alilonunua jana limeoza.
 • Mwizi aliiba pesa zilizokuwa kabatini.

Kundi Nomino (KN) na Kundi Tenzi (KT)

 • Kundi Nomino ni sehemu katika sentensi inayoarifu kuhusu nomino na hutokea mwanzoni mwa sentensi.
 • Kundi tenzi ni sehemu katika sentensi inayoarifu kuhusu kitenzi na hutokea mwishoni mwa sentensi.

Virai

 • Vikundi vya maneno vitumiwavyo na binadamu visivyo na maana kamili.
 • Tungo zinayoundwa kwa maneno aghalabu mawili au zaidi yanayoashiria kitu kimoja na inayojengwa juu ya neno kuu.

 Aina

 

 • Kirai Nomino (Kn)
 • Kirai Kitenzi
 1. T
 2. T+E
 3. T+N
 4. T+N+T
 5. TS+T
 6. t+N
 7. t+V+E
  • Kirai Kivumishi(Kv)
 8. V+E
 9. V+U+V+E
 10. V+V+U+V+E
 11. V+N+V+E
  • Kirai kielezi (Ke)/Chagizo
 12. E
 13. E+E
 14. E+E+E…
  • Kirai Kihusishi (Kh)
 15. H+N
 16. H+N+V
 17. H+N+V+E

 

        Zoezi

       Bainisha virai katika sentensi ifuatayo

 1. Mzazi na watoto wawili werevu sana waliwasili shuleni leo asubuhi kabla ya mwalimu.

Vishazi

 • Kundi la maneno lenye kiima na kiarifu likiwa ndani ya sentensi kuu.

       Aina

 • Vishazi Huru
 • Vifungu vya maneno katika sentensi ambavyo hutoa maana kamili.
 • Vishazi Tegemezi
 • Vifungu vya maneno katika sentensi ambavyo havitoi maana kamili.

Aina

 1. Vishazi tegemezi vya viunganishi k.m. Alimwadhibu ingawa hakuwa na makosa.
 2. Vishazi tegemezi vya virejeshi k.m. Polisi walimpata mtoto aliyekuwa amepotea.
  • Vishazi Viambatani
   • Vinavyoundwa kwa vishazi huru viwili vikiwa vimeunganishwa k.m. Baba analala na mama anapika.

Zoezi

        Bainisha Vishazi Katika Sentensi Zifuatazo

 1. Mwalimu amewasili.
 2. Amina ambaye ni daktari atakuja.
 3. Ametajirika japo hakupata elimu.
 4. Mwalimu anafundisha na wanafunzi wanaandika.
 5. Tumeanzisha shirika ili tunyanyue hali zetu.
 6. Unaweza kuamua kunyamaza au kujitetea.

Shamirisho/Yambwa

Aina

 • Shamirisho Kipozi/Yambwa Tendwa
  • Nomino inayoathiriwa na kitenzi.
 • Shamirisho Kitondo/Yambwa Tendewa
  • Nomino inayotendewa kitendo.
 • Shamirisho Ala/Yambwa Kitumizi
  • Chombo kinatumiwa kufanyia kitendo fulani.

        Mifano

 • Mama alimpikia baba chakula kwa sufuria.
 • Baba alipikiwa chakula na mama kwa sufuria.
 • Sufuria ilitumiwa na mama kumpikia baba chakula.
 1. Chakula (Shamirisho Kipozi/Yambwa Tendwa)
 2. Baba (Shamirisho Kitondo/Yambwa atendewa)
 3. Sufuria (Shamirisho Ala/Yambwa Kitumizi)

Ngeli za Nomino

 • Makundi ya nomino katika lugha ya Kiswahili yenye sifa zinazofanana kisarufi.
  • A-WA
 • Huwa na majina ya watu, vilema, viumbe, vyeo na viumbe vya kiroho, n.k.
 • Huchukua miundo kama vile M-WA, M-MI, KI-VI, n.k.

 

 • mtu-watu,
 • mkulima-wakulima
 • mtume-mitume
 • mkizi-mikizi
 • kiwete-viwete
 • kibyongo-vibyongo
 • nabii-manabii
 • kuku-kuku
 • Waziri-Mawaziri

 

 • U-I
  • Huwa na majina ya mimea, sehemu za mwili, vifaa, matendo, maumbile, n.k.
  • Huchukua muundo wa M-MI.

 

 • Mchungwa-michungwa
 • Mkoko-mikoko
 • mkono-mikono
 • mfupa-mifupa
 • msumari-misumari
 • mgomo-migomo
 • mwendo-myendo
 • msukosuko-misukosuko
 • mlima-milima
 • mwamba-myamba

 

 • U-YA
 • Huwa na majina ya hali, matendo, n.k.
 • Huchukua muundo wa U-MA.

 

 • Ugonjwa-magonjwa
 • upana-mapana
 • uasi-maasi
 • uchungu-machungu
 • ulezi-malezi
 • uovu-maovu
 • uhusiano-mahusiano

 

 • YA-YA
  • Huchukua muundo wa MA-MA.
  • Huwa na nomino zipatikanazo kwa wingi.
  • Hazibadiliki katika umoja na wingi.

 

 • manukato
 • mauti
 • maziwa
 • marashi
 • mahubiri
 • majira
 • maradhi
 • maafa
 • mazingira

 

 • KI-VI
  • Ni majina ya vifaa, sehemu za mwili, vitu, udogo, lugha, n.k.
  • Huchukua miundo KI-VI na CH-VY.

 

 • kisu-visu
 • kitabu-vitabu
 • chakula-vyakula
 • chanda-vyanda
 • kijitu-vijitu
 • kigombe-vigombe
 • kiguu-viguu
 • kidovu-vidovu

 

 • LI-YA
  • Huwa na majina ya sehemu za mwili, dhana, vifaa, ukubwa, n.k.
  • Huchukua muundo wa JI-MA, JI-ME, JA-MA, JE-MA n.k.

 

 • jicho-macho
 • jina-majina
 • jitu-majitu
 • goma-magoma
 • jambo-mambo
 • janga-majanga
 • jembe-majembe
 • jeneza-majeneza
 • wazo-mawazo
 • tunda-matunda
 • jua-majua
 • ziwa-maziwa
 • ua-maua

 

 • I-I
 • Huwa na nomino dhahania na vitu visivyoweza kuhesabika.
 • Hazibadiliki katika umoja na wingi.

 

 • sukari
 • amani
 • chai
 • mvua
 • Imani
 • chumvi
 • subira
 • imani
 • amani
 • furaha

 

 • I-ZI

 

 • Huhusisha nomino dhahania na vitu.
 • Hazibadiliki katika umoja na wingi.

 

 • nyumba

 

 • baiskeli
 • karatasi
 • redio
 • meza
 • dini
 • dawa
 • ndizi
 • jozi

 

 • U-ZI
 • Huchukua miundo W-NY, U-NY, U-F, n.k.

 

 • wayo-nyayo
 • wakati-nyakati
 • uso-nyuso
 • ufa-nyufa
 • ufunguo-funguo
 • ufagio-fagio
 • wembe-nyembe
 • uwanja-nyanja
 • ujumbe-jumbe
 • ukoo-koo
 • waraka-nyaraka
 • waya-nyaya

 

 • U-U
 • Huwa na nomino za dhahania na vitu visivyoweza kuhesabika.
 • Hazibadiliki kimaumbo.

 

 • Huchukua U au W.
 • Ujinga
 • Ulafi
 • Ulaji
 • Werevu
 • Unga
 • Uji
 • Ugali
 • udongo

 

 • KU
 • Nomino zinazoundwa kutokana na vitenzi k.m. kuomba kwake kumemsaidia.
  • PAKUMU
 • Ngeli ya mahali.
 • Huwa na nomino moja ‘mahali’.
 1. PA (mahali karibu au panapodhihirika) k.m. Kitabu kipo pa
 2. KU (mahali mbali au kusikodhihirika) k.m. Mahali kule ku
 3. MU (ndani ya) k.m. Mahali mle mna siafu.

        Zoezi

 1. Tunga sentensi ukitumia nomino kutoka katika ngeli ya U-ZI.
 2. Andika kwa wingi. Makaribisho aliyopewa yalimfurahisha.
 3. Andika katika ukubwa wingi: Paka mweupe amenaswa mguuni.
 4. Andika katika wingi wa hali ya udogo: Mtu aliumwa na mbwa.
 5. Huku ukitoa mifano, fafanua miundo mitatu ya majina katika ngeli ya LI-YA.
 6. Tambua ngeli/viwakilishi ngeli vya nomino zifuatazo:

 

 1. chakula
 2. shairi
 • mtwana

 

Uundaji wa maneno

 • Nomino kutokana na mzizi wa kitenzi
 1. danganya-kudanganya, mdanganyifu,udanganyifu
 2. soma-kusoma, masomo,msomi,usomaji
 3. unda-kuunda, muundaji,uundaji,muundo
 4. funika-kufunika, kifuniko, mfunikaji, ufunikaji
  • Kitenzi kutokana na mzizi wa nomino

 

 1. mlo-kula
 2. mlevi-kulewa, kulevuka
 3. mwimbaji-kuimba
 4. fikra-kufikiri
 5. malezi-kulea
 6. fumbo-kufumba, kufumbua

 

 • Nomino kutokana na mzizi wa nomino

 

 1. mwimbaji-kuimba, wimbo, uimbaji, kiimbo
 2. mchezo-kucheza, uchezaji, mchezaji
 3. ulaghai-kulaghai, mlaghai
 4. hesabu-kuhesabu,uhesabu
 5. mdhalimu- kudhulumu, dhuluma, udhalimu

 

 

 • Nomino kutokana na mzizi wa kivumishi
 1. -refu-mrefu, urefu, urefushaji
 2. -baya-mbaya, ubaya
 3. -zuri-mzuri, uzuri
 4. -kali-mkali, ukali
 5. -eupe-mweupe,weupe
 • Kivumishi kutokana na mzizi wa nomino
 1. ujinga -jinga
 2. werevu -erevu
 3. mzuri -zuri
 4. mpumbavu -pumbavu
 5. mpyoro -pyoro
 • Kitenzi kutokana na mzizi wa kivumishi
 1. haramu-kuharamisha, kuharamika
 2. halali-kuhalalisha, kuhalalika
 3. -fupi-kufupisha, kufupika
 4. bora-kuboresha, kuboreka
 5. -refu-kurefusha, kurefuka
 6. sahihi-kusahihisha, kusahihika
 7. -sikivu-kusikia
 8. -danganyifu-kudanganya
  • Kivumishi kutokana na mzizi wa kitenzi
 9. dunisha – duni
 10. Haramisha – haramu
 11. fupisha -fupi
 12. sahilisha -sahili
 13. tukuka -tukufu
 14. fahamu -fahamivu
 15. teua -teule
 16. nyamaza -nyamavu
 17. ongoka -ongofu
 18. sahihisha -sahihi
 19. danganya -danganyifu
  • Kitenzi kutokana na kielezi
 20. haraka-harakisha
 21. zaidi-zidisha
 22. bidii-bidiisha
 23. hima-himiza

 

        Zoezi

 1. Unda neno ulilopewa katika mabano kutokana na maneno yafuatayo:
 1. zingatia (kivumishi)
 2. sahili (kitenzi)
 • taliki (nomino)
  1. Unda nomino kutokana na mizizi ya maneno yafuatayo kisha utunge sentensi.
 1. -kali
 2. lia

Vitenzi

 • Kitenzi ni neno linaloeleza kuhusu jambo linalofanywa.

Aina za Vitenzi

 • Kitenzi halisi
 • Kinachofahamisha tendo halisi.
 • Hutokea peke yake k.m. Boke anacheza
  • Kitenzi kikuu (T)
 • Kinachoeleza tendo kuu katika sentensi.
 • Hutokea pamoja na kitenzi kisaidizi k.m. Baba anataka kulala.
  • Kitenzi Kisaidizi (Ts)
 • Kinachosaidia kitenzi kikuu

Maneno yanayoweza kutumiwa kama vitenzi visaidizi

 

 • ngali
 • kuwa
 • taka
 • pasa
 • bidi
 • huenda
 • kuja
 • weza
 • kwisha
 • stahili
 • wahi
 • maliza

 

 • Vitenzi Sambamba
 • Vinavyofuatana moja kwa moja/vinavyotokea kwa mfululizo.
 • Hutumika kutoa maelezo kuhusu tendo moja maalum kwa uwazi zaidi.
 • Wachezaji huenda wanaweza kushinda mchezo wa leo.
 • Vitenzi Vishirikishi (t)                                                                                                                                            
 • Vinavyoshirikisha vitu kihali, kitabia au kimazingira.

        Aina

 1. Vitenzi Vishirikishi Vikamilifu
 • Ambavyo huchukua viambishi.
 • Mama alikuwa mgonjwa/jikoni/muuguzi.
 • Aisha angali kitandani/mkaidi/ mwanafunzi.
 1. Vitenzi Vishirikishi Vipunguvu
 • Ambavyo havichukui viambishi
kuyakinisha kukanusha
ni/niko

ndiko

yuko

li/liko

si/siko

siko

hayuko

hali/haliko

Viwakilishi (W) na Vivumishi (V)

 • Viwakilishi ni viambishi au maneno yanayotumiwa badala ya nomino.
 • Vivumishi ni maneno yanayotoa habari zaidi kuhusu nomino.
VIVUMISHI VIWAKILISHI
Viulizi Viulizi
G  Maneno ya kuulizia.

G  Mizizi ni –pi, -ngapi na gani.

ü  Amechukua kitabu kipi?(V. kiulizi)

 

ü  Kipi kimepotea? (W. Kiulizi)

ü  Amenunuliwa mangapi?

ü  Gani imefungwa?

a-unganifu a-unganifu
G  Maneno yanayoundwa kwa viwakilishi ngeli na kiishio a.

G  Hutoa maana ya umilikaji

ü  Mtoto wa shangazi amelala. (V. a-unganifu)

ü  Wa Juma analia. (W. a-unganifu)

ü  Cha mlevi huliwa na mgema.

Vimilikishi Vimilikishi
G  Hutoa maana ya umilikaji.

Mizizi

nafsi kuyakinisha kukanusha
1

2

3

-angu

-ako

-ake

-etu

-enu

-ao

ü  Kiatu changu kimepotea. (V. kimilikishi).

ü  Usichukue chake. (W. kimilikishi)
Sifa Sifa
G  Maneno ya kusifu au kueleza jinsi nomino ilivyo k.m. -fupi, -baya, -kali, -dogo, n.k.

ü  Mti mrefu umeanguka. (V. sifa)

ü  Alichukua cheupe. (W. Sifa)
Vionyeshi/viashiria Vionyeshi/viashiria
G  Maneno ya kuonyesha nomino ilipo.

G  Huwa za karibu, wastani na mbali k.m. hili, hilo, lile.

ü  Kiatu hiki kimechafuka. (V. kionyeshi/kiashiria)

Hii ni ya nani? (W. kionyeshi/kiashiria)
Viashiria visisitizi Viashiria visisitizi
G  Maneno ya kutilia mkazo nomino yakizingatia ilipo.

G  Huwa ya karibu, wastani na mbali.

G  Huundwa kwa kutumia kiwakilishi ngeli katika kionyeshi cha kwanza k.m. kiki hiki-vivi-hivi, lili hili-yaya haya, n.k.

ü  Chumvi ii hii ilimwagika. (V. kisisitizi)

ü  Kuku huku ndiko kulinyesha. (W. kisisitizi)
Virejeshi Virejeshi
G  Hurejelea nomino au kukumbusha kuihusu.

G  Huwa amba- na -o- rejeshi.

ü  Mtoto ambaye analala ni wake.

ü  Watoto wanaolala ni wao. (V. kirejeshi)

ü  Mnyama ambaye huwindwa ni nguruwe.

ü  Mnyama awindwaye ni nguruwe.

ü  Ambaye aliniibia ninamjua.

ü  Aliyeniibia ninamjua.

ü  Ambaye hula nyasi ni ng’ombe.

ü  Alaye nyasi ni ng’ombe.

 

Idadi idadi
G  Hutaja idadi ya nomino

Aina

a)      Idadi halisi (iliyo dhahiri) k.m. -moja, sita, n.k.

b)     Idadi ya jumla (isiyo dhahiri) k.m. -chache, -kadha –ingi, n.k.

ü  Mwalimu mmoja na wanafunzi sita wameenda. (V-idadi halisi)

ü  Vitabu vichache vimechukuliwa na watoto kadha. (V. idadi ya jumla)

ü  Nipe kumi na kimoja. (V. idadi halisi).

ü  Amechukua machache tu. (V. idadi ya jumla)

 

Pekee Pekee
G  Hutoa taarifa zaidi kuhusu nomino kwa njia ya pekee.

a)      –enye (umilikaji)

ü  Msichana mwenye maringo ni yule. (V. Pekee)

b)     –enyewe (halisi au kusisitiza)

ü  Barua yenyewe niliipeleka posta.

c)      –ote (bila kubakisha)

ü  Chakula chote kimeliwa.

d)     -o-ote (bila kubagua)

Mtu yeyote anaweza kuugua.

e)      -ingine (sehemu ya baadhi ya vitu)

ü  Mikufu mingine imeibwa.

f)      -ingine-o (mbali na/zaidi ya)

ü  Nyuzi nyinginezo zilikatika.

ü  Mwenye macho haambiwi tazama. (W.pekee)

ü  Yenyewe yaliiva jana.

ü  Kiliharibika chote.

ü  Popote paliposafishwa pamechafuka.

ü  Ametorokea kwingine.

ü  Nyingineyo niliweka katika chakula.

Nomino/majina W
Þ    Nomino/majina ambayo hutumika kama vivumishi

ü  Mtu mzee hutembea kwa mkongojo. (V. jina/nomino)

 

 

W Ngeli
 

 

Viwakilishi ngeli ambavyo huwakilisha nomino k.m. Liliiva jana-Yaliiva jana.
W Nafsi
  Þ    Maneno au viambishi vinavyotajia nafsi.

Aina

a)     Nafsi huru

Þ    Maneno ya kutajia nafsi.

nafsi umoja wingi
1

2

3

Mimi

Wewe

yeye

Sisi

Nyinyi

wao

ü  Yeye ni mtiifu. (W. nafsi huru)

b)         Nafsi tegemezi/viambata

Þ    Viambishi ambavyo hutaja nafsi.

nafsi umoja wingi
1

2

3

ni

u

a

tu

m

wa

ü  Walisahau kumwambia. (W. nafsi tegemezi)

 

Vielezi (E)

 • Viambishi au maneno yanayoeleza zaidi kuhusu kivumishi, kitenzi au kielezi kingine.
 • Yeye ni mweupe sana/ajabu/kwelikweli/kupindukia/pepepe.
 • Alikula pole pole sana.

       Aina

 1. Vielezi vya Namna/Jinsi
 • Ambavyo hueleza vile jambo lilifanyika.

Aina

 • Vielezi namna mfanano
 • Vinavyoeleza vile jambo lilifanyika kwa kufananisha na nomino au vivumishi.
 • Huchukua viambishi KI na VI.
  • Anakula ki
  • Tulifanya kazi vi
 • Vielezi namna viigizi
  • Maneno ambayo kiasili ni vielezi k.m. sana, haraka, ghafla, mno, kabisa, pole, barabara n.k.
   • Mwenda pole
  • Vielezi namna hali
   • Hueleza hali ya tendo.
  • Alilelewa kwa shida.
  • Alilewa chakari
 • Vielezi namna vikariri
  • Huelezea vile jambo lilifanyika kwa kurudiwarudiwa
 • Alinijibu
 • Tembea
 • Yeye hufanya kazi yake hivi hivi/ovyo ovyo
 • Mbwa alibweka bwe! Bwe! Bwe!
 • Vielezi namna ala
 • Walimpiga Stephano mawe/kwa mawe.
 • Vielezi Namna Viigizi
  • Hueleza vile kitendo kilitendeka kwa kutumia tanakali.
 • Mbuni alianguka majini chubwi!
 1. Vielezi vya Idadi/Kiasi
  • Maneno ambayo hutaja kitendo kimetendeka mara ngapi.

Aina

 • Vielezi vya idadi halisi
 • Tulivamiwa mara moja.
 • Vielezi vya idadi ya jumla
 • Alitoroka mara kadha/nyingi/chache.
 1. Vielezi vya mahali
  • Hutaja mahali kitendo kilitendekea.

Aina

 • Vielezi vya mahali vya maneno kamili
 • Ndege ilipofika Nairobi, ilitua chini.
 • Vielezi vya mahali vya aina ya viambishi
  • Ni viambishi po, ko, mo na ni.
 • Alipolala palikuwa na siafu.
 • Wanacheza uwanja
 1. Vielezi vya wakati
  • Hutaja kitendo kililifanyika wakati gani.

Aina                                                                                                                  

 • Vielezi vya wakati vya maneno kamili
 • Rais atawasili kesho/mwaka ujao.
 • Kielezi cha wakati cha kiambishi (po ya wakati)
 • Nililala nilipofika nyumbani

     Viunganishi (U)

 • Neno au fungu la maneno la kuunganishia.

Aina

 

 • Vya kujumuisha pamoja
 • na
 • aidha (pia)
 • isitoshe
 • kadhalika (pia))
 • tena
 • mbali na
 • fauka ya (zaidi ya)
 • Vya kukatiza ili kupambanua
 • walakini (lakini)
 • bali (lakini)
 • ijapokuwa (hata kama)
 • ingawa (hata kama)
 • Vya kuonyesha kinyume cha mambo
  • ilhali
  • licha ya
 • Kuonyesha masharti
 • budi (lazima)
 • lazima
 • sharti
 • ikiwa (kama)
 • bidi
 • Vya sababu
 • kwa
 • kwa sababu
 • maadamu (kwa kuwa)
 • madhali (kwa kuwa)
 • kwa vile/maana
 • kwa ajili/minajili ya
 • mintaarafu (kutokana na)
 • Vya kuonyesha Chaguo
 • au
 • ama
 • wala
 • Viunganishi vingine na maana zake
 • ila (isipokuwa)
 • laiti (kama)
 • lau (kama)
 • mradi (bora)
 • angalau (bora zaidi)
 • bighairi (bila ya kujali) k.m.Minghairi vitu vilivyo kwenye kabati vinginevyo unaweza kuvichukua.
 • seuze/sembuse (kulinganisha ili kuonyesha tofauti)
 • labda (pengine)

 

Vihusishi (H)

 • Maneno yanayoonyesha uhusiano.

Aina

 

 • Mahali
 • juu ya, miongoni mwa, katika, mpaka, hadi
  • Wakati
 • kabla ya, baada ya, tangu, hadi, mpaka
  • Sababu
 • kwa, kwani, kwa sababu, mintaarafu ya
  • Ala
 • Alimkata kwa
  • A-unganifu
 • Simu ya rununu inalia.
 • Jumba la mikutano limeandaliwa.
 • Kiatu cha ngozi hudumu.
 • Kikome cha plastiki ni duni.
  • Ulinganisho
 • Zaidi ya, kuliko, kuzidi, kushinda.
  • Kiwango
 • Zaidi ya, kati ya, takriban, karibu
  • Vya hali
 • Mithili ya, kwa niaba ya

 

Vihisishi (I)

 • Maneno yanayotoa hisia za moyoni.

 

 1. furaha
 • Hoyee! Haleluya! Alhamdulilahi!
 1. hasira
 • Kefle! Ah! He!
 1. majuto
 • Kumbe! Jamani! Ole wangu! Laiti
 1. huzuni/huruma
 • Pole! Ole! Maskini!
 1. kuitikia
 • Bee! Labela! Naam! Ehee! Ahaa!
 1. mshangao/mshtuko
 • Eti! Salaale! Ajabu! Msalia mtume! Lahaula!
 1. kubeza
 • Mawe! Ngo! Mmm! Mwangalie!
 1. kusisitiza
 • Hata
 1. kutakia heri
 • inshallah

 

Mwingiliano wa Maneno

 • Hali ya maneno kuwa na matumizi tofauti mifano:

 

 • W kuwa V
 • Huyu
 • Mtoto huyu
  • V kuwa W
 • Vikombe vizuri vitavunjika.
 • Vizuri
  • V kuwa N
 • Mti mrefu
 • Mrefu alikufa jana jioni.
  • V kuwa E
   • Viatu vibaya
   • Uliifanya kazi
   • Mtu mjinga ni huyu.
   • Anaongea
  • N kuwa V
 • Tajiri alimdharau Razaro.
 • Mtu tajiri
  • N kuwa E
 • Nairobi ni mji mkuu.
 • Amewasili
 • Kitoto
 • Unaongea
 • Haraka haina baraka.
 • Fanya haraka tuondoke hapa.
 • Sindano ya babu imepotea
 • Alidungwa sindano/kwa sindano na daktari.
  • E kuwa N
 • Niliwasili jana.
 • Jana yangu haikuwa nzuri.
  • T kuwa N
 • Nataka kulala
 • Kulala kwake kunaudhi.
  • N kuwa U
 • Ila yake imemwathiri sana.
 • Watu wote ila yeye walikwenda.
 • Kichwa changu kina walakini.
 • Nimekula walakini
  • E kuwa I
 • Mwenda pole
 • Pole! Usijali utapona.
 • Amepaka rangi sawasawa.
 • Sawasawa! Siku moja tutakutana.
  • H kuwa E
 • Paka amepanda juu ya mti.
 • Ameingia katika choo.
  • T kuwa E
 • Mtoto akilia
 • Aliingia akilia.
  • N kuwa I
 • Gege anacheza ala yake ya muziki.
 • Ala! Waniwekea uchafu katika chakula?

 

Mofimu

 • Kipashio kidogo zaidi katika lugha kisichoweza kuvunjwavunjwa zaidi bila kupoteza maana yake.

Aina

 • Mofimu huru
 • Neno lisiloweza kugawanywa katika vipande mbalimbali na linalojisimamia na kuwa na maana kamili.
 • Kuku, baba, mama, sana, labda, jana n.k.
 • Mofimu tegemezi
 • Isiyoweza kujisimamia na kujitosheleza kisarufi, mifano:

 

 • Mzizi (Sehemu ya neno inayobeba maana kuu na isiyoweza kubadilishwa)
 • mtu, samahe-k-a, n.k.
 • Nafsi
 • Tumesahau
 • Ngeli
 • Li
 • Ya
 • Kikanushi
 • Sikumpiga
 • Ha
 • Hu
  • Njeo/wakati
  • Lili
  • Ana
  • Tuta
  • Alipo
  • Hali
 • Me, nge, ngali, hu, ki, ka, n.k.     
  • Mahali
 • Alipo
 • Aliko
 • Alimo
  • Virejeshi
   • Lililo
   • Aliji
  • Mtendwa/watendwa/kitendwa/vitendwa/shamirisho
 • Alichiki
 • Kilichowa
  • Mnyambuliko/kauli
 • Alimpigi
 • Alimlilia
 • Alinikose
 • Alimtole
  • Kiishio
 • a, e, i, u

 

Viambishi

 • Viungo vyenye maana vinavyofungamanishwa na mziziwa neno ili kulipa maana mbalimbali.

 

       Aina

 • Viambishi Awali
 • Ambavyo hutokea kabla ya mzizi.
 • A-li-ye-ku-kata-a
  • Viambishi Tamati
 • Ambavyo hutokea baada ya mzizi k.m. ki-pig-ishw-a-cho

Mnyambuliko wa Vitenzi

 • Kunyambua kitenzi ni kukiongeza viambishi tamati ili kukipa maana tofauti.

Aina za minyambuliko/kauli za vitenzi

 • Kutenda
  • Hali ya kawaida ya kitenzi.
 • Kutendatenda
  • Hali ya kitenzi kurudiwa.
 • Kutendea
  • Kwa niaba ya
  • Badala ya
  • Sababu
  • Kuonyesha kitumizi
  • Mwendo wa kitu kuelekea kingine
 • Kutendwa
 • Huonyesha nomino iliyoathiriwa na kitenzi.
  • Kutendewa
 • Humaanisha kitendo kimetendwa na mtu badala au kwa niaba ya mtu mwingine.
  • Kutendana
   • Unamtenda mtu jambo naye anakutenda jambo lilo hilo.
  • Kutendeana
 • Unamtendea mtu jambo naye anakutendea jambo lilo hilo.
  • Kutendeka
   • Uwezekano wa kitendo kufanyika
  • Kutendesha
   • Mtu au kitu kusababisha kufanyika kwa kitendo.
  • Kutendeshea
 • Kusababisha kitendo kitendeke kwa niaba ya mwingine.
  • Kutendeshwa
 • Kusababishwa kufanya jambo.
  • Kutendeshewa
 • Mtu kusababishwa kitendo kitendeke kwa niaba yake.
  • Kutendeshana
 • Kusababisha kitendo kitendeke kwa mtu naye anasababisha kitendo kicho hicho kitendeke kwako.
  • Kutendesheana
 • Kusababisha kitendo kitendeke kwa niaba ya mtu naye anasababisha kitendo kicho hicho kitendeke kwa niaba yako.
  • Kutendesheka
 • Kitendo fulani kinaweza kusaababishwa.
  • Kutendama
 • Kuwa katika hali fulani bila ya mabadiliko.

 

 • lala-lalama
 • ficha-fichama
 • shika-shikama
 • ganda-gandama
 • chuta-chutama
 • funga-fungama
 • kwaa-kwama
 • unga-ungama
 • andaa-andama
 • saki-sakama

 

 • Kutendata
  • Hali ya mgusano au kushikanisha vitu viwili.

 

 • paka-pakata
 • fumba-fumbata
 • kokoa-kokota
 • okoa-okota
 • kama-kamata

 

 • Kutendua
  • Hali ya kiyume

 

 • choma-chomoa
 • funga-fungua
  • Kutenduka
   • Kuweza kufanyika kwa hali ya kinyume.

 

 • chomoka
 • funguka

 

Vinyume vya vitenzi

 

 • komea-komoa
 • bariki-laani
 • patana-kosana
 • angika-angua
 • mwaga-zoa
 • ziba-zibua
 • tatiza-tatua
 • funika-funua
 • tega-tegua
 • tawanya-kusanya
 • ugua-pona
 • nasa-nasua
 • kwamiza-kwamua
 • kosa-kosoa
 • pakia-pakua
 • twika-tua
 • paa-tua
 • cheka-lia
 • anika-anua
 • simama-keti
 • fukia-fukua
 • inama-inuka
 • funga-fungua
 • furahi-huzunika
 • kumbuka-sahau
 • oa-taliki
 • choka-pumzika
 • uliza- jibu
 • jenga-bomoa
 • ishi-kufa/hama
 • kufa-kufufuka/ishi
 • lewa-levuka
 • anza-maliza/isha
 • saza/bakiza-maliza
 • meza-tapika/tema
 • ingia-toka
 • dharau-heshimu
 • kweya-teremka
 • panda-shuka
 • sifu-kashifu
 • chimba-fukia
 • chafua-safisha
 • cheka-lia
 • panda-shuka
 • babaika-tulia
 • pokea-aga
 • zama-elea
 • vaa-vua

 

kitenzi tendea tendwa tendewa tendana tendeka tendeana tendesha tendeshea tendesheka
cha

ü  ogopa

chia chwa chiwa chiana chika chiana chisha chishia chishika
cha

ü  pambazuka

chea 0 chewa 0 0 0 chesha cheshea chesheka
chwa

ü  jua kuanza kutua

chwea 0 chwewa chweka 0 0 chwesha chweshea chwesheka
fa

ü  tokwa na uhai

fia 0 fiwa fika 0 fiana fisha fishia fishika
gwa

ü  anguka

gwia 0 gwiwa 0 0 gwiana gwisha gwishia gwishika
ja

ü  sogea karibu

jia 0 jiwa jika 0 jiana jisha jishia jishika
la

ü  tia chakula kinywani na kumeza

lia liwa liwa lika lana liana lisha lishia lishika
nya

ü  enda haja kubwa

ü  anguka matone

nyea nyewa nyewa nyeka 0 nyeana nyesha nyeshea nyesheka
nywa

ü  tia kitu majimaji kinywani na kukimeza

nywea nywewa nywewa nyweka 0 nyweana nywesha nyweshea nywesheka
pa

ü  kabidhi

pea 0 pewa peka pana peana pesha peshea pesheka
pwa

ü  maji toka ufuoni hadi mbali ya bahari

pwea 0 pwewa pweka 0 0 pwesha pweshea pwesheka
ta

ü  taga

tia o tiwa tika 0 0 tisha tishia tishika
wa

ü  tokea

wia 0 wiwa wika wana wiana wisha wishia wishika

Matumizi ya Maneno na Viambishi Maalum

Maneno Maalum

 

 • ila
 1. isipokuwa
 • Watu wote ila yeye wameenda.
 1. kasoro
 • Hakuna kizuri kisicho na ila.
  • labda (pengine/shaka)
 • Haonekani siku hizi labda amepata uhamisho.
  • ikiwa
 1. (kama/shaka)
 • Tutamkuta nyumbani ikiwa amepewa likizo.
 1. masharti
 • Mgonjwa atapona ikiwa atakunywa dawa ipasavyo.
  • walakini
   1. dosari
  • Ghorofa limebomolewa kwa sababu lilikuwa na walakini.
   1. lakini/bali
  • Nimekula walakini
   • ingawa/ingawaje (hata kama)
  • Nilijilaza kitandani ingawa sikuwa na usingizi.
   • ijapokuwa/japo (hata kama)
  • Usicheze na nyoka ijapokuwa ni mdogo.
   • jinsi
    1. njia/utaratibu wa kufanyia jambo
   • Sijui jinsi ugali unavyopikwa.
    1. aina/namna/sampuli
   • Siwezi kula chakula jinsi
    1. kulingana na/kama
   • Alikuja jinsi
    • kwa
 1. mahali
  • Ameenda kwa
 2. jinsi
 • Alisoma kwa
 1. sehemu ya kitu kisima/akisami
 • Amepata alama moja kwa tano katika mtihani.
 1. pamoja na
 • Harusi ilihudhuliwa na wazee kwa vijana na tulikula wali kwa
 1. kuonyesha kitu kilitumiwa kama kifaa
 • Alikata mkate kwa
 1. sababu
 • Aliugua kwa kunywa maji machafu.
 1. kuunganisha vipashio viwili
 • Leo ndiwe utapika kwa hivyo tayarisha viazi.
 1. muda/kipindi
 • Alilia kwa nusu sana.
 1. kufanya jambo bila kupoteza wakati
 • Baada ya kula, tulienda moja kwa moja kulala.
 1. kivumishi cha a-unganifu cha ngeli ya KU
 • Kucheka kwa Maria kunaudhi.
 1. umiliki wa mahali
 • Twende nyumbani kwangu.
  • na
 1. kiunganishi
 • Mama na baba wanalima.
 1. umilikaji
 • Kamau ana kitabu kizuri.
 1. wakati uliopo
 • Anaandika barua.
 1. kauli/mnyambuliko
 • Kamau na Juma wanapigana.
 1. kuonyesha tofauti
 • Kiatu hiki ni tofauti na
 1. mtenzi
 • Alipigwa na
 1. kuonyesha ufupisho wa nafsi
 • Alisaidiwa nao.

 

 Zoezi

 1. Eleza matumizi ya na katika sentensi zifuatazo:
  1. Baba na mama wanapigana kwani ana tabia ya kulewa.
  2. Mtoto aliteswa na mama yake kwa kuwa tofauti na wengine nami kikamkanya.
   • wala (kukanusha)
 • Sikumtusi wala

Viambishi Maalum

 

 • me/ja (hali timilifu/kitendo kutendeka na si muda mrefu uliopia)
 • Mama ame
 • Mama haja
 • hu
  1. mazoea/jambo hutokea kila wakati
 • Yeye hulala mapema.
  1. kikanushi
 • Hukutibiwa vizuri.
 • li
  1. wakati uliopita
 • Alitupatia zawadi.
  1. ngeli
 • Tunda li
  1. kitenzi kishirikishi kipungufu
 • Jembe li
 • ni
  1. nafsi ya kwanza umoja
 • Niliwasili jana.
  1. mahali
 • Twende kanisani.
  1. kitenzi kishirikishi kipungufu
 • Yeye ni
  1. wingi
 • Tokeni
 • ndi- (kitenzi kishirikishi kipungufu)
 • Yeye ndiye aliniibia pesa.
 • ji
  1. udogo
 • Kijitu kimeanguka.
  1. ukubwa
 • Jibwa limebweka.
  1. kirejeshi
 • Alijipalia makaa.
  1. nafsi ya pili
 • Jichukulie upendacho.
  1. kiambishi tamati cha kuunda nomino.
 • Mwimbaji
 • Ki
  1. kitendo ki katika hali ya kuendelea
 • Tulikuwa tukila alipoingia.
  1. masharti/kitendo kinategemea kingine
 • Utapita mtihani uki
  1. udogo
 • Kitoto kinalia.
  1. ngeli
 • Kitabu ki
  1. kitenzi kishirikishi kipungufu
 • chakula ki
  1. kielezi namna mfanano.
 • Yeye hula ki
  1. kitendo hakifanyiki kamwe
 • Chai hii hainyweki.
 • ku
  1. kikanushi cha wakati uliopita
 • Hakumpiga kwa jiwe.
  1. nafsi ya pili umoja.
 • Alikupigia simu jana.
  1. mahali
 • Huku ku
  1. ngeli
 • Kuugua ku
  1. mwanzo wa kitenzi
 • Ameenda kusafisha nyumba.
 • ka
  1. mfuatano wa matukio
 • Tulikula chakula, tukanywa chai kisha tuka
  1. vichwa vya habari
 • Mwizi kapigwa mawe
  1. kutoa amri
 • Kachezeeni nje!
  1. kitendo fulani ni tokeo la kingine
 • Tulisoma kwa bidii tukapita mtihani.
  1. kutoa nasaha/shauri
 • Kamwombe babako msamaha.
 • a
  1. Hali isiyodhihirika ya wakati uliopo
 • Watoto wacheza uwanjani.
  1. vichwa vya habari
 • Waziri aaibishwa na wananchi.
  1. kitendo kinaendelea
 • Twaenda sokoni.
  1. nafsi ya tatu umoja
 • Yeye aliudhika sana.
  1. ngeli
 • Mbuzi yule atachinjwa kesho.
  1. kiishio
 • Mtoto amekula
 • nge/ngali (masharti yanayowezekana au yasiyowezekana)
 • Ningekuwa na pesa, ningenunua kiatu.
 • Laiti ningalijua nisingaliingia katika hilo basi.
 • po
  1. wakati
 1. maalum
 • Yeye anapolala hukoroma.
 1. Wowote/mazoea
 • Mwalimu aingiapo wanafunzi husimama.
  1. mahali
 • Paliposafishwa pamechafuka.
  1. masharti
 • Mtoto aamkapo, mpe uji.
  1. kikanushi cha ki ya masharti
 • -asipokula.

 

Viakifishi

 

 • Alama za usemi(“”)
 1. Usemi halisi
 • “Njoo kesho,” mama akamwambia.
 1. Lugha ngeni
 • “Ninunulie jarida la ‘Parents’”, babake akamwambia.
 1. Vipindi, filamu, makala
 • “Vioja Mahakamani”
 1. Semi
 • “kumwaga zigo”
 • Dukuduku (…)
 1. maneno yameachwa ya kutangulia, kati au ya mwisho. Yaweza kuachwa kwa kuwa makali
 • Nyani haoni…
 1. kukatizwa usemi/kauli

AMINA: Mama ni…

MAMA: Kwanza watoka wapi usiku huu?

 1. maneno yanaendelea
 • Alimwambia ajihadhari anapovuka barabara…
 • Koma/mkato/kipumuo( , )
 1. pumziko fupi katika senyensi
 • Tulipofika sokoni, tulinunua mboga.
 1. kuorodhesha
 • Alinunua mboga, samaki, nyanya na viazi.
 1. kuonyesha mwanzo au mwisho wa usemi halisi
 • “Njoo kesho,”mama akamwambia.
 1. kuandika anwani
 • Shule ya upili Gatwe, S.L.P 160, Kerugoya.
 1. baada ya kutaja jina la mtu anayepewa habari
 • Daktari, ningependa kukuona.
 1. kutenganisha sentensi zenye masharti
 • Usipofanya kazi, usile.
 1. kuandika tarehe
 • Alizaliwa mwezi wa Julai, tarehe 18, 1999.
 1. kuandika tarakimu zinazozidi elfu
 • 1,000, 13,000, n.k.
  • Ritifaa/kibainishi( ’ )
 1. herufi imeachwa
 • wal’otutuma
 1. shadda/mkazo
 • `iba, ka`lamu
 1. katika sauti ya king’ong’o
 • Ng`ombe amekufa.
 1. Kufupisha
 • Tu’shasafisha nguo.
 1. katika kuandika miaka yenye namba izilizoachwa
 • `73-`99.
  • Mshazari/mkwaju(/)
 1. Tarehe
 • Alizaliwa tarehe 5/6/1998.
 1. kuonyesha kumbukumbu
 • KUMB 1/2009
 1. kuonyesha visawe
 • Nenda katika shule/skuli.
 1. Kuonyesha au
 • Wanawake/wanaume wataajiriwa.
  • Kistari kifupi( – )
 1. kuandika tarehe
 • 5/6/2006
 1. kuonyesha silabi, viambishi au mofimu
 • sa-la-mu na imb-a.
 1. kuonyesha neno linaendelea katika mstari unaofuata.
 • Usitenganishe sauti za silabi.
 1. Kuonyesha mzizi wa neno
 • -ma,-bwa
 1. kuonyesha kudumishwa kwa sauti
 • Lo-o-o-o!
 1. Hadi/ kipindi cha tukio fulani
 • 1999-2008.
 1. Kutenganisha usemi na msemaji
 • Huo ni upumbavu-Kibaki
  • Kistari kirefu( )
 1. kutenganisha usemi na msemaji
 2. kuonyesha mabadiliko ya ghafla
 • Wanafaunzi ni wajinga-samahani, simaanishi wote.
 1. kutangulia maelezo ya ziada
 • Walisaidia nchi za Afrika Mashariki- Kenya, Uganda na Tanzania kwa msaada
  • Mstari(­­ )
 1. kusisitiza
 • Jibu maswali mawili
 1. kuonyesha aina za maneno
 • Mtoto wangu analala (V. kimilikishi).
 1. kuonyesha vitabu, majarida na magazeti
 • Chemchemi za Kiswahili, “True Love”, n.k.
 1. kuandika anwani/kichwa
 • Mwanafunzi Adhibiwa/Kaadhibiwa Vikali
  • Kikomo/kitone/nukta (.)
 1. mwishoni mwa sentensi.
 2. kuandika tarehe
 • 3.2013
 1. kuonyesha ufupisho wa maneno
 • ,Bw.,Bi.,C.C.M
 1. kuonyesha takwimu
 • 5, 86.27, n.k.
 1. kutenga shilingi na senti
 • 50-shilingi sita na senti hamsini
 1. juu ya herufi j na I
  • Nusu/semi koloni/nukta na kituo (:)
 2. kugawa sentensi mbili zinazoweza kujisimamia bila ya viunganishi
 • Wasichana walifuata maagizo waliyopewa; wafulana waliyagomea.
 1. kama kipumziko katika sentensi ndefu
 • Alipochunguza ile hati aliyokabidhiwa na wale wafanya biashara aliona kuwa si nzuri; akaamua kujitenga nayo.
  • Vifungo/mabano/paradesi( )
 1. kuzingira nambari au herufi katika orodha
 • (i),(a)
 1. kuonyesha maelezo ya vitendo vya msemaji katika mazungumzo, mahojiano au tamthilia
 • MAMA 🙁 ) Hebu njoo haraka.
 1. kutoa maelezo zaidi
 • Ema (kifungua mimba changu) chaja leo kutoka marekani.
 1. kuonyesha visawe
 • Mamba (ngwena) huliwa.
  • Herufi kubwa(H)
 1. mwanzoni mwa sentensi.
 2. kuandika anwani
 • L.P 1000, Bura.
 1. mwanzoni mwa usemi halisi
 • “Twendeni zetu,” akatwambia.
 1. baada ya kiulizi (?) na hisi (!)
 • Lo! Ulienda? Hebu niambie yaliyojiri.
 1. mwanzoni mwa nomino za pekee
 • Musa
 1. ufupisho wa maneno
 • C.M (Chama cha Mapinduzi)
 1. mwanzoni mwa majina ya vitabu, majarida, magazeti, vipindi, filamu, n.k.
 2. kuandika sifa inayotokana na jina la pekee
 • Kiganda, Kikristu.
  • Koloni/ Nukta mbili ( : )
 1. kuorodhesha
 • Ukitaka kuandaa samosa, unahitaji vitu hivi: unga, nyama, chumvi, mafuta na kitunguu
 1. kutangulia usemi halisi
 • Alimwangalia kisha akamtupia: “mshenzi.”
 1. kuandika mazungumo, mahojiano au tamthilia
 • MAMA 🙁 Akiinuka.) Umechelewa wapi?
 1. kutenganisha dakika na sekunde
 • 25:05
 1. kutangulia maelezo fulani
 • Alipofungua mlango alishtuka: mizoga ya punda ilikuwa imetapakaa nje.
  • Hisi/mshangao (!)
 1. kuamrisha
 • Kachezeeni nje!
 • Kamau! Unafanya nini?
 1. baada ya vihisishi
 • Masalaale! Pesa zangu zote zimeibwa.
 1. baada ya sentensi iliyo mshangao
 • Gari langu limeibwa!
 1. kusisitiza
 • Kesho msichelewe kuwasili shuleni!
 1. kudharau/kubeza
 • Mwangalie! Kichwa kama jiwe.
 1. baada ya tanakali
 • Mate yalimdondoka ndo! Ndo! Ndo!
  • Kiulizo (?)
 1. mwishoni mwa sentensi iliyo swali
 2. mwishoni mwa methali zenye muudo wa swali
 • Pilipili usiyoila yakuwashiani?
 1. kuonyesha shaka
 • Kenyatta alizaliwa mwaka wa 1945(?)
 1. kuonyesha mwaka wa kuchapishwa kwa kitabu haujulikani
 • Mlacha J (?) Tujijue Ipasavyo
  • Herufi nzito (h)
 1. kusisitiza
 • Jibu maswali manne
 1. kuonyesha wakati/njeo au hali
 • Nilicheza,Nimelima
 1. kuonyesha umoja na wingi
 • mtoto-watoto
 1. kuonyesha aina ya neno katika sentensi
 • Mtoto wake amelala (kivumishi)
  • Herufi za mlazo/italiki(h)
 1. kuonyesha aina ya kiambishi au mofimu
 • Ki-li-cho-ib-w-a (kirejeshi).
 1. kusisitiza
 • Jibu maswali mawili.
 1. kuonyesha jina la kitabu
 • Nyota ya Rehema
 1. kuonyesha maneno ya kigeni
 • Napenda
 1. kuonyesha maelezo ya vitendo vya mhusika katika mazungumzo, mahojiano na tamthilia
 • AMINA: (Akiinuka) Mama ameenda kwa Farashuu.
  • Kinyota(*)
 1. kuonyesha neno limeendelezwa vibaya
 • *kitaabu
 1. kuonyesha sentensi haina mpangilio sahihi wa maneno
 • *Kisu cha hiki ni nani?
 1. kuonyesha tanbihi (maelezo ya neno yanapatikana chini mwa ukurasa)
 • idhibati*
 1. kuonyesha sentensi ina makosa kisarufi
 • *Kuku hii ni ya nani?

 

Usemi Halisi

 • Maneno halisi kama yanavyotamkwa na msemaji.
 1. Huandikwa bila kugeuza chochote.
 2. Huanzia kwa herufi kubwa.
 3. Hunukuliwa kwa alama za usemi ambazo huandikwa zikiwa mbili mbili na moja moja katika dondoo ndogo k.m. “Mwambie ‘ugua pole’ ukimuona,” baba aliniambia.
 4. Koma hutumiwa mwanzoni au mwishoni mwake.
 5. Msemaji mpya anapoanza kusema, unapaswa kufungua aya mpya k.m.

Alimuuliza, “Huendi kwa nini?”

“Sikupewa ruhusa,” alijibu Zahara.

 1. Baada ya (?) na (!) na (.) maneno huanzia kwa herufi kubwa k.m. Lo! Unatoka wapi saa hii? Aliniuliza.

Usemi wa Taarifa

 • Ripoti kuhusu mambo yaliyosemwa na mtu mwingine.
 1. Si lazima maneno yatokee yalivyosemwa. Yanaweza kubadilishwa mradi ujumbe ubakie ule ule.
 2. Alama za mtajo, kiulizi na hisi hazitumiki.
 3. Maneno “kwamba’ na ‘kuwa’ hutumiwa.
 4. Baadhi ya maneno na viambishi hubadilika k.m.
usemi halisi usemi wa taarifa
-angu

-etu

-enu

-ako

wiki ijayo

kesho

leo

sasa

huyu

hii

ta/ki

ni

na

jana

Lo!

?

 

-ake

-ao

-ao

-ake

wiki iliyofuata

siku iliyofuata

siku hiyo

wakati huo

huyo

hiyo

nge

a

li

siku iliyotangulia

alishangaa

alitaka kujua

 

VITATE                                                                                                                                                                                    T/D

Tata

 1. hali ya kutoeleweka
 • sentensi hii ni
 1. fundo katika uzi
 • uzi umeingia tata/umetata.

Dada

 1. ndugu wa kike

 

Tua

 1. shuka kutoka angani
  • ndege ilitua
 2. weka chini k.v. mzigo

Dua

 1. maombi kwa Mungu
 • omba dua
 • piga dua –apiza/laani

 

Toa

 1. ondoa kitu ndani ya kinginea
 2. kinyume cha jumlisha

Doa

 1. alama yenye rangi tofauti na mwili wa kitu
 2. dosari/ila/walakini

Ndoa

 1. arusi/makubaliano rasmi ya mwanamke na mwanamume kuishi pamoja kama mke na mume/chuo

 

Tundu

 1. uwazi mdogo wa mviringo kwenye kitu k.v. sindano
 2. kitu maalum cha kuwekea ndege kilichotengenezwa kwa mabati, matete n.k.

Dundu

 1. mdudu anayebeba uchafu
 2. rundo la vitu /mtumba

 

Tuma

 1. peleka kitu k.v. barua kwa njia ya posta
 2. agiza mtu kufanya jambo

Duma

 1. mnyama mkubwa mwenye umbo kama la paka
 2. kamata, hasa katika vita

 

K/G                            

Kuku

 1. aina ya ndege anayefugwa nyumbani

Gugu

 1. mmea unaoota mahali usipotakiwa
 2. mmea wa mwituni mfano wa unyasi

 

Kuni

 1. vipande vya mti vya kukokea moto

Guni

 1. shairi la arudhi lililokosa kutosheleza kanuni moja au zaidi ya uandishi

 

Kuna

 1. kwaruza kwa kucha /kitu chenye menomeno

Guna

 1. toa sauti ya kuonyesha kukataa, kutoridhika, au kuchukia jambo.

 

Kenge

 1. mnyama kama mjusi mdogo

Genge

 1. kundi la watu
 2. pango/shimo

 

Kesi

 1. daawa/mashtaka yanayosikilizwa mahakamani

Gesi

 1. hewa inayotumiwa kupikia au kutiwa katika vinywaji
 2. hewa ambayo haigeuki na kuwa majimaji katika joto la kawaida

 

CH/J

Changa

 1. toa kitu ili kukusanya kwa kusudi fulani
 2. siokomaa
 3. chanja/pasua vipande vipande vidogo vidogo k.v. kuni

Janga

 1. hatari/balaa

 

Chema

 1. kizuri

Jema

 1. zuri

 

Chini

 1. kwenye ardhi/sakafu

Jini

 1. shetani/ mtu muovu

 

Choka

 1. pungukiwa na nguvu baada ya kufanya kazi

Joka

 1. nyoka mkubwa sana

 

Chungu

 1. chombo kinachofinyangwa cha kupikia
 2. kinyume cha tamu
 3. idadi kubwa (chungu nzima)
 4. mdudu mdogo wa jamii ya siafu

 

Chambo

 1. kinachowekwa kwenye mtego kunasia wanyama,samaki n.k.

Jambo

 1. habari,tukio shughuli

 

Kucha

 1. elekea asubuhi
 2. ogopa

Kuja

 1. hali ya kusogea karibu

 

Chuma

 1. pata mali
 2. madini magumu yanayotumiwa kujengea na kuundia vitu
 3. tungua matunda au maua kutoka mtini

Juma

 1. wiki
 2. jina la mtu

 

Chenga

 1. hepa kwa hila
 2. mchele uliovunjikavunjika(mchele wa chenga)

 

Jenga

 1. aka nyumba
 2. fanya madhubuti/imarisha

 

Mchi

 1. mti wa kupondea kwenye kinu

Mji

 1. makazi ya watu wengi kulikojengwa nyumba nyingi
 2. mahali kaburini anapowekwa mauti
 3. sehemu ya kati ya chupa ya mwanamke mja mzito inayounganisha mtoto na mwili wa mama

 

Kichana

 1. kitu cha kuchania nywele

Kijana

 1. mtu wa makamo mwenye nguvu/mtoto wa kiume kabla ya kubaleghe

 

F/V

Faa

 1. kusaidia
 2. kuwa vizuri

Vaa

 1. eneza kitu katika mwili ili kufunika sehemu fulani

 

Fua

 1. safisha nguo
 2. tengeneza kitu kutokana na madini
 3. toa maji katika chombo
  • fua maji
 4. Hakufua (hakufaulu)

Vua

 1. pata samaki kwa kutumia wavu, mshipi, ndoana n.k.
 2. ondoa nguo mwilini
 3. nusuru, okoa, ponya
 4. vua macho (tazama)

 

Fika

 1. wasili mahali
 2. bila shaka/kabisa

Vika

 1. valisha

 

Fuka

 1. toa moshi bila kuwaka
 2. uji wowote mwepesi (uji fuka)

Vuka

 1. enda upande wa pili

 

Fuma

 1. piga kwa mkuki
 2. ona kwa ghafla bila kutazamia mtu anayetenda jambo ovu
 3. tengeneza kitu kwa kusokota nyuzi,ukindu n.k

Vuma

 1. julikana kwa watu wengi k.v. habari, mtu n.k.
 2. toa sauti nzito v. simba,.upepo mkali,.ngoma n.k.

 

Afya

 1. hali nzuri ya mwili/siha

Avya

 1. toa mamba
 2. tumia ovyoovyo mali, pesa, n.k.

 

Fito

 1. vipande vya miti au chuma vya kujengea nyumba

Vito

 1. mawe ya thamani

 

Fuja

 1. tumia vibaya
 2. haribu mali, nguo ,chakula n.k.

Vuja

 1. pita kwa kitu mahali penye upenyo
  • Gunia hili lina

Vunja

 1. fanya kitu kigumu kuwa vipande vipande
 2. badilisha pesa ziwe ndogondogo
 3. enda kinyume na kanuni

 

Futa

 1. pangusa
 2. chomoa kisu
 3. toa maji nje ya chombo/fua maji

Vuta

 1. fanya kufuata/burura
 2. ingiza hewa au moshi mapafuni

 

Wafu

 1. waliokufa

Wavu

 1. utando wa nyuzi wa kufulia samaki,kutegea wanyama,kuweka golini/kimiani n.k

 

CH/SH

Chaka

 1. mahali penye miti iliyosongamana
 2. msimu wa kaskasi/joto na ukavu wa ardhi

Shaka

 1. wasiwasi
 2. tuhumuma

 

Chali

 1. lala mgongo juu kichwa chini
 2. mtu anayechekesha watu kwa kuwatolea mkasa

Shali

 1. kitambaa cha begani cha shehe

Shari

 1. balaa (pata shari)

 

Chati

 1. mchoro unaotoa maelezo Fulani

Shati

 1. vazi la juu la mwili lenye mikono

Sharti

 1. ­lazima

 

Choka

 1. pungukiwa na nguvu baada ya kufanya jambo kwa muda mrefu

Shoka

 1. kifaa cha kukatia na kupasulia miti

 

Chombo

 1. ala ya kufanyia kazi

Shombo

 1. harufu mbaya ya samaki

 

Chokoa

 1. tia kitu chenye ncha kwenye tundu au shimo ili kutoa kitu k.m chokoa meno

Shokoa

 1. kazi ya kulazimishwa (fanyishwa shokoa)
 2. shamba lililolimwa na kuachwa kumea nyasi

 

TH /DH

Thamini

 1. tia maanani, heshimu

Dhamini

 1. toa pesa maakamani ili mshtakiwa asitiwe korokoroni

 

Thamani

 1. kima

Dhamana

 1. malipo ya kortini

 

Thibiti

 1. kuwa ya kweli/kuaminika
  1. Habari ime

Dhibiti

 1. tia mkononi
 2. Nikidhibiti pesa zangu kutoka kwake nitanunua baiskeli.
 3. weka chini ya mamlaka

 

Ridhi

 1. kubali
 2. pendezwa na jambo

Rithi

 1. miliki kitu kutoka kwa mtu aliyekufa ama uliye na uhusiano naye
 2. pata jambo au ujuzi kutoka kwa mtu mwingine

 

A/H

Apa

 1. tamka jina aghalabu la Mungu kuthibitisha jambo Fulani

Hapa

 1. mahali karibu

 

Ama

 1. au

Hama

 • toka mahali fulani ili kwenda mahali pengine kuishi (gura)

 

Adimu

 1. -a shida kupatikana,nadra

Hadimu

 1. -mtumishi (mahadimu)

 

Ajali

jambo la madhara au hatari

Hajali

 1. kinyume cha jali

 

Auni

 1. saidia

Launi

 1. rangi

 

L/R

Lahani

 1. tuni

Rahani

 1. chumba maalum katika nyumba au chombo cha kuwekea vitu

 

Lea

 1. tunza mtoto

Rea

 1. ghadhibika

 

Lemba

 1. nyanganya kwa hila,punja

Remba

 1. pamba, rembesha

Fahali

 1. ng`ombe dume

Fahari

 1. -a kujivuniwa kwa watu

 

Mahali

 1. sehemu ambapo mtu au kitu huweza kukaa

Mahari

 1. mali au fedha inayotolewa na mwanamme kupewa wazazi wa mwanamke anayetaka kumuoa

S /SH

Saba

 1. namba inayoonyesha idadi

Shaba

 1. madini yenye rangi ya manjano

 

Saka

 1. tafuta,winda

Shaka

 1. wasiwasi
 2. tuhuma
 3. kutokuwa na hakika

 

Suka

 1. tikisa kitu
 2. pitisha kitu kama nywele baina ya zenyewe kupata mfumo fulani

Shuka­

 1. enda chini kutoka juu ya kitu
 2. kitambaa cha kujifunga kiunoni

 

Soga

 1. mazungumzo ya kupitisha wakati

Shoga

 1. jina waitanalo wanawake marafiki
 2. msenge

 

Sababu

 1. kinachofanya jambo kutokea,chanzo

Shababu

 1. kijana

 

 

J/NJ

Jaa

 1. tosha
 2. tapakaa kila mahali
 3. mahali pa kutupia taka

Njaa

 1. hali ya tumbo kutaka kupata chakula
 2. ukosefu mkubwa wa chakula

 

Chema

 1. kizuri

Jema

 1. zuri

Njema

 1. nzuri

 

Jia

 1. sogelea karibu

Njia

 1. barabara
 2. namna au jinsi ya kufanya jambo

 

Jozi

 1. vitu viwili vinavyofanana vilivyo pamoja

Njozi

 1. maono yatokeayo usingizini;ruia

 

Jana

 1. siku kabla ya leo,mwaka kabla ya huu
 2. buu la nyuki-kama kiluwiwi cha nzi

Njana-samaki mwenye rangi nyekundu

 

D/ND

Dege

 1. eropleni kubwa
 2. ndege mkubwa
 3. ugonjwa wa watoto unaosababishwa na homa kali

Ndege

 1. mnyama aghalabu anayeruka kwa mabawa
 2. eropleni inayosafiri angani
 3. ndege mbaya/mzuri (bahati nzuri/mbaya)

 

Duni

 1. kitu chenye thamani ya chini

Nduni

 1. ajabu/lisilo la kawaida

 

B/MB

Basi

 1. gari la abiria
 2. kisha

Mbasi

rafiki

 

Buni

 1. gundua
 2. unda
 3. tunga

Mbuni

 1. ndege asiyeweza kuruka lakini huenda mbio sana
 2. mkahawa au mti uzaao kahawa

 

Bali

 1. lakini
 2. sijali wala sibali (kusisitiza kutojali)

Mbali

 1. si karibu
 2. tofauti

Mbari

 1. ukoo

 

Bega

 1. sehemu ya mwili juu ya mkono na chini ya shingo

Mbega

 1. nyani
 2. manyoya ya ndege wanayojifunga wachezaji ngoma (jifunga mbega)

 

Iba

 1. chukua kitu cha mtu mwingine bila ruhusa

Imba

 1. tamka maneno kwa sauti ya mziki

 

G/NG

Gawa

 1. tenga katika sehemu mbalimbali
 2. aina ya ndege wa usiku;kirukanjia

Ngawa

 1. mnyama afananaye na paka

 

Guu

 1. mguu mkubwa sana

Nguu

 1. kilele cha mlima
 2. nguru_aina ya samaki

 

Goma

 1. kataa kufanya jambo mpaka masharti fulani yatimizwe
 2. ngoma kubwa sana
 3. duwi (aina ya samaki)

Ngoma

 1. ala ya mziki inayotengenezwa kwa kuwambwa ngozi kwenye mzinga (piga ngoma)
 2. mchezo wa kufuata mdundo wa ngoma (cheza ngoma)

Koma

 1. alama ya kituo
 2. acha kufanya jambo

 

P/B

Pata

 1. kuwa na jambo, hali au kitu
 2. kuwa kali
 • Kinolewacho hupata.

Bata

 • ndege mwenye vidole vilivyotandwa aghalabu akaaye majini

 

Papa

 • samaki mkubwa

Baba

 • mzazi wa kiume

 

Pana

 1. kinyume cha –embamba

Bana

 • finya

 

Bango

 • uwazi ulio ardhini,mtini au jabalini

Bango

 • kipande cha karatasi ngumu kama kadi
  1. bati linalozuia matope juu ya gurudumu la gari au baiskeli

 

Pacha

 1. watoto wanaozaliwa kutokana na mamba moja

Bacha

 1. tundu kwenye ukuta; shubaka(closet)

Paja

 1. sehemu ya mguu kati ya goti na nyonga

 

Pania

 1. kazana ili kufanya jambo lililokusudiwa

Bania

 1. zuia kitu bila ya kutaka kukitumia (bania pesa)

 

Pima

 1. tafuta urefu, uzito n.k.

Bima

 1. mkataba na shirika wa kulipa pesa ili kupata fidia mtu anapofikwa na hasara

 

Punda

 1. mnyama

Bunda

 1. fungu la karatasi,noti,ngozi n.k

 

Panda

 1. enda juu
 2. kifaa cha kurushia vijiwe; manati
 3. baragumu
 4. tia mbegu ardhini ili zimee

Banda

jengo kubwa la kuwekea vitu au wanyama

 

Pasi

 1. fuzu/faulu
 2. hati inayomruhusu mtu kusafiri nje ya nchi/pasipoti
 3. chombo cha kunyooshea nguo

Basi

 1. gari kubwa la abiria

Mbasi

 1. rafiki

 

T/D

Tamu

 1. enye ladha ya kuridhisha mdomo

Damu

 1. maji mekundu yanayozunguka mwilini
 2. ukoo

 

Taka

 1. kuwa na haja ya jambo fulani
 2. uchafu

Daka

 1. pokea kwa mikono kilichorushwa
 2. tunda bichi (nazi daka/danga)

 

Tokeza

 1. fanya kuonekana

Dokeza

 1. toa habari za siri kwa uchache

 

Tai

 1. ndege mkubwa mwenye makucha marefu alaye mizoga (vulture)
 2. kitambaa kinachovaliwa kwenye ukosi wa shati

Dai

 1. taka kupewa kilicho chako
 2. habari inayosemwa na haijathibitishwa

 

K/G

Kamba

 1. uzi mnene
 2. samaki mdogo
 3. mnyama wa baharini mwenye miguu mingi ambaye huliwa
 4. kata kamba (kimbia)

Gamba

 1. ngozi kama pembe ya kasa, samaki ,kasa au kobe(scales)

 

Konga

 1. kuwa mzee
 2. kusanya vitu au watu mahali pamoja (kongamano)
 3. meza maji kidogo ili kupunguza kiu (konga roho)

Gonga

 • kutanisha kitu kimoja na kingine kwa kuvipiganisha

 

Koti

 • vazi zito livaliwalo juu ya nguo

Korti

 • mahakama

Goti

 • kiungo cha mguu kinachounganisha paja na muundi

 

Mfugo

 • mnyama anayefugwa nyumbani kwa ajili ya kuliwa au biashara

Mfuko

 • kitu cha kitambaa cha kutilia vitu

 

Tegua

 1. fanya mtego usifanye kazi
 2. ondoa chombo kama chungu mekoni
 3. fanya kiungo cha mwili kifyatuke

Tekua

 1. angusha kwa kusukuma
 2. ng`oa kwa nguvu k.v. mmea

 

Mkuu

 • kiongozi
 • wenye hadhi kubwa

Mguu

 • kiungo cha binadamu au mnyama cha kusimamia au kutembelea

 

Oka

 • tia ndani ya tanuu kitu ili kiive au kikauke k.v unga uliokandwa au matofali

Oga

 1. safisha mwili
 2. enye hofu

 

Pika

 1. weka kitu k.v. chakula sufuriani juu ya moto ili kiive

Piga

 1. kutanisha vitu kwa nguvu
 2. piga chafya, maji, hodi n.k.

 

Ukali

 1. hali ya kutokuwa mpole
 2. hali ya uchungu (ladha)

Ugali

 1. chakula kinachopikwa kwa unga wa mahindi na kusongwa na maji moto hadi yakauke

Comments are closed.