MUDA: SAA 2
JINA:____________________________________NAMBARI:________DARASA:_______
1.INSHA (alama 20)
Uhalifu umejaa kitongojini mwenu,andika hotuba ya chifu wa eneo lenu kwa wanakijiji.
2.UFAHAMU
SOMA TAARIFA IFUATAYO KISHA UJIBU MASWALI YANAYOFUATA
Wanasayansi wengi wameshidnwa kuelewa ni kwa nini watu huvuta sigara jambo hili kuwa moshi wa sigara huathiri wavutaji wa sigara na watu walio karibu nao na pengine huleta ugonjwa wa moyo. Wavutaji hupatwa na kikohozi cha adaima kisichosikia dawa, maisha hupata limuewatatiza binadamu kwa karne nyingi zilizopita na kuwaacha rundo la maswali kuhusu uvutaji sigara.
sigara au sigareti ni kitu cha uraibu wa kuvuta, kinachotengenezwa kwa majani ya tumbako yaliyokaushwa. Husokotwa katika karatasi maalum. Tumbako pia huvutwa kwenye kiko hunuswa na hutafunwa.. tumbako inayosagwa na kunuswa au kubwiwa huitwa ugoro.
Hapana shaka wavutaji sigara huharibu afya yao. Wataalamu wa sayansi na madaktari wamefanya uchunguzi na wamethibitisha maradhi mfano wa pumu kutokana na moshi wa sigara unaowakereta koo. Kuna pia wanaosema kwamba uvutaji sigara unasababisha saratani ya mapafu. Watu wengi hufa kwa ugonjwa wa ghafla kwa sababu ya sumu ya moshi wa sigara ambao hutunguza na kuyatoboatoboa mapafu.
Baadhi ya wavuta sigara hutupa vipande vya sigara ovyo bila kuzimwa na hivyo husababisha hasara kubwa kama vile uchomaji wa misitu, nyumba na nguo na wakati mwingine husababisha hata vifo. Uvutaji sigara umefika kiwango cha kusikitisha, utaona vijana yaaniwasichana na wavulana wadogo sana, wakivuta sigara mbele ya watu wazima bila kujali hii ni aibu kubwa sana.
Tabia hii inatokana na mifano wanayoiona kutoka kwa wazazi wao au watu wengine. Si ajabu kumsikia mzazi akimtuma mwanawe akamununulie pakiti ya sigara au kopo la tumbako. Wazazi kama hao huwafanya watoto wavute sigara ili nao wajione kama ni watu wazima.
Sababu nyingine ya kuvuta sigara ni kutaka kujionyesha ati wana nakidi na kwao, au umaarufu. Hivyo basi sigara hazifai kupatiwa matangazo yenye kuvutia kwa vijana.
Aina nyingine ya uaraibu ni uvutaji bangi. Bangi ni aina ya mimea Fulani unaolevya na kupumbuza akili yanapotafunwa au kuvutwa. Wavuta bangi kwa hakika hupatwa na baa nyingi mwilini. Hukonda na huvaringika akili sijue wanalofanya. Wataalamu husema bangi ikiingia akilini, huharibu kitivo cha fikira mpaka mtu huwa kama mwenda wazimu.
Ni muhimu wazazi na walimu wawakataze na wawakanye watoto wasishiriki katika tabia hizi mbaya.
MASWALI
- Ipe taaarifa uliyosoma kichwa mwafaka. (alama 2)
- Taja madhara ya sigara katika afya zetu. (alama 4)
- Sababu zipi hufanya watu huvuta sigara. (alama 3)
- Taja jukumu la wazazi na walimu dhidi ya uvutaji sigara wa vijana ni lipi? (alama 2)
- Hasara gani zinazopatikana katika mazingira yetu kutokana na uvutaji sigara (alama 2)
- Fafanua maana ya maneno haya kama yalivyotumiwa katika habari hii (alama 2)
- Uraibu
- Nakidi
- MATUMIZI YA LUGHA (Alama 30)
- a) Eleza tofauti kati ya sauti hizi : (alama 2)
/r/ na /l/
b)Onyesha silabi inayowekwa shadda kwenye maneno haya : (alama 2)
- Karatasi
- Samahani
- c) Andika ukubwa wa: (alama 2)
- Mti
- Kiatu
d)Kanusha sentensi hii katika wingi: (alama 2)
Kifaru anapatikana mbugani
e)Andika sentensi zifuatazo kwa kutumia kirejeshi amba- (alama 2)
Mabondia hawa ni wale waliotuwakilisha hivi majuzi huku Ushelisheli.
- f) Eleza maana ya kiimbo (alama 2)
- g) Onyesha viambishi awali na tamati katika : (alama 2)
Uliotatizika
h)Tunga sentensi yenye sehemu hizi: (alama 2)
N+V+T+E
g)Eleza maana mbili zinazojitokeza katika sentensi hii: (alama 2)
Alimpigia mpira.
h)Andika sentensi hii katika hali ya udogo: (alama 2)
Watu wale ni weusi tititi hawaonekani gizani.
i)Sahihisha sentensi ifuatayo: (alama 2)
Musa alienda sokoni alikonunua ng’ombe mbili.
j)Eleza maana ya misemo ifuatayo: (alama 2)
- Vaa miwani
- Kula kalenda
- k) Taja matumizi mawili ya kistari kifupi: (alama 2)
l)Andika maneno yenye sauti mwambatano zenye miundo hii: (alama 4)
- I+I
- K+K+I
- K+K+K+I
- K+I+I
FASIHI SIMULIZI (ALAMA 5)
- a) Eleza umuhimu wa nyimbo
MWONGOZO
JINA:____________________________________ NAMBARI:____________________DARASA:_______
1.INSHA (alama 20)
Uhalifu umejaa kitongojini mwenu,andika hotuba ya chifu wa eneo lenu kwa wanakijiji.
a)KICHWA
Kiandikwe kwa herufi kubwa na kupigiwa mstari
Kiwe kikamilifu na cha kueleweka moja kwa moja
Neno “hotuba” lazima liwe
b)Utangulizi
salamu zikiwepo ziwe zimefuata itifaki, kuanzia vyeo vya juu hadi vya chini.
Kiini cha hotuba kitajwe.
c)Mwili
Ujumbe uelezwe kwa kina
Vipengele vya kuzingatia ni kama vile:
- Matumizi ya dawa za kulevya
- Ukosefu wa ajira
- Umaskini
- Kulipa kisasi
- Kutotendewa haki
- Kuogopa aibu na kulinda hadhi
- Wivu wa mali
d)Hitimisho
2.UFAHAMU
SOMA TAARIFA IFUATAYO KISHA UJIBU MASWALI YANAYOFUATA
Wanasayansi wengi wameshidnwa kuelewa ni kwa nini watu huvuta sigara jambo hili kuwa moshi wa sigara huathiri wavutaji wa sigara na watu walio karibu nao na pengine huleta ugonjwa wa moyo. Wavutaji hupatwa na kikohozi cha adaima kisichosikia dawa, maisha hupata limuewatatiza binadamu kwa karne nyingi zilizopita na kuwaacha rundo la maswali kuhusu uvutaji sigara.
sigara au sigareti ni kitu cha uraibu wa kuvuta, kinachotengenezwa kwa majani ya tumbako yaliyokaushwa. Husokotwa katika karatasi maalum. Tumbako pia huvutwa kwenye kiko hunuswa na hutafunwa.. tumbako inayosagwa na kunuswa au kubwiwa huitwa ugoro.
Hapana shaka wavutaji sigara huharibu afya yao. Wataalamu wa sayansi na madaktari wamefanya uchunguzi na wamethibitisha maradhi mfano wa pumu kutokana na moshi wa sigara unaowakereta koo. Kuna pia wanaosema kwamba uvutaji sigara unasababisha saratani ya mapafu. Watu wengi hufa kwa ugonjwa wa ghafla kwa sababu ya sumu ya moshi wa sigara ambao hutunguza na kuyatoboatoboa mapafu.
Baadhi ya wavuta sigara hutupa vipande vya sigara ovyo bila kuzimwa na hivyo husababisha hasara kubwa kama vile uchomaji wa misitu, nyumba na nguo na wakati mwingine husababisha hata vifo. Uvutaji sigara umefika kiwango cha kusikitisha, utaona vijana yaaniwasichana na wavulana wadogo sana, wakivuta sigara mbele ya watu wazima bila kujali hii ni aibu kubwa sana.
Tabia hii inatokana na mifano wanayoiona kutoka kwa wazazi wao au watu wengine. Si ajabu kumsikia mzazi akimtuma mwanawe akamununulie pakiti ya sigara au kopo la tumbako. Wazazi kama hao huwafanya watoto wavute sigara ili nao wajione kama ni watu wazima.
Sababu nyingine ya kuvuta sigara ni kutaka kujionyesha ati wana nakidi na kwao, au umaarufu. Hivyo basi sigara hazifai kupatiwa matangazo yenye kuvutia kwa vijana.
Aina nyingine ya uaraibu ni uvutaji bangi. Bangi ni aina ya mimea Fulani unaolevya na kupumbuza akili yanapotafunwa au kuvutwa. Wavuta bangi kwa hakika hupatwa na baa nyingi mwilini. Hukonda na huvaringika akili sijue wanalofanya. Wataalamu husema bangi ikiingia akilini, huharibu kitivo cha fikira mpaka mtu huwa kama mwenda wazimu.
Ni muhimu wazazi na walimu wawakataze na wawakanye watoto wasishiriki katika tabia hizi mbaya.
MASWALI
- Ipe taaarifa uliyosoma kichwa mwafaka. (alama 2)
Uvutaji sigara
- Taja madhara ya sigara katika afya zetu. (alama 4)
Huunguza na kutoboa mapafu
Husababisha saratani ya mapafu
Hupata maradhi ya pumu
Kufa kwa ugonjwa wa ghafla
- Sababu zipi hufanya watu kuvuta sigara. (alama 3) Kujiona wana nakidi ya pesa
Watoto huiga mifano ya wazazi wao
Hutokana na matangazo ya kuvutia
- Taja jukumu la wazazi na walimu dhidi ya uvutaji sigara wa vijana ni lipi? (alama 2)
Wazazi na walimu wa wakanya vijana kuvuta sigara
- Hasara gani zinazopatikana katika mazingira yetu kutokana na uvutaji sigara (alama 2)
Msitu huchomeka,nguo na nyumba
- Fafanua maana ya maneno haya kama yalivyotumiwa katika habari hii (alama 2)
- Uraibu-uzoefu,kupenda sana
- Nakidi- pesa taslimu
- MATUMIZI YA LUGHA (Alama 30)
- a) Eleza tofauti kati ya sauti hizi : (alama 2)
/r/ na /l/
/r/ ni kimadende na /l/ ni kitambaza
b)Onyesha silabi inayowekwa shadda kwenye maneno haya : (alama 2)
- Karatasi- Kara’tasi
- Samahani-Sama’hani
- c) Andika ukubwa wa: (alama 2)
- Mti- Jiti
- Kiatu-Jiatu
d)Kanusha sentensi hii katika wingi: (alama 2)
Kifaru anapatikana mbugani
Vifaru hawapatikani mbugani.
e)Andika sentensi zifuatazo kwa kutumia kirejeshi amba- (alama 2)
Mabondia hawa ni wale waliotuwakilisha hivi majuzi huku Ushelisheli.
Mabondia hawa ni wale ambao walituwakilisha hivi majuzi huku Ushelisheli.
- f) Eleza maana ya kiimbo (alama 2)
Kupanda na kushuka kwa mawimbi ya sauti
- g) Onyesha viambishi awali na tamati katika : (alama 2)
Uliotatizika
U-li-o viambishi awali
i-ka viambishi tamati
h)Tunga sentensi yenye sehemu hizi: (alama 2)
N+V+T+E
Mwanafunzi bora alituzwa jana. (mwalimu akadirie mifano zaidi)
(mwalimu akadirie miundo ingine mwafaka)
g)Eleza maana mbili zinazojitokeza katika sentensi hii: (alama 2)
Alimpigia mpira.
Alipiga kwa niaba yake
Aliupiga mpira kwenda upande wake
h)Andika sentensi hii katika hali ya udogo: (alama 2)
Watu wale ni weusi tititi hawaonekani gizani.
Vijitu vile ni vyeusi tititi havionekani gizani.
i)Sahihisha sentensi ifuatayo: (alama 2)
Musa alienda sokoni alikonunua ng’ombe mbili.
Musa alienda sokoni alikonunua ng’ombe wawili.
j)Eleza maana ya misemo ifuatayo: (alama 2)
- Vaa miwani- kulewa
- Kula kalenda- Fungwa jela
- k) Taja matumizi mawili ya kistari kifupi: (alama 2)
kuandika tarehe km 03-03-2021
kuonyesha neno linaendelea katika mstari unaofuata
kutenga silabi na nyingine hasa katika ufunzaji wa Ushairi
kutenga neno au sentensi na ufanunuzi
(mwalimu akadirie maelezo na mifano)
l)Andika maneno yenye sauti mwambatano zenye miundo hii: (alama 4)
- I+I-oa
- K+K+I- m-cha
- K+K+K+I-mbwa
- K+I+I-kaa
FASIHI SIMULIZI (alama 5)
- a) Eleza umuhimu wa nyimbo
Kuburudisha
Kukejeli
Kuasa
Kupata riziki
Kuhifadhi na kuendeleza utamaduni
Kutimiza shughuli mbalimbali